Ndugu Moderaters, hapa sijamshauri Rais bali nimewashauri watu wanaompinga. Hamkuwa na sababu ya kuulete huu uzi huku.
Ndugu Max, niwewe uliyefanya hivi au vijana wako? Sitaki kuamini kuwa ni wewe maana huwezi kuchanganya vitu vidogo kiasi hiki.
Nina mashaka na vijana wako unaoajiri. Wamenisikitisha sana.
Ndugu Max, niwewe uliyefanya hivi au vijana wako? Sitaki kuamini kuwa ni wewe maana huwezi kuchanganya vitu vidogo kiasi hiki.
Nina mashaka na vijana wako unaoajiri. Wamenisikitisha sana.
Pamoja na kwamba nilimkubali sana JPM sasa kwa moyo mmoja naungana na Mama rasmi.
Uzalendo sio kususa, uzalendo ni kuwa mnyenyekevu na kukosoa kwa utaratibu maalum.
JPM aliweza kuvumilia tawala zilizopita kiasi kwamba akawa anakuwa waziri kila baada ya uchaguzi, Bashiru Ally pamoja na kushushwa vyeo ila yuko na mama na wala hana neno na anaendelea kutumikia nafasi yake kwa unyenyekevu, mimi ni nani hata nikapingana na mamlaka zinazoniongoza tena kwa kufuata katiba?
Kuanzia sasa niko nawe mama, kupitia forums mbalimbali nitaendelea kukupongeza, kukushauri na kukukosoa pale inapobidi.
Nawashauri team JPM na wapinzani wote kumsapoti mama maana kwa sasa ndo Rais wetu. Hatupaswi kugombania fito wakati tunajenga nyumba moja. Siku zote sikio halizidi kichwa.
Mwisho, namtakia mama kila lakheri katika utendaji wake!