DellaPina
JF-Expert Member
- Jun 19, 2016
- 1,011
- 3,471
Atajua mwenyewe
Tangu atoe mtazamo wake juu ya 'watoto kupisha watu wazima kwenye dadala' sikupata tabu kutambua kuwa huyu mama ni Mkoloni
Kisha zawadi kwa mzee isivyo na kichwa wala miguu na kulazimisha iwe habari ya mjini maisha yasimame waonekane wao tu wanapolipana fadhila.!
Nina hakika kaagiza yeye labda ajikoshe kwa kugeuza watu kafara
Ila hapo juu kusema mtu mtoto ampishe mzee mbona ni sawa hivi hilo nalo ni la kumlaumu ehh?utamaduni wetu sisi watanzania au waafrica kiujumla mbona upo hivyo,mtu mzima yaani umri wa mzazi wako huna budi kama ana mzigo kumpokea na kama ni mtaani kwako unamsaidia kumfikishia kwake ndivyo tamaduni zetu waafrica.Yaani mzee yeyote ambaye ana umri wa mzazi wako au babu yako heshima yake anatakiwa apewe kama ni mzee wako,hata nyumbani kwako tu mzee wako akaingia nyumbani unatizama TV ukampa salam huku umekaa kwenye kochi kiustaarabu kuonesha heshima ni bora usimame umpe salamu kisha unakaa.Tatizo linalotutoa kwenye tamaduni bora za kwetu na kuiga tabia za magharibi ndilo linatuponza na huko tunapoenda usishangae mtoto wako pia asikuheshimu halafu tuje kulaumu watoto wa siku hizi.Tunatakiwa tulaumu tulipojikwaa na siyo tulipoangukia.Wewe leo ni kijana hayo unayotaka uwafanyie wazee wako au wazee wa wengine kesho yakiwa mazuri na wewe pia unatarajia ufanyiwe kama hayo ila ukiwa unasema ahhh achana nao hao zama zao zishapita potelea mbali,huenda kesho kama Mungu atakupa umri kama wa hao utakuwa wa kwanza kulipwa wewe kama malipo uliyoyafanya enzi zako za ujana na huenda ukapokea mazuri zaidi ya hayo au mabaya zaidi ya hayo.Ni mtazamo tu tusijenge chuki.