Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Wadau wenzangu japokuwa tupo msibani lakini pia lazima tugange yajayo. Miaka mitano iliyobaki ni parefu kwa hiyo lazima tuweke mazingira safi ili tuweze kufika salama.

Wapo viongozi ambao moja kwa moja walihusika kuchafua kurasa huko nyuma. Hawa walihusika moja kwa moja kuhakikisha, haki za watu na uhuru wa watu unaminywa. Kwa hivyo hawafai kuwepo kwenye hii kurasa mpya tunayokwenda kuianza.

Sidhani kama ni vyema tuwe na Igp ambae hakutaka kufanya uchunguzi suala la Lissu kupigwa risasi. Pia kuwa na wakuu wa mikoa kama John Mongela au Chalamila ambao hawa ni viongozi wanafiki ambao waliunga mkono uvunjifu wa haki za binadamu.

Pia kuwa na Waziri kama Mwigulu Nchemba au Simbachawene haitafaa hata kidogo. Maana ni sawa na kutoanza kurasa mpya. Hivyo rais lazima afagie ngazi zote ili kupata kurasa mpya ambayo italeta amani kwa watanzania.

Ni hayo tu wanabodi.
 
Kurasa gani tena ,si tumekubaliana Simbachawene awe makamu wa Raisi ....
 
Awafukuze Mwigulu Nchemba, Doto katibu mkuu wizara ya fedha na waziri wa Afya mapema kabsa kwani ndiyo watendaji wa hovyo kupata kutokea Duniani
Siyo kufukuzwa tu, Mwigulu na Doto James hadi muda huu walipaswa kuwa jela
 
Wanabodi pole kwa maombolezo.

Wakati nilipoanza kuwa na ugahamu, nilikuwa nasikia maneno, mabeberu, mabwanyenye nk
Maneno hayo hata kwenye somo la historia ya nchi yetu yamo.

Nyakati zile hayakusikika wazi Kama nyakati hizi na hasa awamu hii
NI NENO BAYA LINALOZALISHA CHUKI NA HAO WANAOITWA MJINA HAYA

Wapinzani ni watanzania halisi, mfumo wa vyama vingi, upo karibu nchi nyingi za dunia hii
Kinachoshangaza upinzani nchi hii no dhambi na uadui.

Nchi imegawanyika
Nikuombe Rais na mwenyekiti mtarajiwa was ccm, yakomeshe maneno haya mawili yanaunda chuki ndani na nje ya nchi yetu.
Maneno haya yametumika Sana na kupata nguvu awamu hii ya 5.
 
Kumbe mpinzani ni beberu🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom