Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
MATARAJIO YANGU KWA JOHN POMBE MAGUFULI
Baada ya kuapisha kuwa Rais wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05.11.2015 (10:49 A.M), mimi kama raia wa Tanzania nina matarajio yafuatayo kwa Mh. Dr.John Pombe Magufuli.
? Kutatua haraka tatizo la Zanzibar lililotokana na ZEC kufuta uchaguzi pasipo na sababu za Kimsingi.Hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa na Wananchi wake.
? Kuwaunganisha Watanzania ambao wametofautiana kutokana na Vyama vya siasa kuwagawa kwa misingi ya itikadi za vyama,dini,makabila na ukanda wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba,25,2015.Makovu haya ni mengi na kwa watu wote sehemu zote.
? Kuinua ari ya uwajibikaji na uchapakazi Serikalini na watu binafsi na Viongozi wote watakaozembea wawajibishwe mara moja.
? Kuboresha huduma za afya katika Hospitali zote nchini na Zahanati na kuepuka Viongozi kwenda kutibiwa nje ya nchi.
? Kuhakikisha kila anayepaswa kupata elimu anaipata na hatimaye kufuta ujinga ambao umekithiri sana hivi karibuni.(Rejea kura nyingi kuharibika)
? Kuwashughulikia wote waliohusika na watakaohusika na rushwa (Matumizi mabaya ya Ofisi na mali za Umma kwa manufaa yao binafsi)
? Kuboresha Viwanda vilivyokuwepo kwa kuvipatia ruzuku na kuondoa mlolongo wa kodi na michango ambayo badala ya kuviendeleza huviumiza zaidi.
? Utatuzi wa matatizo ya wakulima uwe wa kweli na wenye tija.Matatizo kama pembejeo,masoko,mitaji n.k huwarudisha nyumba sana wakulima na hatimaye Taifa.
? Ajira kwa Vijana ambao wanamaliza shule na vyuo. Kuiunua viwanda,kufufua kilimo,kukomesha rushwa,uwajibikaji na elimu za ufundi kwa pamoja zitatoa ajira kwa vijana.
? Kutokomeza umaskini wa kipato kwa wananchi wa hali ya chini kwa kufufua kilimo,kutoa ajira,kukomesha rushwa na kutoa huduma safi za afya.
? Kupunguza pengo kati ya wenye nacho na wasionacho (Tajiri na Maskini) kwa kupunguza mianya ya unyonywaji kwa wasionacho.
Ni matumaini yangu kila Mtendaji atatoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha haya na JPM atafuatilia kwa ukaribu watendaji wasio na tija wenye nia ya kuendekeza ulaji na upigaji wa madili badala ya kuleta maendeleo.
 
hilo kundi la watoto na wajukuu wa viongozi wa ccm ni balaa tupu...
 
Mkuu uzuri wa Raisi unapimwa kwa kutokana na kukataa ushauri wa watangulizi wake?? haya ngoja wamwachie issue ya Zanzibar tuone, acheni u bogus bwana

Wakati fulani ndio. Raisi anatakiwa kwa kiasi kikubwa awe independent thinker, sio kila kitu aombe ushauri.

Pia kwa Magufuli suala lililopo ni kama uongozi wake utakuwa ni muendelezo wa style au mfumo ule ule wa uongozi wa kina Mkapa na Kikwete. Kama wao watakuwa ndio washauri wake wakuu, basi mfumo wa uongozi hautabadilika, na wananchi hawataona mabadiliko wanayotaka.
 
Mkuu malipo ya huduma halali pale Taasisi MOI unapatiwa risiti tena kuanzia saa 1:30 - 9:30 unalipia NMB hapohapo MOI then unapeleka risiti yako kwa macashier wao wanakupatia risiti yako. Baada ya muda huo utapata risiti ya cashiers tu cause NMB watakuwa wamefunga. Kuhusu huduma Taasisi inategemea fund (OC) kutoka Serikalini ili kujiendesha kiufanisi zaidi hapo ndo tatizo unapaswa kuliwekea mkazo. All in all ujumbe utawafikia walengwa
 
Jambo moja ambalo Magufuli aliliona wazi katika kampeni zake ni kwamba Watanzania wanataka mabadiliko, na kwamba wengi walihisi mabadiliko haya yangeletwa na UKAWA. Magufuli akaahidi kwamba yeye ataleta madadiliko Watanzania wanayotaka.

Ushauri wangu kwa Magufuli ni kwamba kama kweli kweli anataka kuwaletea Watanzania mabadiliko - basi asiwe mtu wa kutafuta ushari kwa Kikwete na Mkapa. Wao walikuwa na nafasi ya kuletea Watanzania mabadiliko, na wengi waliona kuwa kwa sehemu kubwa walishindwa kuleta mabadiliko yaliyotakiwa, japo kulikuwa a mafanikio kataka sehemu chache.

Magufuli be your own man and master - Personality yako, kufikiri kwako na kule kwa kwa Kikwete na Mkapa ni tofauti kabisa na Watanzania wanategemea hilo litaleta mabadiliko wanayotarajia. Kuendelea kupokea ushauri toka kwa Kikwete na Mkapa ni kuwapa Watanzania mvinyo ule ule wa zamani katika glasi mpya; hilo ni hatari sana, na linaweza kukufanya uongoze kwa miaka mitano tu na kushindwa uchaguzi ujao.

Tunajua Kikwete a Mkapa walikuwa na mchango kukufanya uwe Raisi wa Tanzania - washukuru yaishie hapo. Waambie wakapumzike sasa, kazi yao imekwisha. Kuendelea kupokea ushauri wao kila wakati utajikuta unafanya kazi ili kuwaridhisha wao na sio Watanzania waliokuchagua. Pia epuka sana kupokea ushauri wao kwa mambo ambayo hujawaomba ushauri.

Lakini kuwa na washauri ni jambo nzuri tu - ila sasa tafuta washauri wako mwenyewe, watu wasio rafiki zako ambao wanaeleweka kuwa na busara na uzoefu katika uongozi, bila kuwa na haja ya kukufurahisha wewe kibinafsi, kutafuta urafiki na wewe au kujipendekeza kwako

Kula like ya nguvu mkuu, wangalau wewe ummempa ushauri wa uhakika. Asikubaliane kabisa na ushauri ambao hajaomba na katika cabinet yake ya washauri ajitahidi kuweka na wapinzani maana watampa picha halisi ya kili kinachoendelea. Uzoefu unaonyesha wanaccm wengi huwa wanatoa ushauri anaopenda kuusikia boss wao ili wapate maslahi binafsi. Pia namshauri asome mitandao ya kijamii pindi anapopata nafasi ili wangalau apate maoni yetu sisi tusiouma maneno, na akiweza kuanzia january aanza kubadili viongozi walioteuliwa na rais aliyemaliza muda wake, kwani wengi walipata vyeo kama fadhila ama kulinda maslahi binafsi. Aepuke tafrija za wafanya biashara lakini awatendee haki. Kwenye ile list ya wapiga debe 32 wa ccm awaepuke sana kwenye eneo la uwaziri maana wale ndio wahuni wenyewe ambao ndio remote za hao marais wawili waliopita.
 
Ha Ha haa: Wewe juzi hukumchagua, kwa nini unamshauri? Suala hilo tuachie sisi tuliomchagua.

Kuchagua ni ushindani tunaweza kumchagua yoyote, ila akishakuwa rais ni wa wote na anapaswa sio ombi kutusikiliza wote. Mbona wakati wa kukusanya kodi anakusanya mpaka zetu ambao hatukumchagua? Halafu sisi ambao hatukumchagua hatumpi ushauri wa kujipendekeza tunampa ushauri ulionyooka. Kama ni hivyo inabidi tume ya uchaguzi ndio imshauri zaidi maana imetoa kura nyingi kuliko hiyo yako moja, nguruwe pori wewe.
 
1/
Waandishi wa habari ni watu wa muhimu sana kama source chokonozi dhidi ya madudu!
2/
Tunaomba usiwaghasi wala kuwasumbua au kuwaona ni maadui dhidi ya dhamira yao hasa juu ya kufichua madudu!
3/
Tulegezee sheria za mitandao ili watu wote wawe huru mara waonapo madudu popote pale wayaonapo,hapa utawaweka watanzania huru kufuatana na dhamira yako kama ni kweli UNADHAMIRA YA KWELI.
4/
mods,wauache uzi huu uwe ni mahsusi juu ya utoaji fununu wa madudu kama kweli umedhamiria kwa jinsi ULIVYOKUWA UKIJIAPIZA HADHARANI.
5/
Watanzania wawe huru kufichua RUSHWA,UZEMBE,UFISADI,WIZI,HONGO ZA OVYO,RUSHWA ZA NGONO,NA YOOTE YASIYOPENDEZA POPOTE PALE NDANI YA TANZANIA.
NAWAKILISHA
******************
 
Mkuu chikub kupenda sifa si shida kama wafanya kazi vizuri. Hata Magufuli ni mpenda sifa, na sasa kapewa dhamana ya Urais.
Lakini Magufuli ana resources kubwa sana za kujua watu, ambao bahati nzuri wengi wao kafanya nao kazi sehemu mbalimbali. Sasa kila mtu anajifanya mwenye hekima wa kutoa ushauri.
Magufuli ameshachaguliwa kuwa Rais, mengine kama ya uteuzi tumwache afanye mwenyewe sawasawa na vyombo husika vinavyomshauri. Hatafuti Malaika, anatafutwa mchapakazi. Tutoe ushauri kwa policies huko... Sio uteuzi. Tutapoteza muda.
tumuachie mwenyewe nani? sisi pia ni wadau kwenye nchi hii tusiache kutoa maoni yetu kwa tuliyemkabidhi nchi yetu kutuongoza. Sisi tunashauri tu na yeye anayo hiari kamili kwa mujibu wa katiba yetu kuacha au kuchukua ushauri huo, lakini afanye hivyo akijua kwamba 2020 kuna uchaguzi tena.
 
Unauhakika au unaishi kwa kukalili? 2005 sio 2015, kuna mabadiriko, yeye anajua anachokifanya,

nakachaguaa yeye??? yeye hana ubavu wa juchagua wanaochaguaa akina kikwete na mkapa. hakuna lolote ccm ni ilele. nothing new.
 
Waandishi wa habari mithili ya kubenea ...!!

Hawa ndio sumu ya maendeleo ya Taifa.
 
Kuanzishwe na hotline special kwa ajili ya wanaoomba on spot rushwa kama traffics, nurses doctors n.k. watu wawe na uwezo wa kutuma photographic evedence
 
Ujumbe wako mzuri lakini bado asilimua 75% akili yako ni siasa za maji taka, ukiwa na ujumbe unaotaka wasomi tuchangie basis siasa zako acha weka hoja,tutakuelewa,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom