Pale pamesheheni wasomi. Kuanzia viongozi wa Chuo,wafanyakazi wa Chuo na wanafunzi. Wote ni wasomi. Kuyatumbua majipu ya UDSM kutawavua nguo wasomi wetu. Pale kuna magari mawilimawili kwa viongozi,Safari nononono na posho nenenene. Yapo magari ya viongozi wa pale yanahudumia nyumbani lakini yanahudumia na Chuo.
Wapo Watumishi wanaolipwa wakiwa hawako kazini. Na hata wale hewa wapo. Viongozi pale hulipiwa Safari na sherehe binafsi. Hata ukarabati wa makazi yao au ya watoto wao,ya pale chuoni na kwingineko,hug anyway kwa haraka na kulipiwa haraka. Jipu la UD lipo kisomi zaidi. Likitumbiliwa,litadhalilisha elimu yetu na wasomi wetu.Rais usiende UDSM. Nakuomba sana. Wahifadhi kwanza wasomi labda watajirekebisha!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam