Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Wakuu wa Wilaya hawana Kazi, wafutwe! Hawamo hata ktk Katiba! Huapishwa na Wakuu wa Mikoa na siyo Rais! Kazi ya kusimamia Maendeleo ni ya Wakurugenzi wa Halmashauri! Ma- DC, eti ni Wenyeviti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya! Waachiwe Polisi kazi hiyo, na kuwajibika kwa IGP! Ma-RC, badala ya kuhudhuria Sherehe tu, wasimamie Wilaya zao zote, wao wenyewe, wakiwa wawakilishi wa Rais! Itapunguza sana Gharama za Serikali!
 
na bado gharama za chuo zipandishwe tuu,si huwa hamsikii na kuelewa,wahenga walisema majuto ni mjukuu na kufka 2020 muimbe mbele kwa mbele tuu,komen japo na mm n mwanachuo
 
Hakuna MTU ambaye haombi ushauri , na kiongozi bora lazima usikilize ushauri ongeza na zako Fanya maamuzi

Mkuu ansvin usiwe na haraka kwa kusoma title za post tu. ungesoma post yote ungeona sijasema asiwe na washauri. Angalia hapa chini

 
Wasomi huwa mnajifanya hamkiungi chama cha mapinduzi kwa kujifanya kimbelembele na ukawa mfate boom ukawa sasa na boom hampati tukiwahurumia sana tutawapa 12000 wengne tu au tusiwape kabisa hatuna pesa za kuchezea kuwapa wasiotuunga
 
Serikali inatoza kodi watu wake, kazi ya kodi hizo ni nini? Serikali iweke miundombinu kama maji, umeme, barabara, elimu, afya, na usalama ili kutoa mazingira bora kwa wananchi kuwekeza akili, nguvu na mitaji yao kwa urahisi.
 
Rais Magufuli aunde Wizara ya Habari na Mawasiliano! TCRA iwe chini ya Wizara ya Habari, badala ya sasa Habari kusimamiwa na Wizara 2 tofauti - Habari (Magazeti n.k.) na ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano (TV, Radio, Mitandao)! Tozo za Simu, Leseni za TV/Radio, zingeimarisha Sekta ya Habari, ambayo siku zote haina kitu! Kuna mkanganyiko, TBC, inasimamiwa na Wizara ya Habari, Jengo lake Mikocheni, lililoanza Miaka ya 1990 (zaidi ya Miaka 20 iliyopita!), halijaisha, wanaishi popo! Wizara ya Habari, inapanga! TCRA, wanachezea pesa, ndiyo maana wana Jengo kubwa, Ubungo!
 
Ushauri wako mzuri ila mwongezee kukumbuka ahadi zake kwetu. Asipozitenda ajue kuwa 2020 zitakuwa fimbo ya kumtandikia.
Pamoja na uzoefu wetu wa "goli la mkono" 2020 halitapita. Wtz wamesha amka na sasa hawatakubali tena kampeni za kitoto za kuwadhalilisha watu. Wanataka uwaambie ulifanya nini tu katika kipindi chako. Kama huna uwezo wa kuwaonesha a realy BRN kaa kando wala fomu ya urais usichukue.
 
Si hao hao? Wataacha kuombana ushauri jinsi ya kuendeleza umaskini wetu?
 
kutegemea ushauri wa jk na mkapa lazima aliwe tu. ameingizwa mkenge kuteua masaju kuwa AG...
 
Kama ameweza kufaulu mtihani mkuu ambao umemfikisha hapo alipo hivi sasa.

Basi hiyo mingine haiwezi kuwa mitihani hata siku moja, labda twaweza iita ni majaribio
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…