Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Jambo moja ambalo Magufuli aliliona wazi katika kampeni zake ni kwamba Watanzania wanataka mabadiliko, na kwamba wengi walihisi mabadiliko haya yangeletwa na UKAWA. Magufuli akaahidi kwamba yeye ataleta madadiliko Watanzania wanayotaka.

Ushauri wangu kwa Magufuli ni kwamba kama kweli kweli anataka kuwaletea Watanzania mabadiliko - basi asiwe mtu wa kutafuta ushari kwa Kikwete na Mkapa. Wao walikuwa na nafasi ya kuletea Watanzania mabadiliko, na wengi waliona kuwa kwa sehemu kubwa walishindwa kuleta mabadiliko yaliyotakiwa, japo kulikuwa a mafanikio kataka sehemu chache.

Magufuli be your own man and master - Personality yako, kufikiri kwako na kule kwa kwa Kikwete na Mkapa ni tofauti kabisa na Watanzania wanategemea hilo litaleta mabadiliko wanayotarajia. Kuendelea kupokea ushauri toka kwa Kikwete na Mkapa ni kuwapa Watanzania mvinyo ule ule wa zamani katika glasi mpya; hilo ni hatari sana, na linaweza kukufanya uongoze kwa miaka mitano tu na kushindwa uchaguzi ujao.

Tunajua Kikwete a Mkapa walikuwa na mchango kukufanya uwe Raisi wa Tanzania - washukuru yaishie hapo. Waambie wakapumzike sasa, kazi yao imekwisha. Kuendelea kupokea ushauri wao kila wakati utajikuta unafanya kazi ili kuwaridhisha wao na sio Watanzania waliokuchagua. Pia epuka sana kupokea ushauri wao kwa mambo ambayo hujawaomba ushauri.

Lakini kuwa na washauri ni jambo nzuri tu - ila sasa tafuta washauri wako mwenyewe, watu wasio rafiki zako ambao wanaeleweka kuwa na busara na uzoefu katika uongozi, bila kuwa na haja ya kukufurahisha wewe kibinafsi, kutafuta urafiki na wewe au kujipendekeza kwako
 
Tatizo ni mfumo......atabebwa na mawimbi tu na ndio maana ccm naichukia

Hapo umesema ukweli mkuu.
Hana ubavu wa kuuvunja mfumo.

Yaani atyumbishwa vibaya sana na wazee wa chama chake. Kwa mtazamo wangu naweza kusema Magufuli atakuwa Rais ambaye atawaangusha watu wengi zaidi ya walivyotarajia. Tutamuona Kikwete bora mara mia kuliko huyu.
 
Ingekua awamu ya pili,bado mgeni kuna mambo lazima aombe ushauri,nchi ngumu hii
 
Watu wengi wanaishi wilayani na mahitaji yao mengi yanatatuliwa wilayani hukohuko, hivyo kuweka watendaji mahili na wabunifu kwenye ngazi ya wilaya ndio mtihani wa kwanza wa rais Magufuli. Wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa JK sio kabisa, na huwenda ndio chanzo cha migogoro mingi ya wananchi dhidi ya serikali yao. JPM hana namna nyingine zaidi ya kuwaweka pembeni watendaji wote wavivu na wabadhilifu wilayani na mikoani ambao wengi wao wameshachukiwa tayari na wananchi wao.

Mtihani wa pili ni namna atakavyo atakavyotumia uwezo wake kupambana wa watu wajanjawajanja kama vile akina Lyatonga, Chenge, Tibaijuka, Manji, Aziz, Nazir, Harison, Samuel na wengine. Kwa muonekano wao ni wapenda sifa binafsi na kujali maslahi yao tu.

Mtihani wa tatu ni namna atakavyoweza kukaa mbali na kundi la mzee Mkapa waliohusika na kuuza viwanda, migodi, mabenki, mashamba, nyumba za serikali na hata waliotajwa kwenye kashifa ya EPA, meremeta, rada, ndege ya rais, n.k, ambao ni chanzo kikubwa leo cha ukosefu wa ajira kwa vijana na ongezeko kubwa la deni la taifa.

Mtihani wa Nne ni namna ya atakavyopambana na wimbi la watoto na wajukuu wa viongozi wa wakuu wa CCM wanaotaka kupewa nafasi serikalini kwa upendeleo kutumia nafasi za wazazi wao.

Mtihani wa Tano ni namna atakavyoweza kupambana na udini, ukabila, na ukanda katika kutoa nafasi za ajira nchini. Hali ilivyo hivi sasa ni mbaya sana, ajira wizarani, kwenye vitengo mbalimbali, mialiko kwenye mikutano, semina na nafasi za mafunzo inatolewa kwa ukanda, ukabila, udugu na udini.

Asipozingatia haya atahesabika kuwa ameanza na mguu mbaya sana utakaomgarimu sana uchaguzi wa 2020.

= mahiri
= huenda
= wabadhirifu
= Harrison

Tatizo kubwa kabisa ni ujinga wa asili. Nnauhakika hata yeye hawezi kuuondoa.
 
Ha Ha haa: Wewe juzi hukumchagua, kwa nini unamshauri? Suala hilo tuachie sisi tuliomchagua.
 
