Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Habari za wakti huu;

Kwanza kabisa nimpe Pole mama yangu ,Samia Hassan Suluhu kwa kuondokewa na Boss wake,Lakini zaidi nimpe hongera kwa kupata fursa ya kuwa RAIS wa Jamhuri katika kipindi ambacho Jemadari mwendazake JPM alikuwa ameweka moja kati ya malengo makubwa sana(Most ambitious goals of the Modern Tanzania) ya kutaka kufanya Tanzania iwe nchi ya kisasa.Lakini Pia niseme tu kwamba Mwendazake JPM amemuachia TAIFA ambalo kwanza ni divided yet united.Lakini pia anayo kazi ya Pembeni ya kufanya Damage control and healing

Sasa nirudi kwenye mada kuhusu nzi.Kuna nzi wengi sana ambao wamezagaa na najua mpaka wakati huu wengi tayari wameshaanza kujisogeza karibu.Kuna nzi wa aina mbili ambao wanajisogeza kwa kasi sana karibu na RAIS wetu Mama Samia Suluhu Hasan

Nzi wa Aina ya kwanza ni wale ambao walinufaika na Mfumo uliokuwepo zama za Magufuli ambao wanatafuta kila namna kuhakikisha kwamba Maslahi na fursa walizokuwa nazo kisiasa,kijamii na kiuchumi zinaendelea kuwepo na kuna wale Nzi ambao hawakupendezwa na mfumo ule na wengine hata kama waliufaidi lakini hawakuupenda na wengine ambao waliumia na hawakunufaika nao na ambao nao wanasogea kwa kasi kabisa ili waweze kubadili uelekeo wa Upepo.Hawa nzi wote ni nzi hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu.

Najua wachache wa nzi hawa unawajua ila pia najua kuna ambao huwajua au hujaweza kuwatambua ila jihadhari nao.Mheshimiwa RAIS ninapoandika waraka huu ninawaona jinsi wanavyoweka mikakati, wengine wanafuatilia historia yako kujua kama kuna kitu wanaweza kukitumia ili kukufikia kwa urahisi uweze kusikia ushauri wao. Mimi nakusisitizia waepuke hawa nzi.Kazi uliyo nayo ni kubwa sana.

Mheshimiwa RAIS, Wewe ni mrithi wa Magufuli na jamii haitakuelewa kama utaachia kusimamia yale mema ambayo Mwendazake Magufuli aliyasimamia.Usije kushawishika kudharau kukamilisha baadhi ya miradi ambayo ina tija ambayo iko katika hatua za utekelezaji kwani utajishushi heshima yako wewe na utakuwa umeitukana kumbukumbu ya mtangulizi wako JPM ambaye kifo chake kimekupa nafasi ya kuwa rais wa nchi.

Hata hivyo usiogope kuonesha tofauti hasa katika maeneo ambayo kwa hakika Mtangulizi wako hakuwa sahihi.Ndio hakuwa mkamilifu.Kuna baadhi ya mambo mengi sana yanahitaji kurekebishwa na usiogope kuwa tofauti kwani wewe unayo haki ya kuweka tone ya uongozi wako.

Naendelea kukusisitiza kwamba kwa sasa litazame Baraza la Mawaziri, kuna watu hawatakiwa kabisa kuwa humo,watakuvuruga.Kumbuka moja kati ya heshima kubwa uliyo nayo ni kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mpya.Nafasi hio inakupa jukumu moja kubwa nalo ni kuukamilisha mchakato ule na kuhakikisha sauti ya wananchi inasikiwa.

Mama Samia, Wewe ni Mzanzibari, tena Mzanzibari kweli kweli Usisahau hilo.Fanya Jambo kuhusu Zanzibar

Sitaki kusema zaidi ila kama nikajaliwa nitaongeza mengine ila kwa sasa nikutakie kila la heri katika kazi yako ya kuendesha nchi yetu

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu Mbariki Mh. Samia H. Suluhu

Rais wa JMT
Maelezo Mengi mno.
 
Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1.Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2.Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa
3.Futa Mpango wa kujenga Daraja la Mwanza la ziwani
4.Ondo miradi ya Maendeleo ya maji chato
5.Ondoa makao makuu Dodoma, na turudi Dar
6. Futa strogiers gourge..tuendeleze gas na tuwape makampuni binadsi kuzalisha umeme ili tupate ajira zaidi
7.Futa SGR ili hera ziendele kwenye maendeleo ya watu na siyo ya vitu
8.Fut mambo ya EFD kwani yanasababisha biashara kusinyaa.
Mmhhh!!!,Labda umvutishe bhangi.
 
