Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mabibi na mabwana mama Samia Rais wetu ni wa kupongezwa sana na watanzania wote.

Huu ni muda wa kuita sepeto kwa jina lake.

Jambo lolote lisilo na faida na liitwe kwa jina lake.

Watanzania sisi ni masikini mno kukumbatia hasara, kumkumbatia yeyote, mradi wowote, mashirika au hata taasisi yoyote inayotutia hasara.

Mbadhirifu yeyote hata kama ni rafiki yake nani, huyo naye ni mwiba mchungu kwa ustawi wa taifa letu.

Jamani sote tumsaidie mama hata kama sisi wenyewe ndiyo wahusika wakuu kwenye kumbebesha mtanzania mizigo hii mizito mtanzania huyu maskini isiyokuwa na sababu.

Au nasema uongo ndugu zangu wa pale TPA, ACTL, TANROADS, TANESCO, TRL, na wote kokote mlipo?

Hivi haswa ndiyo vita vya kiuchumi. Kuvipigana si rahisi lakini penye nia ipo njia.

Sambamba na hili tunasubiria pia vita ya kurejesha haki na usawa. Kwa pamoja, tutafika tu.

La kuwalinda wakosoaji tumelisikia na kulipokea kwa mikono miwili. Kukosoa ni uzalendo. Wakosoaji hawa wamedhihiri kwa vitendo dhidi ya wanafiki kuwa hii nchi wanaipenda na ni wazalendo kweri kweri.

Kusema kweri kwa jana tu umetupa tabasamu la kutosha. Tayari harufu ya Tanzania isiyokuwa na wakimbizi ugenini inaanza kunukia.

Udumu mama Samia Suluhu Hassan rais wetu wa JMT.
 
Uko Tanzania mkuu? Una-account ajira portal ambayo iko chini ya sekretarieti ya ajira(utumishi)?
Ajira zote zinapatikana kwa interview, tena kuanzia interview mbili au tatu na hata nne kutegemeana na idadi ya waombaji.
Nashuhudia kama interviewee kwamba hamna undugu wala kujuana ni uwezo wako utakaokubeba.
Tembelea link zifuatazo kwa msaada zaidi;
1. Recruitment Portal
2. https://www.ajira.go.tz/
 
Unaishi wapi wewe jamaa yanguu,vijana wamejazwa mashirika ya umma bila hata interview
Labda waliingia kabla ya magufuli...mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Kila shirika, kada na taasisi baada ya 2015 wote walikuwa wanatoa nafasi wazi kupitia ajira portal.
 
Yaani mkurugenzi nimepewa kibali cha kuajiri , nimwache mtoto wa kakaangu niliyemsomesha mwenyewe.
 
Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1. Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2. Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa
3. Futa Mpango wa kujenga Daraja la Mwanza la ziwani
4. Ondo miradi ya Maendeleo ya maji chato
5. Ondoa makao makuu Dodoma, na turudi Dar
6. Futa strogiers gourge..tuendeleze gas na tuwape makampuni binadsi kuzalisha umeme ili tupate ajira zaidi
7. Futa SGR ili hera ziendele kwenye maendeleo ya watu na siyo ya vitu
8. Fut mambo ya EFD kwani yanasababisha biashara kusinyaa.
we kiazi kweli
 
Labda waliingia kabla ya magufuli...mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Kila shirika, kada na taasisi baada ya 2015 wote walikuwa wanatoa nafasi wazi kupitia ajira portal.
Sio kweli ,baada ya 2015 ndio upuuzi wa kuhamishia wafanyakazi toka halmshauri kuja kwenye mashirika ya umma ndio ulishamiri
 
Hakika mheshimiwa Rais umeanza kazi si kwa kishindo bali kwa haiba ambayo nimebahatika kuwashudia marais wa awamu kuanzia ya pila hadi leo hawakuwahi kuwa nayo .Kukubalika kwako na makundi yote iwe ndio fursa pekee ya kuhakikisha swala kuu kwa vijana linatatuliwa ingawaje kulimaliza ni ngumu kwani duniani kote ajira ni tatizo .Wakati wa utawala wa JK ajira sio kwamba zilikuwepo za kumwaga bali ni njia zilizotumika kujaza ajira serikali ndio iliyoonekana kuwa serikali kwa wakati huo ilikuwa inatoa ajira.Sifa kuu ya kupata ajira ilikuwa ni kwa njia ya ushindani na aliekosa ajira aliamini kuwa nafasi alikosa baada ya kufeli kwenye usaili.Piga marufuku ajira ambazo hazifuati utaratibu wa ushindani (interview)
Ajira za Serikali hazina ushandani, wanaofanya kazi serikalini na wahitimu wa vyuo Tanzania kwa 90% ni wako chini ya viwango
 
Well..ni sudden...hakutarajia kushika kijiti

Na kama mjuavyo kuwa serikal inabid uijue kiundan kila chocho kila kona ndio utakua unaweza cheza nayo kama unapeta mchele kwenye ungo

Bado hayuko detailed sana sababu ya ugafla wa kiti ..ila nawahakikishia huyu mama kadiri siki znavyoenda atayajua mengi....na atawadaka wengi

Na atawachinja weng kwa tabasamu sababu ameonyesha tayar kutembea mule mule na hatotaka wa disapoint wananchi na dunia

Atataka onyesha kuwa mama anaweza..mwanamke anaweza

Nimeandika ki layman na kwa uharaka kdogo

I just felt like talking to myself..thinkin out loud nilipoiskiliza hotuba yake tena kwa mara ya pili asubuh hii

Msimchukulie poa mama la mama..Mama presidaa
 
Tujikumbushe kwa JPM wakati anamrithi JK, watu walibet vipi. Pia hata atayefuata watasema hivihivi
Hakuna cha kubet! JPM alirithi nchi ikiwa pazuri sana hasa kiuchumi. Alitakiwa kurekebisha machache sana ili aendane na kasi ya JK kiuchumi. Kwa kifupi kwenye uchumi JPM ameharibu kupita maelezo.
 
Mimi Johnthebaptist naomba mh Rais Samia Suluhu Hassan aunde Baraza lake la mawaziri ili tuweze kuipima na kuitathmini serikali yake kwa haki.

Anaweza kuwarejesha mawaziri hawa hawa kama anaridhika nao ila iwe wameteuliwa na yeye mwenyewe badala ya kuwa amewarithi.

Ndugu mdau wewe una ushauri gani mahsusi kwa Rais mpya wa JMT mh Samia Suluhu Hassan?

Kila zama na kitabu chake!
 
Ushauri awafute kazi Mwigulu, Bashiru, Olesabaya, DPP, Mkumbo, Ndalichako, Jafo, Kabudi, Gwajima na timu yake yote wizara ya afya, RC Mbeya, Mambosasa, RPC Dom n.k
 
Ushauri wangu kwake!
Atukumbuke walimu tusio na ajira kusudi tukalisaidie taifa katika upande wa elimu!
Hilo tu sina lingine!
 
Back
Top Bottom