Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Hakuna asiyeshangilia anachofanya Magufuli sasa hivi, hakika ameonesha madudu mengi sana yalifanyika kipindi cha utawa uliopita.
Ninaamini pale bandarini na tra kuna watu wa usalama wa taifa, na waliona makontena yakipotea bila kusema neno, au walisema kwa wakubwa wao kuhusu makontena hayo, sasa kwa nini hii idara isisafishwe na Magufuli ili kuwaondoa watu hao, hawakutekeleza wajibu wao ipasavyo, kodi nyingi ilipotea.
Wapo wanaoishi kama vigogo wa TRA wana utajiri uliopitiliza. Washughulikiwe haraka.
Kuna Jamaa tupo nae Kitaa ni usalama wa taifa,jamaa Ana mpunga hatari Ana v8 matata na anashusha ghorofa ya kufa mtu hapa kitaani,sasa sijui kwa mshahara gani wanaolipwa wa kufanya hayo mambo,nahisi wanapiga madili makubwa makubwa.
eti leo unasimama kujitapa umewafukuza kazi maofisa 7 kutokana na ubadhirifu, swali siku zote ulikua wapi hadi uone MAJIPU YANATUNGULIWA?..
Kuna unaloficha ila jipo lako linatumbuliwa tena lipo jichoni mda si mrefu bz hata wewe ni walewale, pia hakuna shirika bovu kama tanesco, wewe hadi CUSTOMER CARE unajaza WAHANDISI mbinu za mabadiliko kwenye shirika hawana wapo kidilidili tu