Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
..akienda huko ajue atalazimika kuongea KIINGEREZA.

..hivyo bora asubiri-subiri kidogo mpaka atakaporekebisha suala hilo.
 
Yaah tuvute subra...maana kuna wengine wanasubiriwa waingie kwenye 18....😎
 
Pia TANESCO hapa wilaya ya Mwanga wanabambikizia wateja bill.isiyo halali na ni wagumu kutoa machine za LUKU
 
Mzee Magufuli: Wakati wa kudai hela za escrow kutoka kwa hawa wabunge wako wawili (Chenge na Prof) ni sasa!



Chenge lazima akamatwe na kusekwa zoo kabla hajaenda jela. Huyu alikuwa anaiba kwa kiburi kwani alikuwa analindwa na Mkapa.
 
Mheshiwa kuna makampuni yanayofanya shughuli za clearing and fowarding hapa nchini yanayomilikiwa na wakereketwa wa chama chako cha ccm inabidi uyachunguze pamoja na wamiliki wao maana yamechangia kwa kiasi kikubwa sana kudumaza uchumi wa taifa letu kwa vitendo vyao vya uhaini na uhujumu.Usiwaogope maana wengine uko nao kwenye NEC na CC ya chama chako.
 
Wewe Al Shabab, kwa nini usingemshauri Mh. rais amkamate mjomba wako Kikwete kwa kuwa useless miaka 10 madarakani? Pia ikumbukwe, ni mjomba wako (JK) ndiye aliyehalalisha watu wake wasilipe kodi huku akiwachekea watanzania kwa kuongea useless points. Tunataka mjomba wako akamatwe haraka sana.
 
Naomba sana tena sana Mungu awaamshe salama Magufuli na Majaliwa ili wakatumbue jipu la Tanesco kabla hajatangaza baraza la mawaziri ni muhimu sana ili waziri ajaye asiwe muoga.
Mungu ivisha hili jipu mapema.
Amen

Kwakweli mi ntaomba nijitolee kushika pamba,mikasi na sindano wakati wa kutumbua mjipu wa tanesco!!nahisi liusaha lake litakuwa linanuka sana!
 
Mali zote nchini zisajiliwe.
Vituo vya mafuta vyote vijulikane nani mmiliki.
Majumba yote nchini yajulikane kuanzia vijijini mpaka mijini yasajiliwe ili kutambua wale wenye uroho wa kupitiliza wa kukwapua mali au kutumia madaraka vibaya kujipatia mali.
Watu wa ardhi wachunguzwe nchi nzima na mali wanazomiliki.
Watu wa uhamuaji wachunguzwe nchi nzima na mali wanazomiliki.
Watu wa TRA wachunguzwe nchi nzima na mali wanazomili.
Watu wa TANROADS wachunguzwe pia.
Watu wotu wa TANESCO.
Watumishi wote wa Mifuko ya ustawi wa jamii.
Watu wa hazina.
Wakuu wa idara kwenye vyombo vya usalama wachunguzwe usafi wao wa kusimamia idara hizo zinazopewa mafungu makubwa kwenye bajeti .
Hii itaondoa huu ujanja wa watu kupoteza malengo kwa kusema mali zote ni za mtu fulani kwa hisia tu. Mfano utasikia vituo vyote vya mafuta na malori ni ya Riz 1 au majengo yote ni ya Lowasa. Mara mashamba yote ni ya Sumaye wakati kuna mfisadi Nyangumi yamejificha huko kwenye maidara ya serikali wanachekelea kuona wanasiasa ndio wanaokimbizwa kwa tuhuma.
 
Kama ataendelea na kasi hii napendekeza katiba ifanyiwe marekebisho ili JPM atawale milele
 
Ushauri wangu kwa Mh rais, ulirudishe jeshi la kujenga taifa JKT, ili vijana wote waliomaliza shule waende huko, hata wale wasio na ajira wote waende ili wapate kupevuka kiakili ili wakiwa huko watapa fursa ya kujifunza mambo mengi kama kilimo na ufundi. hii itawasaidia pale wanapoanza kujitegemea Pia itasaidia kuuguza kwa kiasi kikubwa vijana majumbani na mitaani, uzururaji na kupeleka kuathirika na madawa ya kulevia hovyo kama ilivyo sasahivi. Asante
 
Mhe. Rais na waziri mkuu wazishukie kama tai halmashauri za jiji,manispaa,wilaya na miji ambako kuna upotevu mkubwa wa fedha za miradi ya maendeleo katika idara ya elimu,ujenzi,maji,afya,nk.
 
Watendaji Wengi Wa Serikali Wametimuliwa Kazini Na Rais Magufuli Kwa Makosa Ya Wizi, Uzembe Kazini, Ufisadi, N.K, Maoni Yangu Ninampa Rais Magufuli Asiishie Kuwafuta Kazi Bali Aende Mbele Zaidi Kwa KUWAFILISI MALI ZAO ZOTE ILI KUFIDIA HASARA WALIOISABABISHIA SERIKALI KWA KIPINDI CHOTE WALICHOKUWA WANAFISADI NCHI HII HADI WAALIM WAKOSE KULIPWA MADAI YAO. Pili, Namuomba Apite Pale Feri UTUMISHI Kuona Madai Ya Walim Yanavyoshughulikiwa Naona Ataondoka Na Mtu Pale.
 
Watendaji Wengi Wa Serikali Wametimuliwa Kazini Na Rais Magufuli Kwa Makosa Ya Wizi, Uzembe Kazini, Ufisadi, N.K, Maoni Yangu Ninampa Rais Magufuli Asiishie Kuwafuta Kazi Bali Aende Mbele Zaidi Kwa KUWAFILISI MALI ZAO ZOTE ILI KUFIDIA HASARA WALIOISABABISHIA SERIKALI KWA KIPINDI CHOTE WALICHOKUWA WANAFISADI NCHI HII HADI WAALIM WAKOSE KULIPWA MADAI YAO. Pili, Namuomba Apite Pale Feri UTUMISHI Kuona Madai Ya Walimu Yanavyoshughulikiwa Naona Ataondoka Na Mtu Pale. Tatu Uje Na Kwenye Halmashauri Huku Uone Waalimu Hadi Sasa Hawajapata Barua Zao Za Madaraja Wakisingizia Et Mitihani Ya Necta Ndo Maana Walim Hawajapandishwa Madaraja Utafikiri Mitihani Hy Imejitokeza Kwa Dharula Wakati Ilijulikanika Wazi Kabisa Kwanini Hawakuziandaa Mapema Hz Barua Za Madaraja? Hao Wote Mh Rais Timua Kazi Ni Wazembe Kazi Yao Ni Kuning'iniza Tai Na Kufuga Vitambi Tu, TIMUA KAZI HAO WAKALIME MALIMAO
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom