Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Najua maana ya jina Suluhu. Mwenye kujua maana ya jina Samia anisaidie. Names matter.
 
Hayati alifanya maendeleo ya miundombinu na kuboresha njia za kuongeza pato la taifa, lakini kuna mambo ya kikatiba ambayo yanalenga maendeleo ya mtanzania mmoja mmoja hayati hakuyatekeleza ila aliahidi kuyatekeleza kabla hajatoka madarakani.

Mambo hayo ni -ajira, kuboresha maslahi ya watumishi, kuondoa kodi kandamizi! Je, mrithi atayatekeleza hayo? Au atayapuuza kama hayati?
 
Moja ya kazi kubwa iliyopo mbele ya Mhe. Rais ni kusoma majalada. Hii Ni ka i ngumu kwake kwa sababu mengi ya majalada hayo tayari yapo hatua yakutiwa sahihi, kukataa kutia sahihi au kutia sahihi ni Jambo linalohitaji kutulia na kufanya consultation nyingi sana

Kazi inakuwa ngumu kwa sababu zipo kazi nyingi chini ya Rais ambazo hazimuusishi Makamu wa Rais na hivyo yeye hakuwahi kuzifanya.

Lakini pia kiongozi aliyetangulia akuwa na safari za nje na hata wakati wa mapumziko aliendelea na kazi hivyo yawezekana kabisa kwa miaka mitano iliyopita madaraka na ofisi ya Rais hailuwahi kukasimia kwa Makamu wa Rais.

Kwa mantikii hiyo, mwanzo wa utawala wa Mama usionekane Kama mwanzo wakujificha ofisini na kutoonekana na tusiishi kwa kuamini kwamba kuwa Makamu unakuwa na uelewa wa kinachoendelea ofisini kwa Rais la. Ni maamuzi ya Rais aliyepo kukushirikisha au kutokukushirikisha. Hii dhana ndiyo iliyopelekea kwa miaka mingi Makamu wa Rais kuonekana kama mkata utepe.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ni mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Tanzania.

Ni mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa rais wa Tanzania.

Ni makamu wa kwanza wa rais kuwa rais.

Ni rais wa kwanza kuchukua madaraka baada ya kifo cha aliyekuwa madarakani.

Mwanamke wa kwanza rais toka Visiwani.

Ni rais wa kwanza toka visiwani hasa ikizingatiwa kuwa mzee Mwinyi ni mtoto wa kivure hivyo mbara.

Mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa wa mwenyekiti ya tume ya kukusanya maoni ya kubadili katiba.

Je, yawezekana akawa rais wa kwanza kuchaguliwa rais?

ONGEZA REKODI NYINGINE IUJUAYO AU UIONAYO.
 
Rais wa kwanza kumuumbua Marehemu Rais mbele ya wananchi wake.

Mi bado naiwaza ile ya Marehemu kutengeneza sinema ikulu kupokea hundi ya gawio la ATCL baada ya kutuaminisha shirika linatengeneza faida, kufikia hatua likapewa tuzo kabisa kulizidi shirika la Turkey Airlines.

Na ya kutuaminisha utawala wa Marehemu Rais ulikua hauna ufisadi kabisa, mara paap TPA yamezuka yakuzuka.

Na za chini ya kapeti Waziri Wa Madini kuihujumu Mirerani kwenye kutorosha madini ya Tanzanite kwenda kwa jirani yetu fulani hivi aliokua anatua Arusha kitalii.
 
Sioni shida kabisa mwanamke kupewa kitengo.

Wanawake wengi sana wana sifa za kazi hizo.

Kuanzia sasa mama anapoteua ahakikishe teuzi nusu ni wanaume na nusu ni wanawake.
 
Sioni shida kabisa mwanamke kupewa kitengo...
Sasa mbona unaendeleza yaleyale.

Kwa nini iwe nusu/nusu; kwani haiwezekani kuwa wanawake zaidi ya wanaume?

Mbona huko nyuma iliwezekana wanaume kuwa wengi zaidi ya wanawake.

Inaonyesha bado huamini wanawake kushikilia nafasi hizo?
 
Pole na kazi mama za ujenzi wa taifa nikiwa Kama mtanzania mwenye kulitakia taifa maendeleo mapendekezo ya waziri wetu wa fedha hapo naomba nikushauri watu 3
Professor Asad
Dct dau
Chares kimei

Hawa watu ni vichwa sana kwenye sector ya fedha na hazina kubwa Sana kwa nchi yetu hayo ni mawazo yangu tuuu Kama itakupendeza.
 
Kama kweli tunataka kumuenzi Hayati Magufuli Uongozi uliopo Uendeleze Kununua MADEGE Mengi zaidi kama Hayati alivyotuahidi .kutokufanya hivyo tutakuwa hatujamtendea Haki.Hayati alitamani Tanzania iwe Kama ULAYA,alitamani Dar iwe kama DUBAI Shime Tuyatekeleze TANZANIA ni TAJIRI sana.
 
Pole na kazi mama za ujenzi wa taifa nikiwa Kama mtanzania mwenye kulitakia taifa maendeleo mapendekezo ya waziri wetu wa fedha hapo naomba nikushauri watu 3
Professor Asad
Dct dau
Chares kimei

Hawa watu ni vichwa sana kwenye sector ya fedha na hazina kubwa Sana kwa nchi yetu hayo ni mawazo yangu tuuu Kama itakupendeza.
Dau ni mwizi hafai, mama usithubutu kuleta jizi lililofisadi NSSF.
 
coat-arms-tanzania-vector-840858.jpg

MH. RAISI MAMA SAMIA SULUHU UKITAKA UTUPE MAENDELEO YA KWELI KWA 100% BAS TUMIA HII NEMBO KATIKA UTENDAJI WAKO WOTE.

NAKUTAKIA KAZI NJEMA.
 
Umoja ni ngumu kuupata kwenye Taifa ambalo kila mtu anajifanya ana akili ya kumpangia raisi jinsi ya kufanya majukumu yake.
 
Back
Top Bottom