Mama unataka tukukumbushe hili mara ngapi ili utuelewe Wanao tunaokupenda na kukutakia mema? Wengine hatujaumbwa na Unafiki wa Kukupamba ( Kukusifia ) tu hata kama kuna mahala Unaharibu ila maana yetu halisi ya Kumpenda Mtu ni Kumkosoa kwa Kumjenga pale akikosea ( akikengeuka ) mahala.
Sasa kama Wewe ( Rais ) tunayeamini kuwa una Taarifa zote na Ufahamu mwingi wa Kimaarifa iwe ni Binafsi au kupitia Wasaidizi wako kila mara ukizungumza au ukitolea Ufafanuzi Jambo muhimu ni lazima useme Neno I think ( Unadhani ) je, Sisi Watu wa kawaida mno nchini Tanzania akina MINOCYCLINE tusemeje au tutumie neno gani?
Mbele ya Watu very Serious na Werevu ndani na nje ya nchi nina uhakika ukiwa unasema ( unalitumia ) neno hili la Unadhani ( I think ) huwa Wanakudharau na hupoteza pia imani nawe na hata Credibility yako vile vile hushuka ( inashuka )
Binafsi neno Nadhani ( I think ) silipendi na hata huku Kimtaa Mtaa ( Mtaani ) nikiwa naongea na Mtu ( hasa kwa Jambo Muhimu ) halafu akiwa anasema Nadhani ( I think ) huwa namdharau na hata kutamani Nimzabe tu Kibao kwani huwa nahisi ni Mtu asiye Knowledgeable and Well Informed katika Mambo ( Masuala Mtambuka ) mengi ya Tanzania na nje ya Mipaka ya Tanzania.
Wasaidizi wa Rais msaidieni katika hili.