Enyi TISS, sisi raia wema huku mitaani tuna imani Sana na nyinyi,kusema kweli tunawapenda Sana,Sasa Mimi Lee kwa niaba ya Watanzania wema,tunawaomba mumshauri na mhakikishe amepokea ushauri huu mheshimiwa Samiha.
Nawe mama Samiha Rais wetu nakuomba upokee ushauri huu Ili kufanya Tanzania iwe na amani upendo raha furaha na haki,kwani haki huinua Taifa.
Ushauri wangu
Naomba TISS chombo chetu Watanzania,mshaurini Rais Samiha atengeneze taasisi imara ili zilete haki.
Baadhi ya taasisi imara Ni
Mahakama huru,
Bunge huru,
Polisi huru,
TISS huru,
Takukuru huru,
NEC huru,
N.k
Faida ya taassisi huru itamfanya atawale kwa haki,kwa urahisi,kwa raha na bila lawama.
Taasisi huru itawafanya TISS wawe na kazi nyepesi bila lawama kutoka upande wowote.
Polisi hawata onea raia,
Mahakama itaamua kwa Haki,
Bunge litafanya kazi kwa weledi,
Takukuru hawata mwonea mtu,
NEC haitalaumiwa,
TISS haita laumiwa,
Hivyo Mama ataongoza kwa raha bila lawama,yeye atasimamia kuleta maendeleo tu.
Mbali na hayo yote tunaomba Rais Samiha uruhusu katiba pendekezwa ya Jaji Warioba, ambayo wewe Rais ulikua Spika wa Bunge la katiba,tunaomba haya kwa Mustakabali wa Taifa.
Ukiruhusu hayo utatawala ka amani Sana.
Tunaomba Taasisi Imara.