Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Yani wewe
Ujenzi wa SGR ambao umeruka kipande cha Dodoma-Isaka na kwenda Isaka-Mwanza, urekebishwe.

Uanzie Dodoma-Tabora.

Mabadiliko haya yafanyike mapema ili kupunguza hasara kwa Taifa kabla Wakandarasi hawajaanza kazi.

Wakandarasi hao hao wahamishiwe kwenye kipande cha Dodoma-Tabora.
Yani wewe jamaa unaongea bila kuwa na uhakika eti wameruka wameruka nn na eti mara wakandarasi waheshimiwe ndio nn ebu weka facts
 
Mama, hatari ya maambukizi ni kubwa, uhai ukikatika haurudi tena. Majukumu yako ni makubwa. Ushauri.

1. Uwe na team mbili za wafanyakazi wa karibu hasa walinzi na wafanyakazi wa nyumbani. Kila team iwe na wiki mbili za duty. Kabla way team haijaingia kazini ipimwe covid na majibu yakitoka salama ndiyo waanze kazi.

2. Tumia virtual meetings kuliko kuonekana hadharani. Sikuhizi karibu kila mtu ana iPad, smartphones na TV tunaangalia hata kwa jirani.

Mengine ni njia za kawaida za kujilinda kama Barakoa na kunawa mikono kila mara.
Umeongea jambo zuri ila kuna mambo muhimu zaidi kwa wananchi uliza uambiwe
 
Aanze upya asihesabu yaliyopita.

1.Waachilie Waliobambikwa kesi jela, na mashehe kama ni adhabu tayari imetosha pili watesi wao awapo tena duniani.

2. Wakimbizi wa kisiasa wote waliokimbia nchi waruhusiwe kurudi nchini mtesi wao hayupo.

3.Futa sheria zote za kidikteta rejesha Utawala wa uwazi na ukweli

4.Wapinzani wape viti 40 bungeni Ili kuleta mariadhiano.

5.Baraza jipya la mawaziri kabudi, mwigulu,waziri wa afya na naibu wake out ingiza January,mtaka,nape,mavunde.

6.Wasiojulikana wote wasakwe popote wakachukue maharage yao waliyoyapanda.

8.Balance dini,kanda na kabila zingine nchi sio ya kabila moja.

9.Teua CDF,IGP,AG,DPP, mwanasheria mkuu, mkurugenzi mkuu wa tume ya uchaguzi.

10.Sheria za kodi zifumuliwe ziwe rafiki toza kidogo ukusanye zaidi.

11.Uhuru wa vyombo vya habari Ili visaidie kufichua uovu na ufisadi.

12.Mazingira mazuri ya Wawekezaji Ili ajira na kodi ziongezeke.

13.Ikulu ya dodoma igeuzwe chuo kikuu cha ufundi nchini kuanzia veta Hadi phd kuwa na ikulu mbili ni gharama.

Uwanja wa Chato wapewe jeshi uitwe Magufuli airwing Base Ili usipotee.

14.Boresha maslai ya watumishi.

15.Lipa fidia waliobomolewa nyumba zao.

16.Waliofukuzwa Kazi warejeshwe au walipwe kiinua mgongo si wamefanya Kazi lakini.
17.
Mkuu una madini..ila namba tisa..haina umuhimu kwa Sasa... kwenye namba tano ongeza Mwanri..Ummy arudi kwenye nafasi yake..kabudi, ndalichako..na ikipendeza Makonda arudi kweye nafasi yake au ampe wizara
 
Mkuu una madini..ila namba tisa..haina umuhimu kwa Sasa... kwenye namba tano ongeza Mwanri..Ummy arudi kwenye nafasi yake..kabudi, ndalichako..na ikipendeza Makonda arudi kweye nafasi yake au ampe wizara
Makonda akafungue kanisa alipie madhambi yake,Mwanri poa
 
Kwa nchi za kiafrika, mwanamke kukiongoza kiti cha uraisi kwa weledi inakuwa ngumu. Kwa sababu zifuatazo,
1: Sheria za utawala ni mbovu, katiba ni duni.
2: Vitengo vya ki-usalama na nyeti vya serikali na taifa kwa asilimia kubwa vimeshikiliwa na wanaume (Jeshi, Polisi, taasisi za intelligentsia, taasisi za ujasusi, taasisi za ushushu).
3: Mihimili ya serikali (Bunge na mahakama) vimeshikiliwa na wanaume.
4: Mitazamo dume kwa wanaume (Kuwa hatuwezi kutawaliwa na mwanamke).
5: Maamuzi ya wanawake (Mfano: Mama Banda kule Malawi, ndani ya miaka miwili kaanza kusema Ziwa nyasa ni lake).

Mwisho wa siku, unakuta mwanamke kiti Cha uraisi amekalia kama pambo nchi inaongozwa na wanaume vile vile.

Kama ulikuwa huna cha maana kuchangia ingekuwa vema kama ungekaa kimya kuliko kuonyesha your inbuilt "male chauvanism" kama umeoa na una mabinti basi familia yako hiko kifungoni - ufahi kabisa hata kuongoza familia maanake una dharau na chuki binafsi 2wards jinsia ya kike - nafikiri na malezi vile vile yanachangia katika maoni yako hasi kuhusu jinsia ya kike.

Sina lengo la kukusema vibaya, jaribu ku-revisit your skewed comments halafu ujitathimini kama ulicho andika kina mantiki.
 
Mkishindwa kabisa mpeni Asha rose Migiro ni diplomatic huyu.Heri tuongozwe na kina mama wanaweza mbona ndo walezi wa familia nyumbani watashindwa vipi kulea Jamii.Maana wanaume wametuangusha.Kina mama sio madikteta, mafisadi,wezi,wauaji ni wazazi Wana familia.
Migiro ana sifa zote zitakiwazo.
Shule, familia,ndoa,nk
 
R.I.P JPM
Umeondoka na siri kubwa, uliahidi kabla ya kuondoka madarakani utaongeza mishahara kwerikweri. Mara ghafla Mungu amekunyakua. Ulisema hutaongeza 10,000/= labda ulimaanisha utaongeza 100,000/=

Tunakuomba Mama yetu, Rais wetu utimize ahadi hii pamoja na mengine mema aliyoahidi
 
R.I.P JPM
Umeondoka na siri kubwa, uliahidi kabla ya kuondoka madarakani utaongeza mishahara kwerikweri. Mara ghafla Mungu amekunyakua. Ulisema hutaongeza 10,000/= labda ulimaanisha utaongeza 100,000/=

Tunakuomba Mama yetu, Rais wetu utimize ahadi hii pamoja na mengine mema aliyoahidi

Hapana, wafanyakazi wa serikalini haswa walimu, wengi ni wanafiki. Wamemsema sana JPM, hakuna kuwaongezea mishahara mpaka akili zikae sawa.

Mitano tena.
 
😂😂😂naiona roho ya Magufuli ikifanya kazi kwa kasi ya ajabu kupitia Mama Samia! Wezi mtajiju! Siyo kwa mapovu hayo! Magufuli's secret weapon Mama Samia ndio kapewa rungu! Gogogogo 'Iron lady' go go go!
Tanzania 1st
Haya ndo matokeo aliyoyaacha Magufuli, Mpasuko katika jamii yaan watu masikini wanawachukia wenye uwezo kwa kuamini kuwa nchi ni kwa ajili ya tabaka fulani halafu kauli za masikini huwa ni za ajabu sana mwisho ni hivi kama unahisi yule ana pesa za wizi tafuta sehemu na wewe uibe kama una uhakika yule kaiba kazi kulalamika tu kuhisi umeibiwa mtu hujishughulishi bado unaamini unaibiwa sasa sijui unaibiwa nini acheni chuki za bure piga kazi utainuliwa na hao hao unaowadhihaki Mwisho ni kuwa kushindana kumchukia tajiri au mpambanaji ni kumpiga kofi zito mbu aliye juu ya p.... zako povu kafulie nguo hapa hatulihitaji.
 
Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1.Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2.Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa
3.Futa Mpango wa kujenga Daraja la Mwanza la ziwani
4.Ondo miradi ya Maendeleo ya maji chato
5.Ondoa makao makuu Dodoma, na turudi Dar
6. Futa strogiers gourge..tuendeleze gas na tuwape makampuni binadsi kuzalisha umeme ili tupate ajira zaidi
7.Futa SGR ili hera ziendele kwenye maendeleo ya watu na siyo ya vitu
8.Fut mambo ya EFD kwani yanasababisha biashara kusinyaa.

Si vyote vya kufuta viko vya kutafakari jinsi kurekebisha, viko akifuta vitamfuta. Chato ni ya kidunia mpama hivi sasa ni andikapo. Na mshauri Chato atengeneze mazingira kwani inaenda kuwa moja ya vivutio vikubwa vya utalii Tanzania likiwemo Kaburi la JPM. Designer wa kaburi hilo azingatie hajachelewa.
 
MMEONGEA MENGI,MMESHAURI MENGI,MMEWAZA VINGI, LAKINI MAMBO AMBAYO MAMA SAMIA ANATAKIWA AYAFANYE NI MUENDELEZO TU WA YALE ALIYOYAANZISHA RAIS ALIETANGULIA, ANACHOTAKIWA KUFANYA KIPYA NI AMBAYO HAYAJAFANYWA NA MAGUFULI NAYO NI MACHACHE LAKIMama Samia akizingatia haya Tz tutakuwa nnchi ya Maziwa na Asali

MMEONGEA MENGI,MMESHAURI MENGI,MMEWAZA VINGI, LAKINI MAMBO AMBAYO MAMA SAMIA ANATAKIWA AYAFANYE NI MUENDELEZO TU WA YALE ALIYOYAANZISHA RAIS ALIETANGULIA, ANACHOTAKIWA KUFANYA KIPYA NI AMBAYO HAYAJAFANYWA NA MAGUFULI NAYO NI MACHACHE LAKINI NDIO KIU YA WATANZANIA (1) AJIRA (2)MISHAHARA (3) KODI KANDAMIZI (4) DIPLOMASIA
Rais Mama Samia Akizingatia huu ushauri TZ itakuwa nnchi ya maziwa na Asali
 
Kipindi hiki cha maombolezo siku 21.
1. Radios,Tvs,Magazeti,Online Media zicheze nyimbo za huzuni tu na maombolezo. Maana tunapaswa tumboleze sote.

2. Bendera za aina zote nchini zipepee nusu mlingoti. Zote...kila sehemu.ikikutikana bendera imesimama wima mhusika ahukumiwe kwa kosa la kutaka sababisha machafuko

3. Hakuna kupiga horn yoyote barabarani.na gari sizijae barabarani.iwe kutoka kwa ulazima sana barabara ziwe nyeupe. Na wale wauzaji barabarani wapigwe marufuku wengine huuza radio na vitu vya anasa.

4. Asionekane mtanzania anatembea huku anatabasamu. Au wamekaa wanacheka na kusogoza. Watu kama wamekaa kikundi wawe wamejiinamia na kujishika tama. Na kuongea waongee kwa kupokezana.

5. Kwenye magari kuwe kimya kabisa...haya ya umma. Kimya sana hata sauti ya simu isiruhusiwe watu waweke simu zao silent mode na vibration.

6. Salama iwe ni kwa kupungiana mikono tu. Hakuna kuambiana habari za asubuhi au mambo vipi. Sabab tayari tunajua mambo yote ni mabaya. Hakuna jambo zuri kwa sasa.

7. Asiruhusiwe mtu kununua condoms au kwenda guest house jinsia mbili tofauti ikiwa si mke na mume kwa kuonesha cheti cha ndoa.watu hawa wakiruhusiwa watakuwa wanaenda kusheherekea au kufurahia hakuna cha kufurahia kitu.

8. Wana ndoa wote waambie hakuna tendo la ndoa kwa siku 21 kuunga mkono maomboleza na waliofiwa. Ukibainika ni kifungo.

9. Hakuna kukusanyika sehemu bila kibali maalum.iwe ni nyumba za ibada tu. Bar,Pub na Clubs zifungwe ndani ya siku 21 wote tuhuzunike.maduka ya vitu vya urembo,umeme na visivyo vyakula yafungwe. Yabaki maduka ya vyakula tu na vinywaji muhimu visivyoburudisha. Soda, Juice,beer visiuzwe.

10. Watu wasionekane wamevaa nguo za kupendeza, wasionekane wamevaa nguo maridadi.wanaovaa nguo fupi na za kubana wakamatwe.

Kifupi ni kuwa tunataka nchi iomboleze. Na iomboleze kweli kweli kwa namna ambayo next time tukisikia Rais anaumwa tufunge na kuomba asije akafa ili kuepuka adha hii ya maombolezo. Kama Taifa tunapaswa kushirikiana.
Huko tumeshatoka mkuu hatupo tena huko
 
Mama, Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia; Pole kwa msiba wa aliyekuwa Rais wetu JPM; Lakini Hongera kwa kushika Kijiti! Mama Mungu atakusaidia kuliongoza vema taifa letu kwenda mahali ambapo wengi tunapatamani.
OMBI LANGU KWAKO: Mama, naomba ile bandari Kavu kule Kwala ikamilike,ili kuondoa msongamano wa magari hapa jijini; maeneo ya Buguruni, Tazara kuelekea Temeke, msongamano wakati wa mchana ni hatari. Mama, Jemadari wetu naomba hili pia lipewe kipaumbele kati ya mengi. Mungu akubariki.
 
Ngoja mpigwe lock down sasa

Ova

Tunataka mwongozo mpya wenye chimbuko la kisayansi.

Wapiga nyungu wameshaonekana hadharani wakiwa wamepania barakoa.

Yaliyopita si ndwele!
 
Mara baada ya waziri mkuu msitaafu Edward Lowasa kujiunga na kuinunua Chadema ili awe mgombea urais mwaka 2015 , kitu cha kwanza kabisa alipokabidhiwa tu chama alipiga marufuku siasa za kiharakati na kushauri siasa hizo hazina tija kwa sasa. Edward Lowasa alionya kuwa Chadema lazima igraduate kutoka chama cha kiharakati hadi kuwa chama cha siasa sasa.

Edward Lowasa alifafanua madhara ya chama kubaki cha kiharakati muda wote kuwa ni pamoja na kupinga maendeleo yote ya nchi ,kuombea mabaya nchi ,kushirikiana na mabeberu ili kuiibia nchi ,pamoja na kushangilia kila lililobaya kwa taifa ili kumfurahisha tu anayefadhili hizo harakati zako. Matokeo ya harakati hizi ni chama kuchukiwa na wazalendo na kupoteza ushawishi kwa wananchi.
Hakika Lowasa aliona mbali. Leo brand ya chadema imeharibiwa vibaya, chama kilichojizolea umarufu kwa kutetea wanyonge leo kinataka machinga na mama ntilie wafukuzwe mitaani!!! Leo ni furaha kubwa kwa Chadema ndege kukamatwa na wazungu!!!

Pia tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.
Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!
Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.
Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.
Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia

Mkuu umeandika mengi ila yanahusu uzi huu kweri?
 
Back
Top Bottom