HNi muujiza kusukuma gari ukiwa ndani yake.

Madenge tu wa sani ndo anaweza.
 
Tunajua Kikwete a Mkapa walikuwa na mchango kukufanya uwe Raisi wa Tanzania - washukuru yaishie hapo. Waambie wakapumzike sasa, kazi yao imekwisha. Kuendelea kupokea ushauri wao kila wakati utajikuta unafanya kazi ili kuwaridhisha wao na sio Watanzania waliokuchagua.
ushauri wako unaweza kuwa na mantiki, ila hilo unalolitaka wewe haliwezekaniki.
 
Ingekua awamu ya pili,bado mgeni kuna mambo lazima aombe ushauri,nchi ngumu hii

Hapo ndipo tatizo litakapoanzia - kujenga silka ya kuomba ushauri. Anapaswa kutengeneza njia yake mwenyewe; kwani Nyerere alijifunza kutoka awamu ipi alipochukua uraisi mara ya kwanza?
 
No vision no Mission ... Hajui aendako je? atafikaje bila Msaada wa wale wale ? ... CCM ni ile ile ..
 
Ha Ha haa: Wewe juzi hukumchagua, kwa nini unamshauri? Suala hilo tuachie sisi tuliomchagua.

Watanzania wapo karibu milioni 50, waliomchagua Magufuli ni milioni 8. Sasa sikujua kwamba Magufuli anakuwa raisi wa wale milioni 8 tu waliomchagua kama unavyotaka wewe.

Hata hivyo mie siku zote siko upande wa CCM wala UKAWA - neutral. Wote nyie ni ndugu zangu; Akiwa Magufuli Raisi sawa; Lowasa sawa; Wasira sawa; Sugu sawa; Slaa sawa; Mrema sawa; Zitto sawa nk; ili mradi tu awe kiongozi mzalendo atakaeleta mabadiliko ya kweli kwa Tanzania na wananchi na kila mtu aone hivyo.
 
Uchaguzi ulisha kwisha good enough tuna katiba ambayo inasema mtu akishwa tangazwa basi ndiyo raisi na huna uwezo wa kupinga matokeo hayo popote its good when it is your turn but mind you atakuja tokea chizi mmoja me or ke ambaye ataamua kumuingiza mkewe au mmewe kwa kujua siku ya siku yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya urais atamtangaza spouse wake kutakucha, tuyaache hayo.

Binafsi kama ningepata wasaa wa kuongea na magufuli ningemshauri haya yafuatayo

1. Hali ya hudumu ya afya ya Tanzania ni mbaya mbaya mbaya hakuna daktari aliye na moyo wa kufanya kazi kwa moyo ule uliokuwapo mwanzo. Mfano, hospitali yetu ya taifa ambayo ni tegemeo ya maskini wote wa Tanzania na daraja la viongozi kupita kwenda India huduma ni hovyo hovyo.

Hivi unajua kuwa huduma za CT Scan na MRI Muhimbili zimesimama Zaidi ya miezi minne na hakuna anayejali. Watu wa wizara ya afya naona hawajali kabisa.

Mimi nashauri wizara ya afya isihusike moja kwa moja na Muhimbili kama mtafuta habari nilienda pale, hakuna mwenye nia za dhati wa kuikomboa sekta ya afya.Wao wanachotaka serikali iendelee kupeleka watu India ili waendelee kupata pesa wanazopata wanajua namna wanavyopata, si watu hawa tunakufaa maskini.

2.Taasisi ya mifupa MOI tunaomba ijipambanue kama ni taasisi ya umma au ni kama Agha Khan kwani huduma zinazotolewa hapa afadhali malipo yake yangekuwa na risiti basi ni ujanja ujanja tu.

Heri na feri kwenye soko la samaki kuliko hapo, elimu yao haifanani na huduma wanazotoa.


Mimi naomba kama kama una power hiyo hizi taasisi ziwe chini yako kwani afya ya watu unaowaongoza ni muhimu saaana tena sana elimu ifuate.
 
Kuuza viwanda na nyumba yeye ndo alikuwa boss wao hatawaepuka
 
Mkuu chikub kupenda sifa si shida kama wafanya kazi vizuri. Hata Magufuli ni mpenda sifa, na sasa kapewa dhamana ya Urais.
Lakini Magufuli ana resources kubwa sana za kujua watu, ambao bahati nzuri wengi wao kafanya nao kazi sehemu mbalimbali. Sasa kila mtu anajifanya mwenye hekima wa kutoa ushauri.
Magufuli ameshachaguliwa kuwa Rais, mengine kama ya uteuzi tumwache afanye mwenyewe sawasawa na vyombo husika vinavyomshauri. Hatafuti Malaika, anatafutwa mchapakazi. Tutoe ushauri kwa policies huko... Sio uteuzi. Tutapoteza muda.
 
Last edited by a moderator:
hivi naye JPM yupo humu jf aipate hiyooo!? inapendeza sana akichabo japo kwa sekunde kadhaa humu jf ili kuona mawazo nyeti na adimu ya watz.
 
Mkuu uzuri wa Raisi unapimwa kwa kutokana na kukataa ushauri wa watangulizi wake?? haya ngoja wamwachie issue ya Zanzibar tuone, acheni u bogus bwana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom