Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hongera Rais wetu kuzungumza na wafanyabiashara wenyeji na wamekupa yao ya moyoni na wewe umewapa yako ya moyoni. sasa waite na wale wa kigeni akina Barclays Stanbic Symbion TBL CRJE nao wakupe yao ya moyoni,hii itakupa picha halisi ya nini kilichoko mbele yako.

Ukisimamia bandari vizuri kila mtu akalipa kodi na ukasimamia export vizuri hakiyamungu ndani ya miaka miwili tutakuwa mbali sana.
 
Mhe Waziri Mkuu kuna sehemu nyingi za nchi hii ni Majipu kwa mfano Idara ya kazi kupendelea wawekezaji pindi kunapo kua na mgogoro baina ya muwekezaji Na mwajiliwa hii unamaanisha matajiri wanyanyase watumishi wao kwa kua tu kuna tatizo la ajira,Tumbua jipu hilo kwa kuwa amuru wazingatie sheria ya kazi nasio rushwa!Watu huangalia nani ana nini ndiyo anapewa haki hatakama sio haki unyanyasaji umezidi mpaka raia kuichukia serikali hili ni jipu
 
Ndugu zangu

Na mimi nianze kwa kumshukuru sana mwenyezi Mungu kwa mengi sana na yote. Mojawapo ni kwa kunipa pumzi ya kushuudia haya. Utendaji wa raisi wetu Ngugu John Magufuli na timu yake unaleta matumaini makubwa sana ambayo nikiri bila hiyana yalikuwa yamefifia sana kama sio karibu kutoweka.Namuomba kwa dhati kabisa Mwenyezi Mungu amjalie yeye na timu yake moyo huo huo na binafsi namuaihi kuwa nae bega kwa bega, mguu kwa mguu kuwatumikia watanzania na kuleta maendeleo ya kweli ya nchi yetu.

Jana nilijaliwa kusikiliza hotuba yake nzuri sana kwa wafanyabiashara wa ndani. Ni hotuba ya kipekee iliyosheheni umahiri, ukweli, uwazi, unyenyekevu na iliyotoka moyoni. Ahsante sana Ndugu raisi kwa hotuba hii.

Moja ya vitu alivyovigusia ni mwenye uwezo kujimilikisha maeneo ya jamii kwa faida yao, alitolea mfano wa eneo moja hapa Dar, japo hakulitaja lakini dalili zote zinaonyesha alikuwa anazungumzia Coco beach. Siku kadhaa hapo nyuma nilijaliwa kuuona mpango waliokuwa nao hao wenye uwezo wa kulibadili eneo hili kuwa la kisasa kwa ajili ya wachache wenye uwezo. Japo sii jambo baya katika kuinua uchumi na maendeleo lakini iliniuma sana nilipomkumbuka mama yangu moja ambaye nimekuwa nikinunua mihogo kwake tangu enzi hizo nilipokuja Dar kwa mara ya kwanza na basi la Lang'ata. Iliuma sana. Kwa kweli nilimuomba Mungu hili zoezi lisifanikiwe. Nashukuru sana Mungu sala zangu zimejibiwa tena kwa haraka sana. Ahsante Mungu.

Ushauri wangu kwa Ndugu rais na time yake ni waliboreshe hili eneo kwa kujenga viti vya zege, meza za zege na wale wafanyabiashara waliopo kwa sasa waboreshewe mazingira ya kutolea huduma, wajenge vyoo hata kama ni vya kulipia nk. Ila pawe free to all.

Ahsante Mungu, ahsante Ndugu rais Magufuli na timu yako.

Reaspect !!!
 
Malim Seif anatekeleza ilani gani kwenye serikali ya mseto Zanzibar?
ni kutoelewa kwako tu ndiyo tatizo, masuala ya Zanzibar yapo kwenye katiba yao ndugu yangu - hivi upo dunia ipi? ndiyo maana wana Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kama huelewi hata haya mambo madogo madogo basi hili ni tatizo.
 
Wazo zuri,kipimo kibovu.."anatema hotuba kama word processor " kama hiki ndio kipimo,magufur muache aendelee kuwa benchi..
 

Kwa heshima na taadhima, namwomba rais wangu John Pombe Magufuri aifufue TISS ( usalama wa Taifa!)

Natambua ni kwa namna gani hii taasisi ilivyo nyeti. ukiangalia nchi nyingine za Asia na ulaya taasisi hizi hazina mlengo wowote kisiasa na hazifungamani na taasisi nyinginezo, hufanya kazi zake kwa kujitegemea misingi mikuu ikiwa ni kulinda masilahi mapana ya Taifa lao/yao.

Hapa kwetu ni tofauti, sio usalama wa taifa bali ni usalama wa vyama na watu binafsi.
Ukiishitaki tu selikari, una asilimia kubwa ya kuuwawa je, huo ndo usalama wa taifa!?

Ni marangapi vitu vya polisi vimevamiwa na kuporwa silaha.,

Ni mara ngapi Pembe za tembo/faru zimetoroshwa.?

Ni mara ngapi wahamiaji wa kisomali wamekamatiwa dar ,mbeya, dodoma na mikoa mingine?

Ni mara ngapi madawa ya kulevya yametoka Tanzania na kukamatiwa nje?

Je.?niendelee kuamini kuwa nchi hii ina USALAMA WA TAIFA au haina!!

Magufuli ulitaka uraisi mimi nataka uhuru wa TISS
 
Wassalam..!
Amani iwe nanyi watanzania wenzangu ambao kwa namna moja au nyingine umeguswa /unaguswa na mwanzo mzuri wa mwalimu John Pombe Joseph Magufuli (JPJM) tangu alipoapishwa novemba 05 kuwa Rais wa awamu ya 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nikiwa kama Mtanzania ambaye naathirika hasi na ubadhirifu pamoja na ufisadi, Naomba uongozi wa jukwaa letu pendwa la Jamii forums mtuwekee jukwaa maalumu kwa ajili ya uongozi wa awamu ya tano hasa utendaji wa serikali chini ya Dr. Magufuli ili iwe rahisi kwa wageni wanaotembelea jukwaa hili pendwa la JF na sisi member kupata mkusanyiko wa habari za Dr. Na utendaji kama Rais na hii itakuwa rahisi kufanya mlinganisho wa kasi atakayomaliza nayo 2020 Mungu akituweka hai na hii ambayo ameanza nayo 2015.

Nawasilisha
 
Sawa sawa kabisa, Ila Bavicha watauchafua tu.

Ila hata hao Bavicha wanakubali kimoyo moyo utendaji wa Dr. Mtumbuaji ndo maana wakati mwingine wanatafuta vimakosa vidogo vidogo kama lugha.
 
Rais wangu Magufuli wafanyakazi wa TRA wanaogelea katika utajiri haramu nchini. Ndio "wawekezaji" wakubwa nchini kwa pesa ya rushwa. Kama kodi iliyokwepwa kwa msaada wa maafisa wa TRA na rushwa iliyotolewa kwa maofisa hao kama rushwa ingekwenda katika hazina ya serikali, tungekuwa na mapato makubwa sana. Ziba mianya hii ya TRA kwanza, utaokoa robo ya kodi yote.
 
Nakuunga mkono. Mh rais, weka sanduku tukupelekee majina na mali zao uzikague tu kwa nia njema kama walivipata kihalali. Hatuko hapa kwa kuleta umbeya ila, inauma sana atii. Mtu ana gari 12, majumba lukuki, viwanja and what have yu. Tena majumba yao ni kufru wala hawaogopi chochote. Swali; wanalipwa ngapi??
 
👏👏👏👇👇

Kwanza nitoe PONGEZI KUBWAAAA.. kwa Mh. Rais Magufuli na Mh. Waziri Mkuu Majaliwa...!! Good job so far but NOT THE BEST YET... ila najua, best starts from GOOD...!!

Ebu ongezaaa speed kabisa... hasa ktk mashirika haya... na mje na mtindo huo huo wa kuwa na MAJIBU SAHIHI MKONONI YA SHIRIKA HUSIKA, kisha UNAENDA KWA KUSHTUKIZA na kujifanya hujui chochote, kumbe una data zoteee mkononi za uhakika... ila unaenda kama mjinga vile, hujui kitu... kisha UNAWASHUKIA KAMA ELNINO...!!

