Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Wakuu wa Wilaya hawana Kazi, wafutwe! Hawamo hata ktk Katiba! Huapishwa na Wakuu wa Mikoa na siyo Rais! Kazi ya kusimamia Maendeleo ni ya Wakurugenzi wa Halmashauri! Ma- DC, eti ni Wenyeviti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya! Waachiwe Polisi kazi hiyo, na kuwajibika kwa IGP! Ma-RC, badala ya kuhudhuria Sherehe tu, wasimamie Wilaya zao zote, wao wenyewe, wakiwa wawakilishi wa Rais! Itapunguza sana Gharama za Serikali!
 
na bado gharama za chuo zipandishwe tuu,si huwa hamsikii na kuelewa,wahenga walisema majuto ni mjukuu na kufka 2020 muimbe mbele kwa mbele tuu,komen japo na mm n mwanachuo
 
Hakuna MTU ambaye haombi ushauri , na kiongozi bora lazima usikilize ushauri ongeza na zako Fanya maamuzi

Mkuu ansvin usiwe na haraka kwa kusoma title za post tu. ungesoma post yote ungeona sijasema asiwe na washauri. Angalia hapa chini

Lakini kuwa na washauri ni jambo nzuri tu - ila sasa tafuta washauri wako mwenyewe, watu wasio rafiki zako ambao wanaeleweka kuwa na busara na uzoefu katika uongozi, bila kuwa na haja ya kukufurahisha wewe kibinafsi, kutafuta urafiki na wewe au kujipendekeza kwako
 
Wasomi huwa mnajifanya hamkiungi chama cha mapinduzi kwa kujifanya kimbelembele na ukawa mfate boom ukawa sasa na boom hampati tukiwahurumia sana tutawapa 12000 wengne tu au tusiwape kabisa hatuna pesa za kuchezea kuwapa wasiotuunga
 
Mtihani wa kwanza kwa JPM ni kuondoamentality ya watanzania ya kutaka kufanyiwa kila kitu. Watanzania wana tabia ya kutaka vyabure.Watanzania wamezoea patronage andclientelistic system ya kuwa na mtu anayeweza kukufadhili kwa fedha na mambomengine.Ndiyo maana utaona wanasemambunge huyu ametufanyia hiki na kile ni lazima tumchague.Hata Magufuli (PhD) naye ameahidi vitu vingivya kuwafanyia watanzania wapenda dezo.Watanzania ni wavivu wa kufanya kazi.Kwa kuliona hili Magufuli (PhD) amekuja na msemo HAPA KAZI TU.Huu ni msemo wenye maana kubwa sana kwenyeuongozi wa JPM.Pamoja na kuwahidiwatanzania vitu vingi lakini ni wazi mwisho wa siku anataka watanzania wafanyekazi.Tabia ya watanzania wanataka serikaliiwanyie kila kitu.Jiji la Dar es Salaamni chafu kupindukia lakini wanataka halmashauri ya jiji ndiyo iwajibike kwayote.Lakini ni watanzania na wakazi wajiji hao hao wanaotupa taka hovyo mitaani na kujisaidia haja ndogo na kubwa nahata kuleta kipindupindu ugonjwa ambao ni wa aibu.
Ni mentality hii ya watanzania ndiyoinayofanya pamoja na kuwepo kwa kamati za shule lakini shule nyingi hazinavyoo. Watanzania wanataka mtu ajeafadhili ujdenzi wa choo.Watanzaniawanataka pia mtu aje afadhili utengenezaji wa madawati ya wanafunzi kwa shuleza msingi.Wananchi wenyewe wanashindwakujipanga kuendesha harambee ya kuhakikisha madawati yanatengenezwa.

Kila mji wa Tanzania wamejaa watu wanaoitwamadalali sijui wa nyumba, shamba, mazao na kadhalika. Madalali wana vitambi na kazi yao nikupandisha bei ya vitu ikiwemo mashamba, mazao, vyumba vya kupanga nakadhalika.Eti wao ni watoto wa mjinikazi yao ni kutumia kinachoitwa bongo......

Yaani watanzania ni watu wa ajabu kwa mambomengi, watu wanaotaka sifa, wanaotaka kutumia bila kufanya kazi, walalamishi,wapenda sifa, wapika na wapiga majungu, wanaolialia hovyo, wasio na ni nidhamuya maisha, wavivu na wapenda vya dezo.....

Kwa hakika JPM (PhD) ana kazi kubwa yakubadili mentality hii miongoni na ndani ya jamii.
Serikali inatoza kodi watu wake, kazi ya kodi hizo ni nini? Serikali iweke miundombinu kama maji, umeme, barabara, elimu, afya, na usalama ili kutoa mazingira bora kwa wananchi kuwekeza akili, nguvu na mitaji yao kwa urahisi.
 
Rais Magufuli aunde Wizara ya Habari na Mawasiliano! TCRA iwe chini ya Wizara ya Habari, badala ya sasa Habari kusimamiwa na Wizara 2 tofauti - Habari (Magazeti n.k.) na ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano (TV, Radio, Mitandao)! Tozo za Simu, Leseni za TV/Radio, zingeimarisha Sekta ya Habari, ambayo siku zote haina kitu! Kuna mkanganyiko, TBC, inasimamiwa na Wizara ya Habari, Jengo lake Mikocheni, lililoanza Miaka ya 1990 (zaidi ya Miaka 20 iliyopita!), halijaisha, wanaishi popo! Wizara ya Habari, inapanga! TCRA, wanachezea pesa, ndiyo maana wana Jengo kubwa, Ubungo!
 
Ushauri wako mzuri ila mwongezee kukumbuka ahadi zake kwetu. Asipozitenda ajue kuwa 2020 zitakuwa fimbo ya kumtandikia.
Pamoja na uzoefu wetu wa "goli la mkono" 2020 halitapita. Wtz wamesha amka na sasa hawatakubali tena kampeni za kitoto za kuwadhalilisha watu. Wanataka uwaambie ulifanya nini tu katika kipindi chako. Kama huna uwezo wa kuwaonesha a realy BRN kaa kando wala fomu ya urais usichukue.
 
Si hao hao? Wataacha kuombana ushauri jinsi ya kuendeleza umaskini wetu?
 
kutegemea ushauri wa jk na mkapa lazima aliwe tu. ameingizwa mkenge kuteua masaju kuwa AG...
 
Kama ameweza kufaulu mtihani mkuu ambao umemfikisha hapo alipo hivi sasa.

Basi hiyo mingine haiwezi kuwa mitihani hata siku moja, labda twaweza iita ni majaribio
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom