MSOMI HURU GEREZANI
Tangu rais samia suluhu hassan alipoingia madarakani nimekua nikifuatilia sana hotuba zake pamoja na ripoti anazotoa CAG na nimegundua baadhi ya vitu.
Kwanza namfananisha samia na msomi huru ambaye yupo gerezani kwasababu anajitekenya alafu anacheka mwenyewe. Ripoti zilizoletwa na CAG hivi karibuni zinaonyesha kuwa kuna upotevu mwingi wa pesa na kuna hasara kubwa ilipatikana kwa taifa kwenye miradi mikubwa iliyojengwa na JPM hivyo moja kwa moja kuinyesha kuwa JPM alikua ni fisadi.
Ila ukweli ni kwamba JPM hakua fisadi kwasababu katika uongozi wake kwa muda mfupi tu wa miaka mitano amefanya mengi zaidi ya marais waliokaa madarakani kwa miaka kumi.
Anachokifanya Samia kwasasa ni kuichafua image ya magufuli ili kuonyesha kuwa yeye ni bora ila anasahau kuwa yeye ni rais kwasasa kwasababu ya kura za Magufuli na kama kuna umati ambao unamkubali kwasasa ni kwasababu ya JPM.
Lakini pia Samia anasahau kuwa kama JPM akichafuliwa kwa namna yoyote ile basi ajue nayeye amechafuliwa kwasababu kwenye utawala wa JPM yeye alikuwepo kama makamu wa rais hivyo ni sawa na kujitekenya na kucheka mwenyewe.
"Ukiona umefanya kitu alafu mpinzani wako akashangilia ujue umekosea"JPM. kwasasa naona wale wachumia matumbo na mafisadi wa nchi wanampongeza sana samia kitu ambacho ni hatari sana kwa utawala wake ,bado hajachelewa anaweza kuangalia alipokosea na kujirekebisha mapema.
Rest in peace JPM, SHUJAA WA AFRICA.