1: TANESCO... hapa sielezi kitu.. mnajua kila kitu... esp. IPTL saga.. and still wanakula CAPACITY CHARGES BIL 4 KILA MWEZI... hii ni tofauti na bei ya UMEME, ambayo wanalipwa Tshs. 8 bil... so hata bunge lilisema Capacity charges ZIFUTWEEEEEEEEEEEEE... Plz vamia Tanesco na IPTL... ASAP..!!

2: TTCL... vamia hapo, madudu yake utazimia bure...

3: ATCL... hapa siongei hata ww Rais unajua kupita mm, i just wanna remind you, ongeza speed jamani..😨
🙆

4: NCAA- Ngorongoro... nenda haraka haraka jamani, plz.. be fast, fanya kama TRA vile, uwe na majibu ya kiintelijensia ya uhakika, na najua mnayo, kisha mnavamia... lazima adabu na heshima ya nchi yetu irudi..!!

5: TCRA... hapa kuna issue ya MTAMBO wa kujua mapato halisi ya kila kampuni ya simu, kisha serikali ipate kodi kubwa.. ila cha ajabu huo mtambo wameanza kujua tu sms na calls tu, sbb kuna hongo hapa, ili SERIKALI ISIJUE MAKAMPUNI YA SIMU YANAPATA SH. NGAPI, KWANI ni trillions of tshs. na serikali inakosa billions hapa, sbb kuna kamchezo ili huo MTAMBO usiweze kujua mapato halisi ya makampuni ya simu, na ina uwezo huo, ila wamebakia kujua sms na calls za watu tu... na purposely wanafanya hivyo kukosesha Serikali BILLIONS of Tshs... perhaps hapa Serikali itapata fedha zaidiii na zaidiiii ya BANDARI... naapa kabisa.. we lose trillions ktk makampuni ya simu... i swear to Almighty God.. Magufuli wahiiiiiiiiiiii TCRA..!! 😨🙆👣

6: TANAPA... hahaaa.. wataka niseme, tembo wameisha.. alafu wamebaki kucheza na media tu.. vamia, tupa kuleeee, chunguza, kamata, mashtaka ASAP.. Twiga walienda kwa Ndege Mh. Rais... wahiiiii TANAPAAAAA.. Ongezaaa speed ...🚀🚀

7: TRL, TRA ushaanza nao, ila TRL kuna nyumba mali ya TRL, mwarab mmoja kachukua zoooooteeee hapo TAZARA Dar, muulizie Halima Mdee, atakupa data zote, na alitoa BUNGENI... na Nyumba hizo mali ya TRL, zimeuzwa kifisadi balaaa, ziko hapo Tazara Dar...hata ww Mh. MAGUFULI UNAZIJUA... ni nyingiiiii...ila zimeuzwa kifisadiiiiiii... plz kula nao sahani moja..!! Zirudishweeeee...!!

8: UDA.... UDAAA... UDAAAA... naona kama huoni hii kampuni.. au sbb ni ya Riz1...? Sijaona umeigusa kabisaaa... Mh. Magufuli, ya UDA huyaoni jamani.. au unataka lecture hata kwa hili....😨💨

9: TGFA, wahi hapo, wanakubeba, ila hujataka hata kujua, fedha zinaliwa hovyo hapo, wahi jamani, hakuna shirika la umma ambalo halina madudu.. wahi hapo, uwe na data ndio ufike.. ongeza speed.. ulizia mafunzo ya marubani wako huko, wanalipwa kidogo mno nasikia, muulizie Katibu Mkuu uchukuzi Mwinjaka, atakupa data zote, marubani nasikia wanakimbia kazi hapo kwa sbb ya malipo madogoooo sana.. serikali inasomesha, inashindwa kulipa hao wataalam nadra sana kuwapata, hiyo ni aibu.. walipe vizuri waruke na viongozi vema

10: TANROAD, najua umeshawanyoosha, ila keep ur eyes and ears on.... sio uondoke umekuwa Rais uwaache, hapo ndiko kwenyewe.. ukizubaa unapigwa za mbavu..

