Ushauri wangu kwa mh.rais samia ni 1) kuruhusu uhuru wa vyombo vya habari,uhuru wa vyama vya kisiasa kufanya na kunadi sera zao bila bugudha,kamatakamata ya wasiokubaliana na sera za serikali ziachwe,kufukuza watumishi au kuwalaumu hadharani kusitishwe(haki za binadamu),
kuigeuza SGR kuwa ya kibiashara zaidi kwani kutaisaidia bandari ya dar kuondoa mizigo haraka hivyo nchi nyingi za jirani zitapenda kuitumia bandari yetu,kujengwe bandari nyingi kavu morogoro kuhifadhi mizigo hiyo,kuwahimiza mama lishe wakalime kwa kuwapatia mashamba na mikopo ya matrekta ili waache kukaa juani kutwa kuuza zambarau,
kuongeza mishahara,kuwapunguzia wafanyabiashara makodi ya kubambikwa,kuwalinda wasanii kwa vituo vya redio,TV n.k kuwalipa kutokana na thamani za nyimbo au maigizo yao.kwa mfano msanii wa nyimbo za kizazikipya anapotoa album yake iendane na thamani ya nyimbo.kwa mfano pana wasanii wengi nyimbo zao zinapendwa sana hivyo moja kwa moja market price inapanda na walipwe pesa inayolingana na kazi zao,
kuhusu michezo Baraza la michezo la taifa livunjwe na kila chama cha mchezo kiboreshe mchezo husika kuanzia mashuleni.jamani uchumi wa kati maanake GDP ya kila mwananchi inapanda.aliyekuwa akipata laki 2 kwa mwezi sasa apate laki 8,tuboreshe hospitali zetu,shule zetu zitoe elimu bora sio bora elimu,waalimu wapewe mishahara kuanzia milioni,madaktari,
wauguzi vivyo hivyo pamoja na sekta zingine.mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu itolewe kwa mujibu wa utaratibu,wanaomaliza masomo vyuoni wahakikishiwe ajira serikalini na kwenye sekta binafsi.
wale wasiotaka kuajiriwa wasaidiwe kuanzisha miradi kutokana na taaluma zao.huu ndio uchumi wa kati kwa kifupi.