MANYORI Jr
JF-Expert Member
- Mar 25, 2012
- 462
- 343
Asalaam aleykhum wanajukwaa !
Ndugu zangu,tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Mwl.John Magufuli hali kadhaa za wasiwasi wa madaraka ziliibuka hasa kwa viongozi waliokuwa wakinufaika na utawala wake.
Wanufaika hawa walijaribu na walitudanganya kuwa Rais alikuwa ni mzima na akichapa kazi kwa kwenda mbele.Lakini pia wanufaika hawa walitengeneza wingu zito liliotaka kupoka madaraka ya yule aliyestahili kuwa Rais baada ya kifo cha mtu wao kwa kushirikiana na vyombo kadhaa na maafisa kadhaa wa ulinzi na usalama.Jaribio hili la kutaka kufanya uhaini wa kumpindua aliyestahili halikuwa siri!
Baada ya jaribio lao kuwa limeshindikana wameanza mkakati mpya wa kumlazimisha Rais Mama Samia H Suluhu aendeleze mambo ya hovyo ya mtangulizi wake kwa kuwa wao wananufaika moja kwa moja na mambo haya.
Baada ya ripoti ya CAG kuwekwa wazi,mambo mengi ya mtangulizi wa Rais Mama Samiah H Suluhu yameonekana kuwa ni kichaka cha hasara na watu kupiga pesa za walalahoi mathalani Ndege,Reli ,Bwawa,Stendi za basi n.k na si siri kabisa ni hasara kubwa kwa taifa letu.
Kikundi hiki ambacho wanakikundi wanashikilia nyadhifa za kiserikali wameenda mbali zaidi na kuwataka kwa lazima wale wote wanaomsema vibaya mwl.Magufuli bila kujiuliza yeye binafsi amelitendea taifa uzuri gani wenye tija tofauti na yale mabaya yanayofahamika.
Kikundi hiki kimejipanga.Ndiyo,kimejipanga kumng'oa Rais kwa kutengeneza msingi wa kitokuwa na imani naye kwa kuwa yeye(Mh.Rais Samia H Suluhu) hayuko tayari kuyaendeleza yale aliyokuwa akiyafanya Mwl.Magufuli.
Ni jambo la hatari sana Spika wa Bunge letu,Waziri Mkuu,DGS wa TISS,Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanapokuwa tayari kumlazimisha mama awe kama baba yao.
Niseme tu kwamba,Rais Samia H Suluhu hayuko salama kama watu hawa wanahamasisha uhaini na chuki dhidi yake.Hayuko salama !
Ninamuomba Rais na Amirati Jeshi Mkuu wa nchi yetu Mh.Samia H Suluhu atengue uteuzi wa waziri Mkuu na alivunje Bunge turudi kwenye uchaguzi.Wabunge waliopo Bungeni hawajatokana na ridhaa za watanzania bali ilikuwa ridhaa ya Mwl.Magufuli,Polisi,Tume,na TISS ! Si jambo geni katika siasa za ulimwengu huu tukirudi kwenye uchaguzi.
Angalizo,Uchaguzi hautakuwa huru na wa haki iwapo hapana TUME HURU YA UCHAGUZI TANZANIA.
Mwanzo ni mgumu lakini tutafika na tutaweza.
MATHA.