Kumekuwa na mkakati mkumbwa wa kuaminisha watu kuhusu mwenendo wa siasa zetu, na kwa bahati mbaya sana chama kilichopo madarakani, chama cha mapinduzi kumekuwa kikipambana chenyewe dhidi ya kivuli chake, yaani kila awamu inaisema awamu iliyopita. Ilitokea kwa Kikwete alivyoachiwa na Mkapa, Magufuli alivyoachiwa na Kikwete, na sasa Rais Samia alivyoachiwa na Magufuli.
Katika kusemeana wanatofautiana logic na relevance, tukiangalia awamu hizi mbili za mwisho, viongozi waandamizi ni wale wale, na viongozi wakuu wanatofautiana namna walivyoingia madarakani.
Uchaguzi 2015 Magufuli aliingia kwa mbinde sababu Imani ya watu katika chama na Serikali ilipungua mno, hivyo ilibidi afanye juhudi kubwa kuturudisha imani hiyo, na Sera ya chama hapa kazi tuu, ilitumika kubadili mindset ya wananchi na watumishi, kusafisha uozo ulikuwepo mf. Mikataba mibovu kama madini na kwingineko, upatikanaji wa huduma za kijamii ulipanda na uwajibikaji ulikuwepo,
Ni mwaka mmoja Sasa umepita toka awamu ya sita, iingie madarakani, kwa viongozi wale wale ajenda kubwa inayonekana sio tena maendeleo wala, namna ya kukuza uchumi wa nchi sambamba na vipato sasa ni vijembe visivyo na logic wala relevance, kukemea mienendo ya mtangulizi wako Hayati Magufuli ni kujidhalilisha tu, haswa wakati huu dunia inapitia kipindi kigumu sana, inakuonesha uko hapo kutetea uonevu, ufisadi na kujinufaisha wewe pamoja na familia yako.
Ni vyema ukachunga kinywa chako na ukachagua maneno ya kusema utazidi kupoteza mvuto, kumuita binadamu Simba wa Yuda ni kumdhihaki sio yeye tuu, hata dhehebu fulani litahisi hivyo
Katika maadhimisho ya mwaka mmoja awamu ya sita iingie, hamna jambo hata, la kujivunia zaidi tozo kandamizi, na diplomasia.
Mimi rai yangu naomba mh Rais, usitafute sifa kwa jirani wakati watoto wako wanakufa na njnn.