Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Ukiona maelfu ya watanzania wanajitokeza kumuaga comrade Hayati Dr John Pombe Magufuli inamaanisha kuwa mmewafanyia kazi kubwa mliyoahidi miaka mitano iliyopita.

Ni kazi yenu iliyorudisha matumaini kwenu na CCM. Wewe na Hayati Magufuli ndio mliozinguka kuomba kura na mkazipata.

Wewe na Hayati Magufuli ndio mliotekekeza ilani ya CCM kwa ukamilifu na kasi ya kipekee.
Hakuna mwanaCCM au Mpinzani wa CCM atakayewatisha. Maelfu ya watanzania waliojitokeza wamekuletea ujumbe kuwa Serikali yenu imegusa maisha ya wanyonge.

hii inamaanisha umepewa nguvu kama Nahodha uliyekuwa msaidizi sasa ni nahodha kamili katika kuukabili upepo wa kaskazi.

Kila la Kheri Iron lady SSH.
Your Team is always behind You!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 

Attachments

Mhe Mama Samia, Salaam!
Ni pongezi za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni pole kwa kupoteza kiungo muhimu ktk safu yenu ya uongozi.

Pili, nashauri kwa asilimia 75 ufanye maamuzi yako mwenyewe ilimradi nafsi yako ikushuhudie kwamba una nia njema dhidi ya watanzania maskini - nimesema hayo sababu kwa vyovyote waliokuzunguka ni wanamitandao ya Urais wa mwaka 2025. Hata ktk nafasi ya Makamu wako watakushauri kwa mtizamo huo.

Tatu, kuwa mkali na usikubali kuyumbishwa - waliokuzunguka ni wajanja sana wakiona wamefaulu kubadili upepo wa Makamu wako tayari kitambo watakusaliti ili wapate Urais "Tanzania haihitaji wanamitandao ya madaraka bali wachapa kazi ya watu maskini".

Msakila M Kabende
Kigoma - 2021
Usimfundishe Kazi
 
Hata wakimtarget Mama tutakuja na version mpya

lengo lazima litimizwe
 
Mama alisema pale Ikulu kwamba tufutane machozi, it means tuanze upya, yaliyopita yamepita, aliongea kama kiongozi na bila shaka watu wamejitokeza kuonyesha kwamba tumekusikia mama, tunamuaga Rais wetu tuanze upya......binafsi nashauri yale majigambo na kejeli kwa wengine viachwe, turudi kule tulipokulia, WATANZANIA WOTE TULIKUWA NDUGU MOJA.
 
Mama, hatari ya maambukizi ni kubwa, uhai ukikatika haurudi tena. Majukumu yako ni makubwa. Ushauri.

1. Uwe na team mbili za wafanyakazi wa karibu hasa walinzi na wafanyakazi wa nyumbani. Kila team iwe na wiki mbili za duty. Kabla way team haijaingia kazini ipimwe covid na majibu yakitoka salama ndiyo waanze kazi.

2. Tumia virtual meetings kuliko kuonekana hadharani. Sikuhizi karibu kila mtu ana iPad, smartphones na TV tunaangalia hata kwa jirani.

Mengine ni njia za kawaida za kujilinda kama Barakoa na kunawa mikono kila mara.
 
Kabla hali haijawa mbaya, hebu toa neno!

Kama sijasahau vizuri, uongozi wa aliyetutoka uliishia kwenye siasa za aina hiyo!

Nisingependa kuona na wewe ukianzia hapo!

Tolea kauli baa hili wakati muda unaruhusu!

Kuna watu bado wanaamini kuwa wakiwatesa wenzao basi wanaufurahisha utawala na watazawadia kitu.

Ukiendelea kunyamaza, basi itatulazimu kuamini kuwa hili lina baraka zako.

Na kama lina baraka zako,basi utakuwa hauna tofauti na ambaye tunamzika 26/03.

Na kam hauna tofauti naye, basi yetu ni maombi tu na kufanya tabiri tu!
 
Back
Top Bottom