Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Salaam wanajukwaa;

Nipo kwenye kipindi fulani hivi cha kutafakari sana Maisha, kusali kuhangaika na namna nzuri yenye baraka ya kuingiza kipato halali na kufuatilia sana mambo mbali mbali yanayoendelea kwenye Dunia hii na haswa hapa nchini kwetu Tanzania.

Leo kuna jambo limekuja ghafla tu kichwani nikasema mhhh labda ngoja niwashirikishe hapa kwenye jukwaa labda tunaweza kupata mawazo tofauti na ninajua Mh. Raisi na wasaidizi wake huwa wanapitia hizi post (thread) za jamiiforum haswa katika mida hii ya jioni prime time. ( Kama kama kuna msaidizi wa raisi unapitia basi naomba umwambie kuna kijana fulani hv ameandika kitu jamiiforum ila hana ajira na bado anajitafuta mtaani)

Twende kwenye mada;
Hizi ni kauli mbiu za uchaguzi tokea tupate uhuru (kwa chama tawala)

1. Julius Nyerere "Uhuru na Umoja"
2. Ali hassan Mwinyi "Ruksa, Mzee wa Ruksa"
3. Benjamin Mkapa " Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe" sema hii kama nitakuwa nimeikosea naomba kusahihishwa
4. Jakaya kikwete "Ari mpya, Kasi mpya, Nguvu mpya"
5. John Magufuli " Hapa kazi tu"

Sasa hapa ndipo kwenye kiini cha mada, Baada ya magufuli kufariki mama samia na wasaidizi wake wakabuni "kazi iendelee" kama kauli mbiu ya kuendeleza yale aliyoyaanza magufuli.

Sasa wazo langu nadhani mwaka 2025 kamati ya uchaguzi ingetengeneza kauli mbiu itayayoonyesha new hope au freshness kwa baadhi ya jamii ya watanzania kwamba Dr. Samia ndio the first elected female president in Tanzania.

Hints za kutengeneza kauli mbiu hii naomba zitengenezwe kutoka kwenye kauli hii "SIASA ZA KISASA NI KUWATUMIKIA WANANCHI KWA KUTATUA SHIDA ZAO, NA SI MANENO TU"

Hapa ninapoongea tayari nishabuni kauli mbiu 20 fupi na zenye kuakisi maendeleo na kuwatumikia watu zaidi kuliko kuwa na maneno tu.

Karibuni sana kwa majadiliano;

NB: Sina ajira yoyote, ajira yangu ni ubunifu tu na mawazo na kutafuta fursa ya kuitumikia nchi yangu, kama kuna msaidizi wa raisi kwenye kata, kitongoji, wilayani, mkoani, Ikulu au afisa mwandamizi wa chama, anaona post hii basi tuwasiliane na tujadiliane na nikutumie mapendekezo yangu labda naweza kupata na mimi sehemu ya kujishikiza na kuitumikia nchi) 0710 782874 na 0693 784003
 
Kodi ya umeme kwa mwezi 2,000. Kila ukinunua umeme unalipa tena kodi za VAT, EWURA na REA. Wameamua kutuangamiza.
EWURA&REA ni Taasisi za Serikali zilizoanzishwa kwa Sheria za Bunge,iweje zinaendeshwa kwa makato kwenye miamala ya kununua huduma za umeme?
Je,hakuna namna ya Taasisi hizi kuendeshwa kwa Kodi zetu kama ilivyo kwenye Taasisi zingine?Kama haiwezekani,zisingeanzishwa/zifutwe.
Kawaida hauwezi kutoka kodi usikowekeza;Huu siyo Wizi wa kimfumo/kitaasisi?
 
Sina mengi ya kuandika, Idara ya Usalama wa Taifa ina changamoto nyingi tuliopo nje tunaziona na Rais asipotuelewa leo iko siku utatuelewa tu.

Nilijiuliza sana maswali mengi dhidi ya mgomo wa Kariakoo wa wafanyabiashara yaani mpaka unapangwa na unafanyika kwa ufanisi Rais hakuwa na taarifa?

Nilizidi kuchanganyikiwa pale nilipomsikia Rais unasema baada ya ule mgomo ulituma watu wako kuchunguza chanzo cha mgomo, yaani ni kweli na kweli kabisa!

Eneo kama Kariakoo ambalo kwa siku kunakanyagwa na watu zaidi ya elfu kumi hakuna vyombo vyako? Yaani pale Kariakoo hakuna usalama wa taifa hata mmoja anayezuga zuga, ila wapo wamejazana Ikulu na suti zao za kaunda suti.

Rais, mfumo wa ulinzi hasa idara hii pendwa sasa inakosa mwelekeo, Maafisa Usalama wa Taifa wa sasa wanavaa neno Afisa. Enzi za Mwalimu hawakuvaa neno Afisa na kuongezea Kaunda suti na kunyoa vipara yaani hawakutambulika ila sasa hivi wanatambulika kiwepesi.

