Wakuu Salaam..
Imependezwa tena kwa siku ya leo kuanza kupata mwanga kidogo kuhusiana na masuala yanayoendelea katika nchi yetu ikiwemo uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwenye shirika la ndege la ATCL... Pia kule bandari napo tumeona hali siyo shwari.
Hatujui kesho maeneo mengine hali itakuwaje kwenye miradi mikubwa ya SGR,Bwawa la kufua umeme la Mwl Nyerere, mabasi ya mwendokasi, madaraja na barabara.
Itoshe tu kusema Mh Rais kachagua njia sahihi ya kuwaonesha watanzania hali halisi ya nchi yetu ili tujue wapi tulipotoka, tulipo na kule tunapotaka kuelekea.
Kipindi cha aliyekuwa mtangulizi wake mara nyingi haya mambo tulifichwa na hawahawa ambao leo wameanza kusema kweli ya hali halisi, hatujui ni kwamba mambo yamebadilika ghafla au wamesoma upepo.
Tunakuomba Mh Rais kwa sasa usimuhakikishie mtu yeyote kuendelea na wadhaifa wake serikalini wala usimtumbue yeyote. Cha kufanya wape muda waweke mambo yote hadharani, baada ya hapo wewe sasa ndio uchuje nani wa kwenda nae.
Kila la kheir.