Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hii ni awamu ya tano mhula wa pili.
Sasa inakuwaje waajiriwa wa serikali ya awamu hiyo hiyo waiseme serikali wanayoitumikia wao?

Kuna umuhimu wa Katiba kueleza kinagaubaga, pakitokea kuna kuondoka kwa kiongozi mkuu wa serikali aliyechaguliwa na wananchi, ni lazima pawepo na uchaguzi ili kiongozi mwingine au serikali nyingine ipatikane. Haya mambo ya kuachiana, halafu ukisha achiwa unajitungia yako hata ambayo hukuyawasilisha kwa wananchi wakupe ridhaa ya kuyatekeleza haifai kabisa.

Samia anatakiwa kutekeleza yale yote yaliyosimamiwa na Magufuli

Ingekuwa ni nchi ya wenye kujitambua, mtu au watu wangejitokeza kupinga mapya haya na serikali inayoyayatekeleza kwa kwenda mahakamani ili sheria iamue, kama kweli Samia anaruhusa kufanya ya kwake, badala ya yale waliyowaeleza wananchi wakati wa kampeni.
 
Ndugu yangu mimi ni mshabiki mkuu wa Kikwete kwa sababu moja tuu alipeleka shule za secondari watoto wa msikini kupita watawala wote unaowajua africa.
Huna hata aibu kusema uongo hapa?

Kama hujui historia ya nchi hii si nenda kajifunze kirahisi tu? Kamuulize yeye Kikwete mwenyewe akueleze kama yeye angeweza kusoma hadi alipofikia bila ya serikali iliyomsomesha wakati huo.
Halafu leo hii unakuja hapa na kuandika usiyokuwa nayo habari kabisa.
 
Maisha yanakwenda kasi na udongo ni wetu, ndio maana makaburi hata siku moja hayawezi kujaa ila nyumba zitajaa.

Swala ambalo la kujiita awamu ya sita ni kama kujitoa kwenye kachumbari ambayo bado upo kwenye awamu ya tano.

Tumesikia kwenye vikao vyenu CCM hapo dodoma ukionesha kuwa kama ukiwepo na yale yote yaliyokuwa awamu ya tano.

Kumbuka awamu yako ya sita ni 2025 mpaka uchaguliwe na wananchi. Kwa sasa endeleza uliyoachiwa si kuleta mengine.
 
Awamu hewa. Wao ni zao kamili la awamu ya 5. Hawataki kutumia ubini wao.
 
Back
Top Bottom