Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Acha uongo wewe jamaa!Dunia ya leo yenye utandawazi ndiyo unaandika ujingaujinga hivyo?Unataka kumdanganya nani?
binafsi siwezi danganya wanyonge, kwanza sio ustaarabu na hakuna haja kumdanganya...

ni bahati mbaya tu wabishi kwenye hili, miongoni mwao wamegoma katukatu kurejea vijijini makwao hata baada ya kumaliza masomo, licha ya kwamba hawaajiriki tena kwasabb ya kigezo cha umri...

hata hivyo,
ukweli utabak pale pale kwamba yapo maeneo nchini hawajui kitu kingine chochote zaidi ya CCM na kiongozi wake Dr.Samia Suluhu Hassan 🐒

kuthibitisha hilo,
tembelea tovuti ya tume huru ya uchaguzi utagundua maeneo ambayo nayazungumzia.

ushindi wa kishindo wa CCM hua ni wa zaidi ya asilimia 98%, huku hizo asilimia zilizobaki ni kura zilizoharibika 🐒
 
ukizungumza habari tofauti na CCM na kiongozi wake mkuu comrade Dr Samia Suluhu Hassan, wanainchi wa maeneo hayo kwanza...

Mahaba waliyonayo dhidi ya Chama na Serikali sikivu ya CCM, hayapimiki, ni ya kufa na kuzikana 🐒
Ni wapi huko? Hujapataja.
 
binafsi siwezi danganya wanyonge, kwanza sio ustaarabu na hakuna haja kumdanganya...

ni bahati mbaya tu wabishi kwenye hili, miongoni mwao wamegoma katukatu kurejea vijijini makwao hata baada ya kumaliza masomo, licha ya kwamba hawaajiriki tena kwasabb ya kigezo cha umri.....
Mpaka hapa inaonekana hujui unachokiongea.
 
Wananchi wa kijiji cha Kipwa waliojengewa shule na zahanati mpya baada ya kijiji chao kumezwa na maji ya ziwa Tanganyika huwezi kuwaambia kitu kuhusu Mama Samia wakakuelewa. Hao wananchi walipewa na viwanja bure. Hicho kijiji kilikuwa hakina barabara ya kuingia kijijini ila Mama akaupiga mwingi kwa kuhakikisha nao wanapata barabara inayotoka Mpombwe hadi Kipwa. Kwa Kipwa na vijiji vya jirani Mama atazoa kura kwa 100%.

Wananchi wa Kigoma walioingizwa kwenye gridi ya Taifa ya umeme hawajui kitu zaidi ya Samia. Barabara ya Nyakanazi - Kasulu ikimalizika kujengwa ndo Mama Samia atawachanganya zaidi Kigoma na kuzoa kura 100%.
 
ukizungumza habari tofauti na CCM na kiongozi wake mkuu comrade Dr Samia Suluhu Hassan, wanainchi wa maeneo hayo kwanza...
Mfano halisi hapa Arusha (chugastani) nenda samunge,soko kuu au kirombero waambie ccm na Gambo hawafai hao kina mama watakuponda na nyanya
 
Mpaka hapa inaonekana hujui unachokiongea.
yaani wew ungekua kwenye mkutano wa hadhara maeneo ambayo nimeyasema kwenye hoja yangu ya msingi wangeshasambaa kitambo sana wakuache mkutanoni pekeyako, yaani unajiandaa kupotosha umma 🐒
 
Habari wakuu Mimi Nina certificate ya laboratory technician pia Nina experience ya miaka 3 kuhusu laboratory technician, laboratory analysis, QC,QA pia blending oparetor au syrup oparetor pia naweza kufanya kazi popote pale penye maabara au panapozalishwa bidhaa .yeyote atakaye nisaidia kupata connection ya job nipo tayari kumpa % kadhaa katika mshahara kama shukurani
 
