Mh Rais Mama Samia, ombi kubwa kwako ni kutoa tamko la kudhibiti ugonjwa wa covid19 (Corona) na pia kukubali kuagiza chanjo (Vaccine).
Mh. Rais, mahospitali yote nchini yamejaa,wengi ni wale wanaougua ugonjwa wa kushindwa kupumua na tatizo ni ukosefu wa vifaa vya upimaji kama huu ugonjwa ni upi haswa.
Lakini madaktari wengi wanatudokeza kuwa wapendwa wetu wanaogua wana kila dalili za covid 19.
Tunaomba tuige wenzetu kwa kuweka hatua za kudhibiti ugonjwa huu na kuwaruhusu mahospitali yote, hasa ya binafsi kuingiza nchini chanjo,chini ya uangalizi wa Wizara ya Afya na Vyombo Vingine Husika.
Tuhamasishe kuvaa barakoa,kupiga marufuku mikusanyiko,maharusini,misibani,mpirani n.k,kunawa mikono,sehemu za ibada za Wakristo na Waislamu ziwe na utaratibu wa Waumini kukaa mita 2 kati yao(Distancing)n.k.
Sie Mh Rais tunaishi duniani kama nchi nyingine. Sote kwa pamoja tuupige vita ugonjwa huu hatari.