Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mheshimiwa Rais ,tupo chini ya Miguu yako sisi wanakijiji wa kijiji cha Nyatwali wilayani Bunda,sasa ni miezi 6 imepita tokea serekali yako tukufu itoe Tangazo la kutuhamisha katika ardhi yetu kwa madai ya manufaa ya umma,sawa mama tumekubali Serekali yako imefanya tathimini ya kulipa watu wamechora nyumba zetu,wamezuia watu kuendeleza chochote sio Kilimo sio kitu chochote,Mama sisi ni Watanzania wema kabisa,kama mnachukua Ardhi yetu ambayo sio wavamizi kabisa tupo kisheria na hati tunazo na mmetufuliza tumekubali,sasa ni kitu ngani hamlipi hela ili tuwapishe?Mama Rais hebu vaa viatu vyetu na tuonee huruma hatulimi atafanyi kitu chochote shughuli zote za Maendeleo zimesimama,Mama Rais mbona tunakua watumwa kwenye Nchi yetu wenyewe?Mama Rais tunakuomba saana tena saana tulipeni hela zetu,ili tuendelee na maisha yetu kama vile Mkuu wa Mkoa au mkuu wa wilaya Bunda wanavyoendelea na maisha yao na mshahara unaingia kila mwezi.sisi tumefukuzwa hakuna kulima tulisubili malipo.Mama Rais tunaumia saana tena saana.Kama itakupendeza tulipe hela zetu tuondoke kuliko kusitisha tu maisha yetu kwa namna hii.Asante mama yangu mheshimiwa Rais
 
Habari za jumapili ,
Nimewaza na kuendelea kutafakari mengi ambayo yanaleta Tija au laaa.....

Umaarufu wa mama umeongeza au kupungua ndan ya chama na kwa waTz hata katka medali za kitaifa na kimataifa
Forcast to 2025:-

Let have positive comments or view (hii ni research
 
Kipimo cha umaarufu wa mama 'anacho' JK. Yeye ndiye aliyesema kuwa (baada ya kuwapima makada 'wote') hamuoni mtu maarufu zaidi ya mama ndani na nje ya chama.
Labda umuite tena umuhoji... ndio aweze kutuambia kama umeongezeka, umepungua ama umebaki pale pale 😀😀

download.jpeg

Pichani: Mfano wa kipimo cha umaarufu wa viongozi wa umma kilichovumbuliwa na eng Kikwete (Bsc industrial engineering 😎) kinachojulikana kama JAKAOMETER!
 
Kwanza ni seme mimi Ndwate ni mpitaji tu kwenye huu mtandao wa kijamii kama msomaji. Kilichonifanya nijiunge leo kama mshiriki mwanachama kwa kuandika maoni, ni jambo la huyu bwana ndg mmoja niloyekutana naye leo kwenye kashamba bustani kangu akihitaji nazi katika mnazi mmoja tu ulio ndani ya eneo langu hili la mita mraba 320. Huyu ndg ni hustller wa biashara ya nazi na mkwezi. Hii ni moja.

Mbili yake kilicho nistua katika maongezi yetu yale ya undugu wa Kitanzania akaniambia nimekutana na wewe utanisaidia jambo langu linalonisumbua kwa kitambo na nimejaribu kupata ufumbuzi kwa wengine nimeshindwa. Ni kamuuliza kwa nini unasema hivyo? Kabla ya kunijibu naye akaniuliza wewe ni mtu wa wapi? Nikamwambia, Lindi kilwa kijiji cha uteli tatu. Na mie nikamuuliza na wewe rafiki kwenu wapi? Akasema mie kwetu Chakechake Pemba. Eeh niambie unachofikiri naweza kukusaidia. Akatia ungenge, kidogo You are a right personal akimaanisha person I have no doubt about it.

Tatu yake, akasema sina sababu ya kuzunguka I am going right to the point. Mimi nimesoma skuli/ shule ya msingi sasa ni Sekondari Ziwani Chakechake Pemba. Tangu mwaka 1970 mpaka 1978 nilipomaliza form three.
Nikamkazia macho na masikio yakanisimama huyu anataka, kusema nini sasa?

Nne yake, eeh ndio ndugu. Katika miaka hiyo nimesoma na Mh Rais Watanzania Mama Samia Suluhu Hassani kama school na class Mate wangu. Baba yake Maalimu Suluhu Hassani akiwa Mwalimu Mkuu wetu. Nikamwambia haiwezekani unazeeka vibaya wewe rafiki, si amini. Hebu nipe nondo zaidi. Ndio tena alihamia kutoka Zanzibar Makunduchi akaja kuwa Mwl Mkuu hapo shule ya Ziwani Chakechake Pemba. Alikuwa na gari yake yenye reg no LL 1. Nikamwambia basi kwangu imetosha sitaki maelezo zaidi Ni kusaidie nini?

Tano yake, akasema, nimejaribu kutafuta namna ya kufika na kuonana na Mh Rais Samia Suluhu Hassani lakini na ambiwa mambo mengi ya kukatisha tamaa na kufanya nikose ujasiri kabisa, kwamba haiwezekani. Ni kamwambia jaribu kwenda kwenye lango la Ikulu mapokezi waambie wasaidizi wake watakusaidia namna ya kumfikia ili uweze kuwasilisha hilo jambo la moyoni mwako ulilosema ni siri. Akasema nimekuambia wewe ndio utanisaidi.

Hii imenipa wakati mgumu sana na nikamuuliza Mungu kwa nini mimi wakati mchakato huu sijawahi ufanya popote maishani mwangu mbali ya hata kuufikiria tu?! Ndio baada ya kutafakari sana nikaona acha nifanye hiki nilicho fanya hapa sasa .Kama nimekosea nisamehewe bure ni katika kule kujaribu kutenda wema tu.

Najua hapa mpo wasaidizi wa Mh Rais. Cheo cha Rais ni kikubwa mno katika nchi na hivyo hivyo Taasisi ya Uraisi vinatisha kwa ukuu na heshima katika mamlaka za wanadamu, lakini ni meandika ili kama Ndg Saidi Nassoro Hamisi ataweza kusaidika kwa kukutanishwa na classmate wake iwe hivyo na asaidike. Mawasiliano yake ni mobile nos 0682 791614 na 0656 605529. Natanguliza shukrani na rudia tena kama nimekosea nisamehewe bure.
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
.
 
Habari, karibuni katika andiko langu la stories of Change 2023
 
Mtu mdogo kama mimi kumshauri mkubwa utaonekana kama huna adabu na huna akili, lakini ningekuwa na nafasi ningemshauri Mama Samia asiwanie 2025, yale aliyokwisha fanya ni ya kutukuka sana yanayohitaji kuandikwa kwa wino wa dhahabu.
 
Mtu mdogo kama mimi kumshauri mkubwa utaonekana kama huna adabu na huna akili, lakini ningekuwa na nafasi ningemshauri Mama Samia asiwanie 2025, yale aliyokwisha fanya ni ya kutukuka sana yanayohitaji kuandikwa kwa wino wa dhahabu.
 
Hili ndilo somo linalohitajika hapa nchini kwa sasa futa masomo ya Dini na mengine yasiyo na Tija. Naomba waziri wa Elimu na Wadau wa Elimu hili mlitazame kwa Umakini nchi ina Wasomi ila hawana uelewa kwenye mikataba tunalizwa kila siku Aibu! N:B NITAFURAHI LIKIFUNDISHWA NA MADRASA PIA.
 
Back
Top Bottom