11: TAMISEMI... huko sisemi, Majaliwa anajua sanaaaa... Mabwana Halmashauri wanakula hadi basi... wanaweka vikao kila siku wanalipana maposho ya vikao kila siku, kwa wiki moja bwana Halmashauri unakuta ana VIKAO 10, na vyote anajilipa posho milioni kadhaa kwa wiki moja...huko ndiko kumuozaaa.. tenda za kujuana, kugawiana, na kuzidisha gharama zaidiiiii... Mradi wa bil 1 ukiuona utaambiwa nyumba 3 za walimu tu.. utalia.. Majaliwa akupe data..!! FUKUZA KATIBU MKUU Jumanne Sagini... naona ana haha kweli kweli... fukuzaa..!!

12: WIZARA YA ARDHI.. haaaa.. sio nacheka, nalia, Magufuli anajua hili, nitaharibu nikisema... nakumbusha tu, 😨 roho inaniuma..haaa😨😨😭😭😭😭😭🙆🙆

13: TAA, unawajua au..!! Mfuate Mkurugenzi Mkuu, Suleiman Suleiman... mbane mbavu, kuna uchafu uchafu mwingi tu... go fast, and be straight 1, 2, 3, 4... kama TPA mlivyo fanya...!!

14: TPDC... ebu just ulizia hints kidogo tu, ila Mh. Rais usije pata mshtuko wa Moyo bure... ukaanza kuumia moyo vibaya kama Muhimbili, hadi ukasema MUNGU ATAWALIPA TU, watangulizi wako.. na kusema alafu watu wanaumia hovyo MNH huku wengine wakisafiri nje kila siku...!!

OMBI MAALUM:

Mh. Rais, umeanza vizuri, ila ILE KATIBA YA WARIOBA ITAKUSAIDIA SANAA SANAAAA.... sbb ww ukiondoka na Majaliwa, watakuja majitu mengine yanaharibu, so TUNARUDI NYUMA NYUMA KABISAAA... So ili tuzidi kwenda mbele weka system ambayo hata Rais wa ajabu akija HAWEZI KUHARIBU NCHI, na utaweza hilo kwa KUWEKA KATIBA YA WARIOBA
..nchi itasimama vyema ktk misingi yake...!! Sbb ww ukiondoka, likija mla rushwa tutarudi zama za JK...

Mungu mbariki Rais Magufuli... Mungu ibariki Tanzania...

Na kwaheriiiiiiiii....

.......😨😨👋👋💃💃🚶🚶🚶🔥🔥
 
Nimesikitishwa na majibu ya kishenzi na ya kijinga ya mkurugenzi wa TRL kwa waziri mkuu, najua waziri mkuu hana uwezo wa kumfukuza huyo mkurugenzi sasa tunakuomba kwa heshima na taadhima mfukuze huyu babu, kwanza kwa kumtizama kwa macho anapaswa kuwa alishastaafu lakini ndo hivyo tena.

Tunao vijana wachapa kazi wapeleke pale, yupo sabasaba mushongi, nehemia mchechu, hebu wape wafanyekazi wajenge CV zao, hivi vibabu hamna kitu mkuu. Hata huyu dogo DC Makonda ukimpa hilo shirika halafu mwenyekiti wa bodi akawa mzee wetu Samwel Sitta haki ya Mungu hili shirika litasimama na kujiendesha kwa faida.
 
Ahhh kkaru bwana tusiwe wanafiki tuwe wakweli mm na we tukiwekwa sehem zile tutaiba tu ndio mfumo wetu tusione mm na wewe hatujapata nafasitukasema ovyoo ufumo umetuweka hivyo
 

You are completely wrong. Usiwatukane wazee maana ndio wenye experience kuliko ninyi masharobaro. Alichokosea PM ni ku intarogate yule mkurugunzi kwa kumshtukiza mbele za watu , mapolisi, mtv n.k Hata huyo Pm akiwekwa kwenye mazingira hayo angekuwa hivyo hivyo. Huo si utawala bora. Heshima na utu pia ziwepo. Kwani huyu mkurugugenzi ndiye aliyeleta mabehewa feki? Si tunamjua ni Mwakyembe.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…