Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Nichukue nafas hiyi kuipongeza serikali yetu pendwa ya mh rais wa awamu hiyi

Kwa kutufanya wananchi wake tuwe na faraja na amani ndani ya mioyo yetu...
giphy.gif
 
Ukute Mamacsna nia njema waliomzunguka wanamtisha na kumuogopesha .....anashindwa kuwa kichwa kigumu ...anatamani kurudi 2025 ..hizo thawabu pia anazitaka amebakia njia panda nchi iko auto pilot...hajielewi anataka nini.....
Anatakiwa amtie mkwe wake apo wizara ya utumishi na diwani amtie hapo TISS aende akalime
 
Mara paa ndege.............mungu atakuwa ametusikia kilio chetu

a)imepotea angani
b)imeganda angani...
Wenzako hatuna kilio. Ukiondoa hayo maneno "Mungu atakuwa amesikia kilio chetu" itapendeza.

Ndege ifike salama. Mama yetu tunampenda sana.
 
Kwa kweli ni lazima tuishi kwa kujitegemea kodi ni wajibu wetu hakuna mtu atakayetujengea zahanati na kutujengea barabara haya yote ni majukumu nasalimia kwa jina la Jamuhuri
 
hongera sana raisi Samia Suluhu Hassani. Baada ya pongezi kwa kazi nzuri napenda kukumbusha kuwa baadhi ya watendaji na wasaidizi wako hawanania ya dhati kuona wananchi wanafurahia uwongozi wako hivyo huzalisha chuki kwa serikali. Mfano ni kuto walipa Wastaafu wa ATCL madai yao. Najua hili suala unalifahamu vizuri.

Wapo wastaafu wanadai pensheni miaka kumi sasa kwa kuwa makato yao hayakupelekwa PPF (PSSSF) ilihali walikatwa kutoka mishahara yao. Mahakama Kuu ilisha amua walipwe, Katibu Mkuu Kiongozi marehemu Kijazi alisha elekeza wizara ichukua hatua za utekelezaji haraka. Bunge linafahamu hili suala mbunge Chiwelesa alisha lipigia kilele na kuomba wastaafu hawa walipwe lakini hakuna utekelezaji. Tunajua kuna watendaji wizara ya Fedha na wizara ya Ujenzi na Uchukuzi hawataki wastaafu wa ATCL walipwe.

Hali hii inachangia wastaafu, watoto, wajukuu, vitukuu, jamaa zao waione serikali haiwatendei haki uzao wao. Ombi langu kwako Raisi lisimamie hili suala wastaafu wa ATCL walipwe madai yao. Waziri mkuu ananadi kuwa wastaafu wanalipwa hii si kweli kinacholipwa ni pesa serikali ilikopa sasa inarudisha na PSSSF wanatumia kuendesha taasisi maana mfuko huu una hali mbaya.
 
Pamoja na kwamba nilimkubali sana JPM sasa kwa moyo mmoja naungana na Mama rasmi.

Uzalendo sio kususa, uzalendo ni kuwa mnyenyekevu na kukosoa kwa utaratibu maalum.

JPM aliweza kuvumilia tawala zilizopita kiasi kwamba akawa anakuwa waziri kila baada ya uchaguzi, Bashiru Ally pamoja na kushushwa vyeo ila yuko na mama na wala hana neno na anaendelea kutumikia nafasi yake kwa unyenyekevu, mimi ni nani hata nikapingana na mamlaka zinazoniongoza tena kwa kufuata katiba?

Kuanzia sasa niko nawe mama, kupitia forums mbalimbali nitaendelea kukupongeza, kukushauri na kukukosoa pale inapobidi.

Nawashauri team JPM na wapinzani wote kumsapoti mama maana kwa sasa ndo Rais wetu. Hatupaswi kugombania fito wakati tunajenga nyumba moja. Siku zote sikio halizidi kichwa.

Mwisho, namtakia mama kila lakheri katika utendaji wake!
 