Yanayoendelea katika nchi ni ovyo sana

Tunayaona!

Wakuu wa Wilaya ni wenyeviti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani, unamshangaa mkuu wa Wilaya anakwenda SM 200 pasipo Kutuma hata spy one hr before kucheki mazingira na kusoma upepo na kuangalia nini cha kusema mwisho wa siku anaenda pale anaishia kufukuzwa, hii ni aibu tena aibu kubwa.

Unashangaa Mkuu wa Wilaya uliyemteua kutoka Mbwinde anafika Dar anazoa kundi la wadada na wanaume waliopumzika guest house anawaita Malaya, pyuuuuu, alishindwa kutuma spy waliopo chini yake walau three hrs before ili wampe taarifa nani anamnunua nani na saa ngapi?

Nakushauri Mh Rais, wavue Kaunda suti na kuchanganyikana mtaani ili kufuatilia masuala mbalimbali yanayoendelea chini chini yenye maslahi ya taifa

Asubuh njema Mh Rais na namtakia majukumu mema Senior mpya

Namkumbusha tu kifungo cha shati lake akibandike nzi naye inzi atamsaidia.
 
Hilo sio tatizo mkuu!

Tatizo ni mhusika kuongeza siku za kuendelea kukalia kiti kikuu tofauti na makubaliano waliojiwekea wakati akipewa,akapiga u-turn matokeo yake ndio haya unayoyaona na nahisi yataendelea kuwepo Hadi 2025!!

Haiwezekani eti wafanya biashara wanagoma bila kusikia sauti ya waziri mkuu Bado wanagoma,nani yupo nyuma yao!!?

Destabilizing the regime to be incompetent for the next aimed phase of our incumbent!
 
hivi ndio vitu tanzania unaweza kufanya na bila kuguswa:
1. ukivaa kaunda suti wewe ni usalama ?
2.ukiwa na kofia au shati la ccm uwezi kuwekwa kituoni wala kuhisiwa kwa lolote.
3.ukiwa na v8 au zile gari za watu wasio julikana utapita barabara yoyote bila kubuziwa
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Hakuna taifa linaweza kuendelea bila kujenga nifumo imara na kuiheshimu. As long as wewe unaweka talanta zako kwa maono ya mtu mmoja lazima utakuwa dissapointed. Ndo maana aliyoyafanya Magufuli yamepotea kama barafu juani ni kwa sababu aliamini kwamba ni yeye pekee anaweza kutuvusha.

Rumekuwa taifa la ajabu kuamini kwamba mapungufu ya viongozi wa siasa yatafunikwa na nguvu za polisi, usalama nk. Ndo maana viongozi wetu wanategemea polisi kutawala. Siyo sahihi.
 
Rais Samia shikamoo! nimekuandikia huu ujumbe kukupongeza kwa kutibu magonjwa sugu ya kuwaondoa vijana wasiokuwa na adabu ndani ya serikali yake hongera Sana mama yetu
 
Rais Samia shikamoo! nimekuandikia huu ujumbe kukupongeza kwa kutibu magonjwa sugu ya kuwaondoa vijana wasiokuwa na adabu ndani ya serikali yake hongera Sana mama yetu

Kwa hiyo wewe umeanza kumuunga mkono Mh. Rais baada tu ya kuwatumbua vijana wasiopendwa na wengi, mbona umechelewa sana, sisi wenzako tokea ile March 2021, tulikula amini na kufunga tuko na Mama ije mvua, jua, tetemeko, volcano, hata tushikiwe bastola vichwani tuko na Mama kufa na kupona, Mama yetu ni Rais kweli kweli, hana kelele wala majigambo, mtulivu, msikivu, anayefanya maamuzi sahihi kabisa tena bila ushabiki, anatenda haki kwa haki, Mungu amlinde Daima na milele.

Kazi iendelee, hongera sana Mh. Rais wetu.
 
Bado Mwigulu!.
Hata Makonda sijui alimrudisha wa kazi gani...hakuna watz wengine hodari kuhudumu hizo nafasi??.
Mtu kama Ally Happy alishapata mtaji na kujiajiri kupitia kilimo eti unaenda kumrudisha tena kuwa mkuu wa mkoa hiyo akili au matope?!
 
Rais Samia shikamoo! nimekuandikia huu ujumbe kukupongeza kwa kutibu magonjwa sugu ya kuwaondoa vijana wasiokuwa na adabu ndani ya serikali yake hongera Sana mama yetu
Bado ana kosa usafi kwa kuendelea kumlinda Mwigulu.
Huwa ana chelewa sana kufanya maamuzi huku wasaidizi wake wakiendelea kumharibia.
Mwigulu ana makandokando mengi sana.
Ila jicho la tatu la Mama kina ficha Mama asiyaone.
Hii ina endelea kuharibu huku site..
 
Back
Top Bottom