Kuiongoza Tanzania ni rahisi kama kumsukuma mlevi, watanzania ni watu wa ajabu sana, watu wamekaa vyuoni lakini walichofaidi ni kutoka na makalatasi tu na kakingereza ka uongo na ukweli lakini vichwani hamna kitu, tanzania umeme unakatika mwezi mzima ukiwaka wiki moja wanachangilia na kumpongeza meneja huku wakilipa bil hata ile umeme ulikuwa hauwaki, hiyo unaikuta tanzania tu, watu wanachangishwa michango ya kujenga shule, wanafyatua tofali wenyewe, lakini ileta mabati tu wanashangilia na kusema selikali inawajali hiyo unaikuta tanzania tu, watanzania hawajui haki zao, watanzania tumeitwa majina mengi ya aibu na marais wa mataifa mbalimbali, sasa hivi magufuli kafanya katukio kidogo tu, tumesahau shida zote mpaka watu wanamkufulu Mungu wakimwita masihi, magufuli kazi kwako lakini mimi bado nalia na tanzania yangu.