Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kuiongoza Tanzania ni rahisi kama kumsukuma mlevi, watanzania ni watu wa ajabu sana, watu wamekaa vyuoni lakini walichofaidi ni kutoka na makalatasi tu na kakingereza ka uongo na ukweli lakini vichwani hamna kitu, tanzania umeme unakatika mwezi mzima ukiwaka wiki moja wanachangilia na kumpongeza meneja huku wakilipa bil hata ile umeme ulikuwa hauwaki, hiyo unaikuta tanzania tu, watu wanachangishwa michango ya kujenga shule, wanafyatua tofali wenyewe, lakini ileta mabati tu wanashangilia na kusema selikali inawajali hiyo unaikuta tanzania tu, watanzania hawajui haki zao, watanzania tumeitwa majina mengi ya aibu na marais wa mataifa mbalimbali, sasa hivi magufuli kafanya katukio kidogo tu, tumesahau shida zote mpaka watu wanamkufulu Mungu wakimwita masihi, magufuli kazi kwako lakini mimi bado nalia na tanzania yangu.
1001 likes!!

Shida na usumbufu upo palepale... sema tunashangilia ahweni hewa tu !!

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Hii itaondoa mazoea mazoea..kujuana juana ujuaji juaji na taka taka zote. Pia hawatamheshimu rais kwa sababu wamemzoea. Tinga tinga lije na sura mpya zenye sifa ya kazi. Asijaze warembo mle.
 
Jana na leo vyombo vya habari vimeelezea Mauaji ya kutisha ya familia ya watu wanne yaliyotokea huko Geita yakiaminiwa ni Imani za kishirikiana. Huko ndio nyumbani kwao na Rais wetu Ndugu John Magufuli.
Mauaji ya aina hiyo sio habari ngeni kwa maeneo hayo, ni habari ya kawaida sana na ndio maana inachukuliwa kwa uzito mdogo na vyombo vya habari tofauti na kama mauaji hayo yangetokea Dar es Salaam, Arusha, Mtwara au kwingineko.
Ni jambo la aibu kufikia mahali mauaji ya watu wanne wa familia moja tena ya kikatili kwa kukatwa mapanga kuwa jambo la kawaida. Hilo jambo halikubaliki hata kidogo.
Kwa vile kwa sasa kila jambo kubwa tumejenga tabia ya kumwambia mkuu wa nchi achukue hatua, basi na hili tunamwambia alitafutie ufumbuzi tena kwa vile LINATOKEA MKOA ATOKAKO. Ni aibu kwa Rais kukimbizana na makontainer ya bandarini na kufumbia macho Raia wakikatwa mapanga na kufa na yeye bila kukasirika na kuamuru kama anavyo amuru huko kwingine.
Au raia wa Geita hawana thamani nchi hii isipokuwa huyo mmoja tuu aliyepewa dhamana? Waoneeni huruma kina mama na vikongwe wanaolaani kuwa kwa nini walizaliwa mkoa wa Geita.
Mzee Tingatinga chukua hatua haraka okoa maisha ya watu maana hakuna kiongozi anayejali huko Geita katika hili.
 
wakuu kulingana na kasi ya ajabu ya utendaji kazi ya rais wetu kipenzi JPM yaani ni spidi 180 kwenye kona shaaaaaaah. kama rais akiendelea na spidi hii basi ndani ya miaka 2 kuanzia sasa tutegemee mabadiliko makubwa yafuatayo. KUPANDA KWA THAMANI YA SHILINGI YETU, KUSHUKA KWA GHARAMA ZA MAISHA, KUKUA KWA UCHUMI WETU, KUONGEZEKA KWA PATO LA TAIFA, KUPOROMOKA KWA TABAKA LA MABEPARI WANYONYA UCHUMI,KUKUA KWA ELIMU, TUTASHUHUDIA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA,KUFUTIKA KWA VITAMBI KWA WATUMISHI WA UMMA,KUPANDA KWA THAMANI YA CHEO CHA URAIS,IKULU ITAANZA KUHESHIMIKA KAMA ENZI ZA MWALIMU, kwa kifupi rais magufuri amelenga kutufikisha katika nchi ya ahadi ya ASALI NA MAZIWA,
 
Ameanza kwa kufanya mambo yenye uthubutu uliowashinda watangulizi wake...

Tulisema kwa hali nchi ilipokuwa imefikia ilihitaji mtu mwenye maamuzi magumu na ya papo kwa hapo na asiyeogopa...Magufuli anafanya kitu kinachowapendeza wapinzani wanammwagia sifa , japo hali ya chama chake hali ni tofauti kuna kigugumizi kikubwa kwenye kumsifia mtu wao.

Pamoja na utendaji huu usiozoeleka machoni pa wengi na madudu anayoyaibua akishirikiana na Majaliwa lakini kuna mahali wawe makini na maamuzi yao wasije kuangukia mitego watakayowekewa lakini pia kukurupuka kwa namna fulani ili baadae watu wasije wakaenda mahakamani wakashinda kesi na kudai fidia za mabilioni..nitatoa mifano...

1. Ishu ya kupiga marufuku maduka ya dawa karibu na hospital za serikali imeenda vizuri kwa kutowafukuza wamiliki bali kuleta duka la dawa za serikali ambapo dawa zitauzwa kwa bei ya chini

2. Ishu ya kuvunja majengo ya gharama ifanyike kwa umakini mkubwa kuepusha fidia za mbeleni, leo kuna habari kuwa kuna hotel kubwa mpya morogoro imeamriwa kuvunjwa ndani ya siku tatu....

3. Maamuzi ya nyuma Magufuli akiwa Waziri yameliingiza taifa kwenye hasara ya kulipa mabilioni hasa kwenye kashfa ile ya 'samaki wa Magufuli'.

Kwahiyo pamoja na moto huu mzuri lakini mifano ya nyuma iwe fundisho na angalizo
 
Hoja yako ya kizee sana. Imeishia kutoa mfano hapo number 3 tu badala ya hoja na maelezo ya kubeba hoja yako. Taja maamuzi mangapi na yapi yaliyoliigiza taifa hasara?
 
Huu ni mwanzo tu mkuu.
Majipu zaidi kutumbuliwa.

Ndio maana nimeona ana mawazo mgando. Amezoea mitizamo fulani ambayo hana nafasi ya kubadilika.

Hao ambao hawakutumia staili kama ya Magufuli hawajaliigizia taifa hasara?
 
Hoja yako ya kizee sana. Imeishia kutoa mfano hapo number 3 tu badala ya hoja na maelezo ya kubeba hoja yako. Taja maamuzi mangapi na yapi yaliyoliigiza taifa hasara?

Tupe na wewe maoni yako basi mkuu maana uko kama na hasira vile...ni mtazamo wa mtanzania mwenzetu na hiyo katoa kama mifaano tu. Na kabaki kumpongeza kiongozi wetu.je una hoja ipi?
 
kuna uwezekano huko nyuma hizo kesi ambazo serikali ilikuwa inashindwa zilikuwa influenced na mikono mirefu ya waliokuwa wakishitakiana na serikali!!kwa sasa tutazimlika mahakama zetu na hukumu zao!
 
Hoja yako ya kizee sana. Imeishia kutoa mfano hapo number 3 tu badala ya hoja na maelezo ya kubeba hoja yako. Taja maamuzi mangapi na yapi yaliyoliigiza taifa hasara?

Ndio maana nimeona ana mawazo mgando. Amezoea mitizamo fulani ambayo hana nafasi ya kubadilika.

Hao ambao hawakutumia staili kama ya Magufuli hawajaliigizia taifa hasara?

Tulia basi uandike kinachoeleweka usirukeruke kama popcorn kikaangoni
 
Wana JF,

Rais wetu Dr. JPM mtu wa vipimo na viwango anaendelea kuwakonga nyoyo aliowahaidi kumwamini kuibadilisha nchi hii kutoka mzimu wa ufisadi kuwa nchi ya mfano, tiyari juhudi zake za operation OKOa pesa imetamaruki, njia mbili za kumsaidia kuokoa uchumi ni kubadilisha pesa za madafu haraka sana, hali hii itawafanya wafanyabiashara haramu waliokuwa wanaweka pesa zao kwenye mashimo na safe watakimbia kununulia vitu kama mashamba, nyumba na vitu vya thamani, watakaoshindwa kubadilisha basi ziwafie kwani kukaa nazo nyumbani hazina faida kwa uchumi wa nchi, watu hao watakimbia kuzibadilisha katika mfumo wa dola, hivyo dola zitakauka, ni vizuri kuwahi kufunga maduka yote yanayouza fedha za kigeni ili kuziba mianya ya kutorosha pesa, pesa zote zielekezwe kwenye mabenki ya serikali tu,

Jambo la pili, kwa kuwa pesa zetu zimetengenezwa kwa kiwango hafifu sana fedha hizi ziteketezwe utafutwe muundo mwingine wa fedha zetu ziongezewe ulinzi kwa kuweka halama zisizoweza kuigwa, hivyo atakuwa amewakomesha wenye mitambo ya kutakatisha fedha.
 
Aisee kumbe nchi wazalendo wapo wengi sana ila walikuwa hawajapata nafasi .!!! tena zoezi la kubadilisha fedha lifanyike kimya kimya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom