Wenye uelewa zaidi hapa watatusaidia,uchunguzi unaofanyika kuhusu tuhuma za upotevu wa makontena si wa mchezo mchezo kama wengine wanavyodai pesa iliyopotea ni kubwa mno.
MOJA; sasa basi kwa kuanzia nashauri vyombo vya uchunguzi nchini vianzie shipping line TPA wao ndio wasambaji wa kontena hizo kwenye bandari kavu na wao wanajua kuwa kila icd kwa mwezi wamepeleka kontena ngapi ila walikua hawajui tu zile walizopeleka kila icd zimetoka ngapi na ngapi zimebaki (walikua hawafanyi stock taking).Nikiwa hapo hapo TPA, je bandari wanajua baada ya kutawanya kontena hizo icdni wao wenye jukumu ya kuzibeba na kuzifikisha icd husika ila Je haya magari yaliohusika kubeba kontena hizi yalikua chini ya uangalizi wa nani kuhakikisha kontena linafika sehemu husika,mbali na hapo kampuni za ulinzi Ticts na Tpa zinarekodi ya kontena zinazotoka,gari iliyobeba,vibali,mpka jina la dereva mfike hapo kurahisisha upatikanaji wa TAARIFA.
PILI; kama magari haya yalikuwa yanasamabaza kontena hizi bila kuwa na uangalizi basi TpA nao wanakesi ya kujibu,haiwezekani mzigo utoke bandrini haujalipiwa kodi hata shilingi utoke kwenda sehemu nyingine bila ya kuwa na eskoti ni ngumu mno.VYOMBO husika muombe majina ya wasindikizaji wa kontena zinazoenda bandari kavu,itajulikana hizo 349 zilikwnda wapi.
TATU; kama kontena zilifika NI lazima kwa mfumo wa utoaji mizigo wa tancis icd husika ikubali kwenye mfumo wa tancis kuwa inazipokea kontena hizo,na hapo zinakua chini ya uangalizi wa icd husika.vyombo vya uchunguzi kwa kusaidiwa na wataalamu wao wa ict wakague account zote za tancis kuanzia kwa wenye icd mpaka maafisa incharge wa tra kujua kama kontena walizipokea na kuzitoa kwa kufata utaratibu na hii iende mapaka kwenye icd za magari ambazo nazo hutoka kama transit yaani zile zinazo enda nchi jirani lakini huishia humu humu ndani na kukwepa kulipa kodi na hizi zipo nyingi ukitaka kuziona panda gari za kwenda sinza via shekilango shuka kamanyora rudi nyuma kidogo,tafuta guest ya mti mmoja utaziona hapo zimepaki nyingi hapo.
NNE; vyombo vya ulinzi vipige hodi kwenye kampuni za kuondosha mizigo,ndio wenye ruhusa ya shuguli hiyo hawa wataawasaidia kujua mchezo mzima unavyofanyika.E government pia wasaidie kwenye kuhakiki akaunti zote za wenye ruhusa ya kuachia mzigo utoke.
TANO; Idara ya ICT HASA wataalamu wa mfumo wa tancisi wakamatwe wote kwa mahojiano hasa kuhuisu kutokuepo kwa taarifa za kontena hizo,kwakua wao ndio wenye uwezo wa kufuta taarifa ya mzigo wowote kwenye mfumo wa tancis.
SITA; CAG KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI VIPITE KWENYE ICD ZIFUATAZO;
PMM ICD
TRH ICD
DICD
JEFANG ICD
AMI ICD
kwenye icd hizi kuna ujanja ulifanyika, kama vileInchaji officer wa pmm icd mwaka jana alihamishwa na kurudihswa makao,akaunti yake ya mfumo wa tancis ni muhimu ikaguliwe.
inchage wa TRH,Alihamishiwa jefang na baadae icd ya magari itwayo hesu acc yake mfumo wa tancis ichunguzwe.
incharge wa jefang ambae yupo Trh nae acc yaje ichunguzwe.
inchaji officer aliehamishwa mwanzoni ni MRS mponezya acc yake ichunguzwe na aliepo sasa.
inchaji wa AMI,ndie icd yenye uwezo wa kukagua mpaka kontena 100 kwa siku,acc yake ichunguzwe
kuchunguzwa kwa acc hizi za mfumo wa Tancis kutavipa picha vyombo hivi ni kwa jinsi gani mifumo hiyo iliyotengenezwa kusaidia serikali lakini wao wamekua wakijinufaisha wenyewe.