Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Waliokuwa wanashiba "usaha" wanaogopa vyakula halali vya shamba!

Inabidi mjilazimishe kukubali tu! Imeisha hiyo, mama ameshakuwa!!!

Ikibana chomoa!
 
mkuu kuna watu wanawashwa sana,sasa mama kamkosea nini mpaka anakuja kuwanga humu kwa wenye akili.
 
Aisee Mama kweli kawakamata pabaya, jinsi hiz nyuzi za kumponda mnavyozitirisha...! Mngejua humu ndani asilimia kubwa ya watu walikuwa hawamkubali hayati, you are barking at the wrong tree. Kama wewe ni mwanachama mwenye akili ni vizuri uendane na upepo ulioko sasa au subiria cha moto.
 
Hata ukipata coach Mpya kwenye timu upangaji na formation hubadilika.
 
Humu ndani wenye akili wamebaki wachache sana! Sio kama zamani[emoji18][emoji18]
 
Yes ni ccm tena wale magufuli kindakindaki, wanataka sera ya mwendazake iendelee kutawala wanashindwa kujua kwamba huu ni utawala mpya
Yani sijui wanataka aendelee kuwa kama VP wakati sasa hivi ni raisi
 
Na Woinde Shizza, Michuzi Tv

Uongozi shule za BLESSINGS MODEL SCHOOL MWANZA NYASAKA pamoja na BLESSINGS DAY umempongeza Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Samia Suluhu kwa kuanza vizuri kazi yake na kukubalika na makundi yote katika jamii ya watanzania.

Pongezi hizo zimetolewa na muwekezaji wa shule hizo ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi Mwl.Ezekiel Eliphas Meivule Mollel ambapo alimuahidi Rais Samia kumpa ushirikiano wa asilimia zote katika sekta ya elimu.

Aidha pia alisema kasi aliyoingia nayo Rais Samia ni nzuri na anauhakika kabisa itaweza kuivusha nchi ya Tanzania , na kuwafikisha watanzania mbali zaidi katika swala la Maendeleo ukizingatia nchi yetu ina vitega uchumi vingi.

Aliongeza kuwa wataendelea kumuweka katika maombi yeye na viongozi wenzake wa serikali ili waweze kuyatekeleza yale yote ambayo amekusudia kuwafanyia watanzania ikiwemo kumaliza miradi yote mikubwa iliyoachwa na hayati John Magufuli pamoja na kuwaletea maendeleo ya nchi pamoja na mtu mmoja mmoja.

Alisema wanaona azma ya Rais Samia ya kuongeza mawanda ya ukusanyaji wa kodi pamoja na kusaidia katika kuleta Maendeleo ya nchi .

Aidha alimpongeza Rais kwa kuweza kuongeza ajira kwa walimu 6000 ambao wapo mtaani na kusema kuwa hii itadaidia kuboresha elimu yetu iendelee kuwa bora zaidi,pia alipongeza mikakati mipya aliyoitagaza ikiwemo kuhamasisha uchimbaji wa madini

Aliwapongeza watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kutunza amani na mshikamano wa nchi yetu ,ambapo aliwasisitiza watanzania kuendelea kumuenzi hayati Rais John Magufuli ambaye aliwaonyesha watanzania njia ya kuthubutu kwamba wanaweza wakafanya mambo yakaenda sawa.

Alibainisha kuwa jamii yenye ufahamu wa kutosha juu ya wajibu wake katika utawala bora, demokrasia na haki za binadamu, ni jamii inayowajibika na inayoshiriki.

kikamilifu, na kwa hiari katika masuala mbalimbali ya ujenzi wa taifa.

Mwisho.

Picha mwekezaji wa shule za BLESSINGS MODEL SCHOOL MWANZA NYASAKA pamoja na BLESSINGS DAY
zilizopo mwanza ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi Ezekiel Mollel akiongea na michuzi Tv

 
Madam president, please, mpe NAPE NNAUYE wizara ya mambo ya ndani, ataimudu ipasavyo,na pia atawanyoosha hawa Mataga na sukuma Gang wanaoleta ziaka na matusi juu ya mamlaka
 
Madam president, please, mpe NAPE NNAUYE wizara ya mambo ya ndani, ataimudu ipasavyo,na pia atawanyoosha hawa Mataga na sukuma Gang wanaoleta ziaka na matusi juu ya mamlaka
Hahahaha Nape zama zako zimepitwa mzee.
 
Mama SASHA tunaomba uvae mamlaka yako ya kwamba wewe ni Amiri Jeshi mkuu nguvu uliyonayo wewe hapo imetoka kwetu wananchi sisi ndio waajiri wako tunataka ututumikie

"Mama anasema najua kipindi cha miezi minne hadi mitano mapato yatashuka na baadae tutapanda😀,,mama unawapatia wezi chance hadharani,yaani watakusanya Trilion 1.5 watakwambia wamekusanya Trilion 1,cha juu wanapiga kisha watakujibu mhe Rais tunategemea kwa mfumo tunaoenda nao tutaanza kupanda baada ya miezi 6.!"

Hayati aliwahi kusema nchi hii ni tajiri na huo ndio ukweli.

litafakari upya suala la kodi
 

Naamini kwa kauli yako hujawahi kuanzisha biashara, kampuni wala jambo lolote la kimaendeleo kwenye jamii yako zaidi ya kukaa kusubiri mshahara.

Hujui vilio vya wafanyabiashara na watu wanaoporwa mali zao na aina ya dhulma zinazofanyika. Endelea kukaa kula matunda ya fedha za wengine zilizokupa uhuru wa kutyoe usiyoyajua.

Angalia tax rate ya nchi yeyote iliofanikiwa kukua kwa kasi kubwa ni kiasi gani kisha tafakari kwa nini nchi kama Tanzania ina corporate tax ya 30% !! Kushusha kodi na kuencourage biashara ndo njia pekee ya kuingiza mapato sio kupiga mdomo kwa mambo usiyo na elimu nayo.

Angalia nchi za Afrika zenye maendeleo yaliochochewa kutoka ndani kama Mauritius, kisha angalia kodi zao na uhuru wa biashara. Kodi zipo juu nchi hii na dhulma zimezidi kiwango na bila kutatua hili tutabaki masikini
 
Sukuma Gang si mkae pembeni mtulie.

Huo utaalamu wa kodi mmetoa wapi!?

Kalimeni pamba huko Misungwi acheni kutupigia kelele.
 
Kila mfalme na zama zake, afanye shughuli nyingine sasa ubunge unamtosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…