Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Asalaam aleykhum wanajukwaa !

Ndugu zangu,tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Mwl.John Magufuli hali kadhaa za wasiwasi wa madaraka ziliibuka hasa kwa viongozi waliokuwa wakinufaika na utawala wake.

Wanufaika hawa walijaribu na walitudanganya kuwa Rais alikuwa ni mzima na akichapa kazi kwa kwenda mbele.Lakini pia wanufaika hawa walitengeneza wingu zito liliotaka kupoka madaraka ya yule aliyestahili kuwa Rais baada ya kifo cha mtu wao kwa kushirikiana na vyombo kadhaa na maafisa kadhaa wa ulinzi na usalama.Jaribio hili la kutaka kufanya uhaini wa kumpindua aliyestahili halikuwa siri!
Baada ya jaribio lao kuwa limeshindikana wameanza mkakati mpya wa kumlazimisha Rais Mama Samia H Suluhu aendeleze mambo ya hovyo ya mtangulizi wake kwa kuwa wao wananufaika moja kwa moja na mambo haya.

Baada ya ripoti ya CAG kuwekwa wazi,mambo mengi ya mtangulizi wa Rais Mama Samiah H Suluhu yameonekana kuwa ni kichaka cha hasara na watu kupiga pesa za walalahoi mathalani Ndege,Reli ,Bwawa,Stendi za basi n.k na si siri kabisa ni hasara kubwa kwa taifa letu.

Kikundi hiki ambacho wanakikundi wanashikilia nyadhifa za kiserikali wameenda mbali zaidi na kuwataka kwa lazima wale wote wanaomsema vibaya mwl.Magufuli bila kujiuliza yeye binafsi amelitendea taifa uzuri gani wenye tija tofauti na yale mabaya yanayofahamika.

Kikundi hiki kimejipanga.Ndiyo,kimejipanga kumng'oa Rais kwa kutengeneza msingi wa kitokuwa na imani naye kwa kuwa yeye(Mh.Rais Samia H Suluhu) hayuko tayari kuyaendeleza yale aliyokuwa akiyafanya Mwl.Magufuli.

Ni jambo la hatari sana Spika wa Bunge letu,Waziri Mkuu,DGS wa TISS,Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanapokuwa tayari kumlazimisha mama awe kama baba yao.

Niseme tu kwamba,Rais Samia H Suluhu hayuko salama kama watu hawa wanahamasisha uhaini na chuki dhidi yake.Hayuko salama !
Ninamuomba Rais na Amirati Jeshi Mkuu wa nchi yetu Mh.Samia H Suluhu atengue uteuzi wa waziri Mkuu na alivunje Bunge turudi kwenye uchaguzi.Wabunge waliopo Bungeni hawajatokana na ridhaa za watanzania bali ilikuwa ridhaa ya Mwl.Magufuli,Polisi,Tume,na TISS ! Si jambo geni katika siasa za ulimwengu huu tukirudi kwenye uchaguzi.

Angalizo,Uchaguzi hautakuwa huru na wa haki iwapo hapana TUME HURU YA UCHAGUZI TANZANIA.

Mwanzo ni mgumu lakini tutafika na tutaweza.

MATHA.
 
Watu unaodhani wapo na wewe hawapo na wewe,hilo ni kundi lenye itikadi ya mrengo wa kushoto. Ni kundi Toxic,lililoathiriwa na fifth phase administration,ni kundi linaloamini Tofauti na unavyoamini wewe.

Hata namna unavyoendesha Serikali hili kundi linakupinga kimya kimya, Report ya CAG wanaamini imelenga kumchafua Hayati, wanaamini wewe ulikuwa kinyume na Hayati ndo maana CAG kaanika hayo madudu.

Kwanza hawaamini kuwa kifo cha Magufuli ni kazi ya Mungu bali wanaamini kuwa kuna hujuma imefanyika. Hili ni kundi ambalo baadhi yao wengi Tu umewapa vyeo vikubwa.

Baadhi yao wanadiriki kusema kuwa wewe siyo CCM halisi,Eti utakuwa CHADEMA ,yote hii hawataki wala kusikia Hayati anakosolewa.
Walimuona mungu mtu asiyeweza kukosea lolote.

Hawa ndo wanajipanga kuusaka Urais 2025, ndo hawa hawa waliokuwa wanakupiga majungu usifike ili usifike hapo ulipo.
Wataalamu wa ujasusi wana slogan yao inasema,"once an enemy always an enemy".

Usitarajie hao watu wakakupenda au kukuunga mkono, Kwanza hapo walipo wamechanganyikiwa,hawajui la kufanya,hawana uwezo tu kwa sababu upo juu yao.

Ushauri wangu kwako, ni huu:
1.Ifumue TISS yote kuanzia DGS hadi chini yaani from the Top to the Bottom.
2.Teua mawaziri wapya wote sambamba na wakuu wa mikoa na wilaya.
3.Usipuuze mawazo ya wapinzani
MUHIMU
CDF aendelee kuwa Mabeyo,na hata muda wake ukiisha mwongezee,na zaidi ya yote huyu mzee mwongeze mshahara,anakufaa sana,IGP hana shida yoyote pia.
Message sent and Delivered
 
Hadithi ya kuambiwa changanya na akili zako, toka lini Mama akawa "saccos" au ndio mnataka kumghilibu awaone nyinyi ndio wakombozi wake .
 
Ya ushauri mzuri mkuu, nafikili we ni Kati yetu ambaye mungu,kaamua kukufungua ili kufikisha ujumbe muhim KWA wahusika, thanks
 
Hana la kufanya sababu CCM ndiyo imemuweka hapo
 
Poleni sana wafuasi wachache mlioneemeka na utawala mbovu wa marehemu
 
Haya unayoongea yana ushahidi upi au ni just wishful thinking?
 

πŸ€” πŸ€” πŸ€” πŸ€” πŸ€” (Very likely and well thought !!!!!)
 
nakubaliana na mawazo ya mtoa hoja. Kinacho niuma mimi ni pale ambapo wabunge wanajadili masuala bungeni wakisahau kuwa wapo awamu ya sita na siyo ya tano. Nuhimu kuliko yote ni kufumua mfumo mzima wa ulinzi na usalama. Mle ndani kuna watu waadilifu na wacha Mungu. Bahati mbaya sana kuna watu walipenda shortcut kwa kutegemea kulindwa na mtu hao hawatufai hata kidogo. Mabeyo ni mcha Mungu atakusaidia, viongozi wadini na watanzania watukuembea usiku na mchana na mama yetu mpendwa utavuka salama. Kaa karibu na pinda ni mzalendo wa kweli na atakushauri vizuri. Usimuache mze butiku, Mzee Mkama, Mzee warioba, Mzee Lowassa, Mzee Karume, Mzee wasira hawa wana busara nyingi sana na wanaifamu historia ya nchi vizuri. Mwenyezi akulinde akujaliye afya njema na siku nyingi zenye kheri.
 
Kweli wapinzani wa Tanzania wamebanwa wakabanika kweli kweli
 
Wewe unamtega, asikilize wapinzani? Kwani wao hawataki kwenda ikulu 2025? Acha upuuzi wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…