Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Usiwe na tomaso magufuli usimfananishe na jk hata robo subili uone tatizo in mfumo ndo unafanya watu wasifanye Kazi ofisini au walikosa MTU wa kuwasimamia

rais atamsimamia kila MTU peke yake? huo usimamizi unatakiwa uanzie juu. acha kujitoa akili.
 
Waandishi wa habari mithili ya kubenea ...!!

Hawa ndio sumu ya maendeleo ya Taifa.
Kubenea mwandishi wa habari toka lini. Yule kanjanja wa utapeli kwa wananchi.?
Yule alituaminisha kuwa Lowasa na sumaye ni mafisadi wa kutupwa katika nchi hii. Hili kovu halitasahaulika kamwe. Kapewa vijipesa tu akaamua kipindisha ukweli aliousimamia
 
Kwa mini unafikiria kuwa atashidwa ? Na usifikikie ataweza? Je kama aliweza alikokuwa kwanini hasiweze sasa?
Kuna haja ya kutohukumu kitu usichokijua matokeo yake,

usidhani kuongoza wizara moja ni sawa na kuongoza nchi. acha kukariri vibaya mkuu.
 
Mimi nitarudisha imani yangu kwake kama ataweza kuifumua upya katiba pendekezwa
 
Watu wengi wanaishi wilayani na mahitaji yao mengi yanatatuliwa wilayani hukohuko, hivyo kuweka watendaji mahili na wabunifu kwenye ngazi ya wilaya ndio mtihani wa kwanza wa rais Magufuli. Wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa JK sio kabisa, na huwenda ndio chanzo cha migogoro mingi ya wananchi dhidi ya serikali yao. JPM hana namna nyingine zaidi ya kuwaweka pembeni watendaji wote wavivu na wabadhilifu wilayani na mikoani ambao wengi wao wameshachukiwa tayari na wananchi wao.

Mtihani wa pili ni namna atakavyo atakavyotumia uwezo wake kupambana wa watu wajanjawajanja kama vile akina Lyatonga, Chenge, Tibaijuka, Manji, Aziz, Nazir, Harison, Samuel na wengine. Kwa muonekano wao ni wapenda sifa binafsi na kujali maslahi yao tu.

Mtihani wa tatu ni namna atakavyoweza kukaa mbali na kundi la mzee Mkapa waliohusika na kuuza viwanda, migodi, mabenki, mashamba, nyumba za serikali na hata waliotajwa kwenye kashifa ya EPA, meremeta, rada, ndege ya rais, n.k, ambao ni chanzo kikubwa leo cha ukosefu wa ajira kwa vijana na ongezeko kubwa la deni la taifa.

Mtihani wa Nne ni namna ya atakavyopambana na wimbi la watoto na wajukuu wa viongozi wa wakuu wa CCM wanaotaka kupewa nafasi serikalini kwa upendeleo kutumia nafasi za wazazi wao.

Mtihani wa Tano ni namna atakavyoweza kupambana na udini, ukabila, na ukanda katika kutoa nafasi za ajira nchini. Hali ilivyo hivi sasa ni mbaya sana, ajira wizarani, kwenye vitengo mbalimbali, mialiko kwenye mikutano, semina na nafasi za mafunzo inatolewa kwa ukanda, ukabila, udugu na udini.

Asipozingatia haya atahesabika kuwa ameanza na mguu mbaya sana utakaomgarimu sana uchaguzi wa 2020.

Mtihani wa kwanza kwa JPM ni kuondoamentality ya watanzania ya kutaka kufanyiwa kila kitu. Watanzania wana tabia ya kutaka vyabure. Watanzania wamezoea patronage andclientelistic system ya kuwa na mtu anayeweza kukufadhili kwa fedha na mambomengine. Ndiyo maana utaona wanasemambunge huyu ametufanyia hiki na kile ni lazima tumchague. Hata Magufuli (PhD) naye ameahidi vitu vingivya kuwafanyia watanzania wapenda dezo. Watanzania ni wavivu wa kufanya kazi. Kwa kuliona hili Magufuli (PhD) amekuja na msemo HAPA KAZI TU. Huu ni msemo wenye maana kubwa sana kwenyeuongozi wa JPM. Pamoja na kuwahidiwatanzania vitu vingi lakini ni wazi mwisho wa siku anataka watanzania wafanyekazi. Tabia ya watanzania wanataka serikaliiwanyie kila kitu. Jiji la Dar es Salaamni chafu kupindukia lakini wanataka halmashauri ya jiji ndiyo iwajibike kwayote. Lakini ni watanzania na wakazi wajiji hao hao wanaotupa taka hovyo mitaani na kujisaidia haja ndogo na kubwa nahata kuleta kipindupindu ugonjwa ambao ni wa aibu.
Ni mentality hii ya watanzania ndiyoinayofanya pamoja na kuwepo kwa kamati za shule lakini shule nyingi hazinavyoo. Watanzania wanataka mtu ajeafadhili ujdenzi wa choo. Watanzaniawanataka pia mtu aje afadhili utengenezaji wa madawati ya wanafunzi kwa shuleza msingi. Wananchi wenyewe wanashindwakujipanga kuendesha harambee ya kuhakikisha madawati yanatengenezwa.