Mtapata taabu saana maana Mama Samia is the 'iron lady'! Ukiingia anga zake tu kuvuruga serikali iliyoyaanzisha chini ya JPM, ambayo yy naye alikuwa sehemu ya serikali hiyo lazima apite na weye! Hamtaamini huyu mama atakavyokuwa zaidi ya Magufuli kwa kutokucheka na nyani! Mama Samia atapandisha viwango vya uongozi kiasi kwamba tutatamani aendelee kutawala kwa muda mrefu! Nafasi ya mwanamke kuchukua madaraka makubwa inaenda kuhakikishwa kwa utendani bora wa Mama Samia! Wezi mmeula wa chuya! Hamna chenu hapa!
Are you mzenji?
 
Huyu jamaa anafaa kabisa kuwa VP naombeni wana CCM mliopo kamati kuu mtupe huyu mwamba mwingine kutoka Chato

Hapa watu wa Chato tunatamani kuona mambo ambayo JPM ameyaacha huku kwetu Chato yakiendelea na hivyo itakuwa faraja kwa JPM huko aliko

Kuona ndoto yake ya kuifanya Chato inakuwa Wuhan inatimia
 
Samahani lakini..
Kalemani hana uwezo huo!
Hata mtwara na lindi huko kuna watu
Bila kusahau sumbawanga na Ruvuma
 
Huyu jamaa anafaa kabisa kuwa VP naombeni wana CCM mliopo kamati kuu mtupe huyu mwamba mwingine kutoka Chato

Hapa watu wa Chato tunatamani kuona mambo ambayo JPM ameyaacha huku kwetu Chato yakiendelea na hivyo itakuwa faraja kwa JPM huko aliko

Kuona ndoto yake ya kuifanya Chato inakuwa Wuhan inatimia
Mataga should know that u can be f..... and forgotten
 
Huyu jamaa anafaa kabisa kuwa VP naombeni wana CCM mliopo kamati kuu mtupe huyu mwamba mwingine kutoka Chato

Hapa watu wa Chato tunatamani kuona mambo ambayo JPM ameyaacha huku kwetu Chato yakiendelea na hivyo itakuwa faraja kwa JPM huko aliko

Kuona ndoto yake ya kuifanya Chato inakuwa Wuhan inatimia
Wewe unahatari Sana Kama ni ingekuwa ni kiongozi mkubwa serikali ungefail mapema Sana..
 
Kama alichoandika anamaanisha,,basi tungeanza kuwapa madara watoto wa baba wa Taifa,,ili naye tumuenzi,,
 
Hiyo half time kwa sasa
Huyu jamaa anafaa kabisa kuwa VP naombeni wana CCM mliopo kamati kuu mtupe huyu mwamba mwingine kutoka Chato

Hapa watu wa Chato tunatamani kuona mambo ambayo JPM ameyaacha huku kwetu Chato yakiendelea na hivyo itakuwa faraja kwa JPM huko aliko

Kuona ndoto yake ya kuifanya Chato inakuwa Wuhan inatimia
 
[emoji57]nyoooo, ili aendeleze miradi!!!...
Ndio mkuu, unadhani akija mwingine hii miradi itakamilika kweli?

Hapa tulikuwa tunajiandaa kupata vyuo vikuu viwili kwa mpigo UDSM tawi la Chato na MUHAS tawi la Chato, Stendi ilikiwa bado haijaanza kunyanyuka pia uwanja wa mpira wa kisasa

Wampe Kalemani kazi iendeleeee
 
Nilikuwa namuelewa sana mzee,,ila kwenye kubalance miradi alishindwa na chuki nyingi za wananchi zipo hapo,,kuna mikoa amvayo kwa miaka mingi ilikuwa kwenye mpango wa kujenga hospitali za rufaa na matawi ya vyuo ,,lakini mpaka sasa hayajafanyika hapohapo maeneo mengine ambayo hayakuwa kwenye mpango yanapewa miradi kibao
 
😅 😅 😅 😅 😅 daah kweli mtu anapewa cheo siyo kutokana na haiba, weledi na uwezo bali kwa sababu kuna haja ya kumuenzi hayati!

Hii nchi imekuwa ni nyumba ya urithi??
Unique way of thinking that can ONLY be found in Tanzania. Ajabu la dunia🤔

Everyday is Saturday................................😎
 
Back
Top Bottom