Watoto wa teuzi katika ubora wenu, najaribu kuwaza kama wewe ni Bashiru, au ni Ridhiwani maana alisifia sana toka nafasi ya waziri wa ulinzi ilipokua wazi. au ni Nape wewe..😄😄
 
Pamoja na kwamba nilimkubali sana JPM sasa kwa moyo mmoja naungana na Mama rasmi.

Uzalendo sio kususa, uzalendo ni kuwa mnyenyekevu na kukosoa kwa utaratibu maalum...
Hizo hoja nzito. Mwenye madaraka amepewa mamlaka ya kuongoza Jamii, kampuni au Taasisi husika, kwa Kanuni na Taratibu zilizokubaliwa. Hata kwenye Kaya, Mkuu wake huingoza kwa jinsi ya Mila na Tamaduni

Kutii mamlaka ni utu, ujasiri na uungwana. Na Maandiko Matakatifu yasema: Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo? Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana (Marko 12:14, 17).
 
BARUA YA WAZI KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

13|09|2021
JABALI

THE PRESIDENT OF URT,
P.O BOX 01
DAR ES SALAAM
TANZANIA

YAH: PONGEZI ZA WAZI

Nakupongeza kwa haya yafuatayo,

1.Kupandisha bei ya mazao yote,

2. Royal Tour kuvitia watali wengi

3.Kupunguza tozo hadi elfu 6 hata nitume mil 100

4. Kutoa mikopo ya HESLB kwa wanafunzi wote,

5. Kupandisha madaraja watumishi

7. Kutoa ajira mpya elfu 40

8. Kutoa bili 60 kununua mahindi

9. Kufuta matozo zaidi ya 200

10. Kutupenda Watanzani,

Asante Sana Mama,

JABALI
 
3.Kupunguza tozo hadi elfu 6 hata nitume mil 100 hii ni kweli?
 
BARUA YA WAZI KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN




13|09|2021
JABALI




THE PRESIDENT OF URT,
P.O BOX 01
DAR ES SALAAM
TANZANIA

YAH: PONGEZI ZA WAZI

Nakupongeza kwa haya yafuatayo,

1.Kupandisha bei ya mazao yote,

2. Royal Tour kuvitia watali wengi

3.Kupunguza tozo hadi elfu 6 hata nitume mil 100

4. Kutoa mikopo ya HESLB kwa wanafunzi wote,

5. Kupandisha madaraja watumishi

7. Kutoa ajira mpya elfu 40

8. Kutoa bili 60 kununua mahindi

9. Kufuta matozo zaidi ya 200

10. Kutupenda Watanzani,

Asante Sana Mama,

JABALI
Upuuzi mtupu
 
Jamani habari zenu, mimi binafsi kuna binti mmoja yupo idara ya Afya,anafanya kazi vizuri mnoo, amenisaidia sana watoto wangu na hata watu wengine, ni mkarimu ,mcheshi na ana upendo uliotukuka, yupo tayari kuchelewa kutoka ili tu ahakikishe amewasaidia watu, mimi ananigusa sana.

natamani serikali imuangalie kwa jicho la pili ,awe kielelezo bora cha watoa huduma, hakuna mtu atakayekutana na yule binti akaacha kumsifia ,ni msichana mdogo sana, lakini anajali kazi yake.

Mungu aendelee kumuimarisha,
 
Mh Rais tunaomba uteue Mkurugenzi Mwendeshaji mpya wa Arusha International Conferences Centre baada ya aliyekuwepo kufariki miezi kadhaa iliyopita.

Teua mtu akiyeko nje ya hapo AICC, ikiwezekana ipatikane motivation and new ideas. Waliopo wamechoka kimawazo kama shirika lenyewe.

Wapo vijana wasomi wengi wazuri hapa Foreign Affairs na kwenye Embassies. Shirika linapoendelea bila uongozi linageuka kuwa shamba la bibi.
 
Its hard to blame people for dancing when the music still playing.

Mama akiweza kuuzima mziki ulioachwa ukiimba watu hawatocheza maana mziki utakua ushazima ila bila hivyo watu wataendelea kucheza.
 
Back
Top Bottom