Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Ndo naanza kuamini hakuna akina salama leku wanajua alufa bete pekee elimu dunia hawajui kitu mfano hawa waarabu wa dpw wangekuwa na elimu wasingeweza kuandika mkataba wa namna ile wanahisi zama za ukolon
 
Ndo naanza kuamini hakuna akina salama leku wanajua alufa bete pekee elimu dunia hawajui kitu mfano hawa waarabu wa dpw wangekuwa na elimu wasingeweza kuandika mkataba wa namna ile wanahisi zama za ukolon
Natamani sana wapate Elimu Maisha yamebadilika
 
1692379723429.png


Kwa wanaofuatilia kinachoendelea nchini, Tanzania saa ni taifa la kipolisi. Kwani, polisi wanaweza kukamata yeyote wamtakaye na kumfungulia kesi hata asiyohusika nayo hasa anapokuwa mpinzani wa serikali au agenda zake. Mfano wa karibuni ni kukamatwa kwa watajwa hapo juu siyo kwa sababu hawawezi kutenda jinai. La hasha. Ni kwa sababu kesi waliyofunguliwa circumstantially, hawakutenda. Kwa sababu, wahusika walitumia uhuru wao wa kujieleza, hii haiwezi kuwa uhaini.
1692379674446.png

Kwa mambo yanavyokwenda, wapo wanaodhani kuwa rais mama anaingizwa mkenge ili wakati wa kutafuta mgombea urais wa CCM apigwe chini. Je wewe unampa ushauri gani rais mama ili kuepuka kuingizwa box na kujuta baadaye? Je unampa ushauri gani ukimshauri ajue yuko alipo kwa muda na hivyo, awe makini?
Karibuni wanangu wapendwani
 
Aendelee kuwaamini hao washauri fake wake hadi siku anaambulia kura Moja
Kwanza huyo nape mwenyewe alishamtukanaga mwenda zake na sauti zikaja public mbona ye hakushtakiwa na kesi ya uhaini yaani wajinga wachache wanaleta taaluki nchini
 
... chawa ni hatari kwa uhai wa binadamu. Wanachoangalia ni kufaidika na damu yako tu basi; hata udondoke kwao sio issue. Kataa chawa!
 
View attachment 2721013

Kwa wanaofuatilia kinachoendelea nchini, Tanzania saa ni taifa la kipolisi. Kwani, polisi wanaweza kukamata yeyote wamtakaye na kumfungulia kesi hata asiyohusika nayo hasa anapokuwa mpinzani wa serikali au agenda zake. Mfano wa karibuni ni kukamatwa kwa watajwa hapo juu siyo kwa sababu hawawezi kutenda jinai. La hasha. Ni kwa sababu kesi waliyofunguliwa circumstantially, hawakutenda. Kwa sababu, wahusika walitumia uhuru wao wa kujieleza, hii haiwezi kuwa uhaini. View attachment 2721008
Kwa mambo yanavyokwenda, wapo wanaodhani kuwa rais mama anaingizwa mkenge ili wakati wa kutafuta mgombea urais wa CCM apigwe chini. Je wewe unampa ushauri gani rais mama ili kuepuka kuingizwa box na kujuta baadaye? Je unampa ushauri gani ukimshauri ajue yuko alipo kwa muda na hivyo, awe makini?
Karibuni wanangu wapendwani
Sina ushauri Bali aibu hii itamuandama Hadi kaburini
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa mchongo, kaonewa, hana zlsifa za kuongoza nchi labda kitchen party
 
Mh.Rais wangu usipokuwa makini wamebakia pointi Moja kugonga mvinyo.

Sisi mashabiki wako tunakupenda na tunapenda uendelee,hatupendi kabisa kurudi kule Kwa watu wanaoamini mkono wa chuma,watatufukarisha.
Huu ushauri wako ulitakiwa kuutoa kabla mambo hayaja haribika. Kwa sasa naweza kusema, it is too late.
 
Kuhusu suala la BANDARI.
Pongezi hizo nazitoa kwa sababu hakujawahi kutokea masuala ya mikataba tunayoingia kama nchi kujadiliwa kwa uwazi kama ilivyo sasa. Miaka yote tulikuwa tunastukia mikataba tayari imesainiwa. Wala hakuna aliyejua nini kimo kwenye mikataba hiyo.
Hongera pia kwa kusimama imara, maana katika hali ya kawaida kuna wengine pengine walikushauri usifuate maoni na matakwa ya wananchi. Wewe amua mwenyewe kwa sababu una nguvu na mamlaka ya kufanya hivyo. Lakini umekuwa imara na kusema mimi ni Kiongozi ambaye pia ninawajibika kuwasikiliza wananchi. Hongera sana kwa hatua hiyo na Mwenyezi Mungu akujalie yenye heri katika kututumia wananchi.
 
Ningewachukua Hawa wanaopiga kelele akina lisu, Shivji, mwabukusi, mdude, slaa nk nikawaambia twendeni Dubai tukaandike mkataba upya
 
Back
Top Bottom