Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Umoja ni ngumu pale tunapozuia habari za taifa au za wananchi zisitolewe.
 
ufuatiliaji wa makini kwa kila jambo ni muhimu sana, wasiridhike na taarifa za kuletewa yawapasa wajiongeze. hii nchi ina wapiga dili wengi sana kuliko waadilifu.
wasikubali kuendeshwa na kikundi cha watu wacheche.
Masilahi ya wananchi wengi ndio yawe namaba moja.

viongozi wetu wasisikilize majungu na fitina kisha wakafanya maamuzi bila kujiridhisha ni hatari sana,

tusikubali kuyumbishwa au kuendeshwa na mataifa ya nje, yatupasa tuwe imara.

tuchukue hatua haraka kwa wale wote amabao sio waaminifu na waadilifu,
pia tuwa baini na tuchukue hatua kwa wale wote wanao taka kuhujumu jitihada za serikali kwa wananchi, nk
 
Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1. Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2. Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa
3. Futa Mpango wa kujenga Daraja la Mwanza la ziwani....
Wivu tu unakutesa kwani Chato sio sehemu ya Tanzania.Sema tufute ya yaliyopo Mkoa wa Kilimanjaro
 
Nimefuatilia surprise ya mama Samia, hakika kauli na matamko ni ya Mama Samia ila sauti unaweza kupachika ya late Pombe Magufuli.

Wale waliokuwa wanasubiri wali wa nazi kwa ubwabwa naona tunaenda kula dona kwa dagaa asubuhi asubuhi.
Hakuna kulala, kazi inasonga.
 
Kati ya ubalozi wa Japan na ubunge ni kipi kina maslahi zaidi? Tuanzie hapo kwanza
 
Dkt. Mpango najua wewe ni mchumi hasa na mbahili mno waliofanyakazi nawe hiyo sifa wanakupa. Na sifa ya mbahili ni kujali na kuipenda hela yake ama kipato chako. Sasa nakushauri kwa nguvu uliyo nayo hivi sasa fukuza hao mchwa waliofukuzwa na CDM.
 
Tumia kauli nzuri hao ni binadamu na hizo ni siasa tuu hata hazieleweki ujue...uzi ukikosa staha unakua hauna maana
 
Rais na makamo wake wana mambo mengi ya maana ya kufanya.
Hayo maombi yako mwambie Ndungai a.k.a Chuma kikoli moto.
 
Nilichojifunza kwa Rais Mama Samia anasikiliza maoni ya wananchi
Toka Mama Samia ameingia madarakani
Anatembea kwenye laini ya maoni ya wananchi
Kama mama akiendelea hivi hivi atafanikiwa sana kwenye uongozi wake
Ushauri wangu kwa mama samaia awaepuke sana watu wanaotumia neno mimi na awapende sana watu wanaopenda kutumia neno sisi
Mama awakatae watu wanatumua neno mimi
Awaepuke sana watu wanaosifia kila jambo awaepuke sana watu wanaopenda umimi
Hayati Mkapa alishakemea sana watu wanapenda kutumia sana mimi
 
Wananchi wana maoni tofauti tofauti na maono yake.Kama maono yanafanana na maoni ya wananchi atapita humo vinginevyo haitakuwa rahisi KWA kiongozi yoyote kufanya kazi kwa kufuata maoni ya wananchi wake tu
 
Back
Top Bottom