Kila mji wa Tanzania wamejaa watu wanaoitwamadalali sijui wa nyumba, shamba, mazao na kadhalika. Madalali wana vitambi na kazi yao nikupandisha bei ya vitu ikiwemo mashamba, mazao, vyumba vya kupanga nakadhalika. Eti wao ni watoto wa mjinikazi yao ni kutumia kinachoitwa bongo......

Yaani watanzania ni watu wa ajabu kwa mambomengi, watu wanaotaka sifa, wanaotaka kutumia bila kufanya kazi, walalamishi,wapenda sifa, wapika na wapiga majungu, wanaolialia hovyo, wasio na ni nidhamuya maisha, wavivu na wapenda vya dezo.....

Kwa hakika JPM (PhD) ana kazi kubwa yakubadili mentality hii miongoni na ndani ya jamii.
 
Watu wengi wanaishi wilayani na mahitaji yao mengi yanatatuliwa wilayani hukohuko, hivyo kuweka watendaji mahili na wabunifu kwenye ngazi ya wilaya ndio mtihani wa kwanza wa rais Magufuli. Wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa JK sio kabisa, na huwenda ndio chanzo cha migogoro mingi ya wananchi dhidi ya serikali yao. JPM hana namna nyingine zaidi ya kuwaweka pembeni watendaji wote wavivu na wabadhilifu wilayani na mikoani ambao wengi wao wameshachukiwa tayari na wananchi wao.

Mtihani wa pili ni namna atakavyo atakavyotumia uwezo wake kupambana wa watu wajanjawajanja kama vile akina Lyatonga, Chenge, Tibaijuka, Manji, Aziz, Nazir, Harison, Samuel na wengine. Kwa muonekano wao ni wapenda sifa binafsi na kujali maslahi yao tu.

Mtihani wa tatu ni namna atakavyoweza kukaa mbali na kundi la mzee Mkapa waliohusika na kuuza viwanda, migodi, mabenki, mashamba, nyumba za serikali na hata waliotajwa kwenye kashifa ya EPA, meremeta, rada, ndege ya rais, n.k, ambao ni chanzo kikubwa leo cha ukosefu wa ajira kwa vijana na ongezeko kubwa la deni la taifa.

Mtihani wa Nne ni namna ya atakavyopambana na wimbi la watoto na wajukuu wa viongozi wa wakuu wa CCM wanaotaka kupewa nafasi serikalini kwa upendeleo kutumia nafasi za wazazi wao.

Mtihani wa Tano ni namna atakavyoweza kupambana na udini, ukabila, na ukanda katika kutoa nafasi za ajira nchini. Hali ilivyo hivi sasa ni mbaya sana, ajira wizarani, kwenye vitengo mbalimbali, mialiko kwenye mikutano, semina na nafasi za mafunzo inatolewa kwa ukanda, ukabila, udugu na udini.

Asipozingatia haya atahesabika kuwa ameanza na mguu mbaya sana utakaomgarimu sana uchaguzi wa 2020.

Nyie usalama wa taifa mlioko humu...tunaombeni mpelekee mheshimiwa huu ushauri kabla ya Hawa wapiga dili hawajamzunguka magufuli. Tafdhalini mpeni huu ushauri ausome.
 
Mbona mtihani wa kwanza ameshafeli........... AG

Ulitaka AG amchague lissu mkuu? Au yupo ambae unamuona anafaa zaidi ya huyo alieteuliwa na Rais?kwa sisi tunaemfahamu AG sio bwanyenye huingia front mwenyewe kwa ishu nyingi za kimahkama.
 
Hakuna MTU ambaye haombi ushauri , na kiongozi bora lazima usikilize ushauri ongeza na zako Fanya maamuzi
 
Ulitaka AG amchague lissu mkuu? Au yupo ambae unamuona anafaa zaidi ya huyo alieteuliwa na Rais?kwa sisi tunaemfahamu AG sio bwanyenye huingia front mwenyewe kwa ishu nyingi za kimahkama.

hahaha! mkuu una akili za kiQUMER sana. eti huoni mtu mwingine sifa zaidi ya masaju?
 
kinachotakiwa ni kumuombea afanye kaz kama alivyoapa tar5.11 2015 mungu akuongoze rais wetu magufuli.but usitake ushaur kwa kikwwte hata mkapa watakupotosha.NAKUTAKIA KAZI NJEMA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom