Mheshimiwa Rais ,tupo chini ya Miguu yako sisi wanakijiji wa kijiji cha Nyatwali wilayani Bunda,sasa ni miezi 6 imepita tokea serekali yako tukufu itoe Tangazo la kutuhamisha katika ardhi yetu kwa madai ya manufaa ya umma,sawa mama tumekubali Serekali yako imefanya tathimini ya kulipa watu wamechora nyumba zetu,wamezuia watu kuendeleza chochote sio Kilimo sio kitu chochote,Mama sisi ni Watanzania wema kabisa,kama mnachukua Ardhi yetu ambayo sio wavamizi kabisa tupo kisheria na hati tunazo na mmetufuliza tumekubali,sasa ni kitu ngani hamlipi hela ili tuwapishe?Mama Rais hebu vaa viatu vyetu na tuonee huruma hatulimi atafanyi kitu chochote shughuli zote za Maendeleo zimesimama,Mama Rais mbona tunakua watumwa kwenye Nchi yetu wenyewe?Mama Rais tunakuomba saana tena saana tulipeni hela zetu,ili tuendelee na maisha yetu kama vile Mkuu wa Mkoa au mkuu wa wilaya Bunda wanavyoendelea na maisha yao na mshahara unaingia kila mwezi.sisi tumefukuzwa hakuna kulima tulisubili malipo.Mama Rais tunaumia saana tena saana.Kama itakupendeza tulipe hela zetu tuondoke kuliko kusitisha tu maisha yetu kwa namna hii.Asante mama yangu mheshimiwa Rais