Rais Samia, kazi indelee,
  • Mti wenye matunda kurushiwa mawe si ajabu we vumilia people will see the difference,
  • lakini nikuombe usizibe masikio kwenye hoja muhimu zinatishia mustakabali wa Taifa letu hasa umoja wetu na mshikamano, mf. nidhamu kazini, rushwa kukithiri, ukwepaji wa kodi, matumizi ya badget yasiyozingatia mapato yetu mf. ununuzi wa magari ya starehe kila mradi kila wizara ambayo ni gharama kubwa kwa uendeshaji badala ya kuelekeza matumizi hayo kwenye kuinua kilimo mf. kukunua matrecta kama alivyofanya Rais mwenzako wa Bukina Faso.
  • kurekebisha sheria ya sifa ya kugombea ubunge ili kuwapa nafasi kizazi kipya kiingie Bungeni, kudhibiti rushwa ktk uchaguzi, kiwango cha elimu kwa mbunge walau iwe digree tunakoelekea kwenye sayansi teclologia si sahihi kubaki na darasa la saba au kujua kusoma na kuandika tu, kiwezekana kuwe na system ya verting kwa kila jimbo yule anayefaa kugombea nafasi hiyo ikitanguliwa na weledi, tabia na msimamo wake ktk kulinda tunu za taifa.
  • kosa kubwa sana kuua kiwanda cha kunoa viongozi (Kivukoni) na kubakisha vijana wakimbiza mwenge na ji wao ni wakwamba wanaweza kuwa viongozi wa baadae wengi wao upatikana wao ni wa ki-fgodfather, kwa maana hiyo haitakuwa rahisi kupata viongozi wenye taranta kutoka jamii ya kawaida kwa sababu si rahisi kuwaona. imebakia kutea watoto wa waliowahi kuwa viongozi,
  • tusianzishe miradi mipya tumalize iliyopo.
  • Suala la Rais Mwinyi kuongezewa muda ni zuri lakini linahitaji umakini vinginevyo litabomoa katiba ya CCM na mila na destuli zake lakini kwa utendaji wa Husein ingependeza hata kama angepewa miaka 5 kabisa ili aiimalishe hali ya uchumi wa zanzibar waliotangulia nahisi walikuwa kwenye kandamizo furani la kutokufanya wanavyoona vema lakini serikali yako na hata ileya JPM waliipa Zanzibar kuamua hatima yao, Mwinyi si mbinafsi anapenda kuiona hali bora ya watanzania wazanzibar ya kesho ikiwa bora zaidi. na kusema kweli kushika kwako nafasi ya uongozi wa juu imempa nafasi ya kwenda exra miles.
  • viongozi wa sa sasa wameneemeka sana mimi mimi naiona postive hama kweli neema hizi ni genuine na siyo jasho la wanyonge, sokama ulivyo Mama wa huruma kuna wiongozi walioitumikia eshima ya Nchi hii hasa chini ya uongozi wa Nyerere baadhi familia zao zinajuta kwa nini wazazi wao walikuwa wanasiasa wameishia katika umaskini, unaweza kufanya jambo.
  • Wastaafuu waliotumikia Taifa katika nafasi mbalimbali hawana mtetezi wengine wanalipwa kidogo sana, watu wenyewe si wengi sana unaweza kuwatazama kwa jicho la huruma na hizo ndo baraka zenyewe,
  • Wewe ni Mwanamke ambaye ungependa mwanamke wa Tanzania aheshimike, suala la (wadada poa ) halina sura nzuri, tunafahamu kuwa dada poa si heshima na ni zao la hali ngumu, uchumi duni na underemployement tamko lako kwa umma la kukemea litakuwa na impact kubwa na kuwapa nguvu wale wanaosimamia maadil.
-Nikuombee kila lenye kheri katika kuwatumikia watanzania.
- Rejea kwenye msemo waMzee wako MH. Aly Hasani mwinyi, ( si vile utakavyokusanya kwa ajiri yako au familia yako, ) suala la msingi ni hadithi yako itakayosimuliwa baada ya kuondoka kwako na lile fungu unalojiandalia katika ulimwengu ujao.
 
Wadau hamjamboni nyote?

Ujenzi barabara ya mwendokasi kuanzia mwenge hadi Tegeta umeanza

Tofauti na maeneo mengineyo ujenzi huu huku kwetu haujaleta foleni wala usumbufu wowote Kwa magari au waenda kwa miguu

Yaani wakazi wa huku mbezi beach tunaendelea na maisha yetu kama kawaida huku ujenzi ukisonga mbele

Pongezi nyingi kwa Serikali ya Rais Samia

Kazi iendelee
 
Wakuu

Mimi ni shabiki namba moja kabisa wa mama (kwa upande wangu) na nilianza kumkubali tangu aliposhika kiti rasmi

Mama alianza vizuri mnoo kiasi kwamba kila mtu kila mwananchi alimpenda na kumfurahia ila sasa hv kiukwel hali ni ngumu sana mama hatusikilizi tena

Alowaweka kama wasaidizi wake ndo wapigaji wakubwa na mama wala haangaiki nao

Alokaribu na mama amshitue kwa mapenz mema kabsa mama arudi kama alivoanza mwanzo,wananchi wanaomuelewa mtaani ni wachache saaaana kuliko vyawa

Wasaidizi wake wanatumia hela mpk wanakosa pa kuziweka wanataman ht kuziotea moto huku wananchi mtaani wanalia na kusaga meno na wala hata hawawajibishwi wala kuulizwa chochote

Wameachwa wale kwa urefu wa kamba zao sasa wamekata kamba wanakula hadi akiba

Mama tunakupenda sana na tunataman ukiwa kama mzazi basi utaona huruma kwa wanao(wananchi)
Wasaidizi wako wanakula kwa kiburi kabsa maana wanajua mama sio mkali

Mwambien mama nataman sana kuona akishika kiti kwa mara nyingine ila kama na yeye kwel anataman kufanya hivo basi asikilize wana mtaani wanalia kilio gani asizibe masikio

Wananchi wanateseka saaaana
 
Back
Top Bottom