Nimeikuta sehemu, imenifikirisha sana.
Dear Uncle Magufuli,
Japo salamu hii hufaa kutamkwa kwa
mdomo,
lakini acha tu niseme Shikamoo
Uncle Magu.
Pole na kazi. Mimi sijambo kabisa.
Nilitaka
kukupigia simu lakini haina chaji
nimeipeleka
kwenye duka la Mtifuamchwa kuchaji,
si unajua
ndiye mtu pekee mwenye jenereta
hapa kijijini
kwetu!
Uncle najua unaielewa vyema hali
yangu lakini
kama unijuavyo mimi huwa sipendi
kukuomba
chochote labda kama ukiamua
kunitumia.
Kusema na ule ukweli maisha ni
magumu sana.
Jana nilikula mlo mmoja tu na leo
sina uhakika
wa kupata chochote cha kuweka
tumboni.
Nilikuwa na Malaria juzi nimekunywa
tu
mwarobaini sababu sina hela ya
kununua dawa.
Tuachane na hayo, kiukweli Uncle
pamoja na
hivyo roho yangu bado inasita
kukupigia simu
kwa kitendo nilichokifanya. Sijui
kama
utanielewa. Naona aibu sana kwa
kutokukuamini. Najutia
kutokukuamini. Najuta
kutokupa kura yangu.
Sikatai, ulikuwa na maneno ya
kushawishi sana
kwenye kampeni zako lakini
nilikumbuka kuwa
hayo yamewahi kusemwa sana na
waliotangulia
lakini bado maisha yetu yameendelea
kuwa
magumu. Maisha yetu ni magumu
sana Uncle.
Nilijidanganya kuwa ningekupa kura
yangu
ningekuwa namleta mtu
atakayeendelea na
uongozi wa kubebana, uongozi wa
business as
usual, unaoruhusu watu wachache
kufanya
watakalo na kula robo tatu ya keki ya
taifa.
Najilaumu kukariri. Najilaumu kutilia
shaka ahadi
zako. Kama uchaguzi ungefanyika
leo
nisingejifikiria mara mbili kukupigia
kura.
Kiukweli, wewe mwenyewe unajua
jinsi ambavyo
chama chako kilikuwa kimepoteza
uaminifu kwa
wananchi. Naamini si mimi tu
ninayejuta
kupitiwa na upepo huo wa
kutokiamini chama
chako na kudhani ni kosa kubwa
kukupa nafasi
wewe kwakuwa ulikiwakilisha. Uncle
Magu,
tangu uingie madarakani, sikosi
kuangalia taarifa
ya habari kwenye TV kwa
Mtifuamchwa
kuangalia ni kitu gani kipya
umekifanya. Unanipa
raha sana.
Yaani una siku 32 tu tangu uingie
madarakani
lakini umefanya mambo makubwa
kuliko
kawaida. Nasikia umepata umaarufu
mkubwa
barani Afrika. Nilisoma gazeti moja
wameandika
kuwa sijui kuna mtandao wa kijamii
unaitwa
Twira kwamba Afrika nzima ilikuwa
ikikujadili
kwa kasi yako. Nasikia nchi za
Kenya, Uganda,
Afrika Kusini, Malawi, Zambia na hata
Australia
wanatamani wangekuwa na kiongozi
kama
wewe. Yaani naskia raha sana kila
nisikiapo jina
lako likitajwa.
Nasikia siku hizi maofisini
wafanyakazi
wanawahi utadhani enzi zile
nilivyokuwa
nikiwahi namba asubuhi ili kuepuka
viboko vya
mwalimu wa zamu! Huku kwetu
utafanya
surprise lini? Kuna manesi kwenye
kile kituo
chetu cha afya wanachambua mchele
kazini na
kuwaacha wagonjwa wakihangaika
tu! Njoo
uwanyooshe na huku.
Kweli nimeamini kuwa mtu mmoja
anaweza
kubadili kabisa mwelekeo wa nchi.
Unapataje
ujasiri huo Uncle? Umenifurahisha
sana
ulivyofuta safari za nje. Nasikia
umeokoa
mabilioni ya fedha kutokana na safari
hizo.
Yaani kweli Uncle hawa viongozi
waanze kuja na
huku vijijini wajionee maisha
tuliyonayo, tunaishi
kwa tabu. Pale Muhimbili
ulichokifanya
unastahili sifa kwakweli.
Unafanya kazi nzuri hadi wananchi
wa nchi jirani
wanatamani ungekuwa rais wao.
Nasikia
wanataka wakukodi ili ukawanyooshe
pia. Hata
hivyo haiwezekani. Lakini viongozi
wao
watajifunza mambo mengi kutoka
kwenye
uongozi wako.
Halafu Uncle huyu Kassim Majaliwa
siku
umemtangaza kuwa waziri mkuu
nilipata
wasiwasi kama angeiweza kasi yako.
Lakini
naye ni jembe aisee. Ulimjuaje?
Yaani
mnachokifanya ni sawa na ile movie
ya The
Expendables! Wewe ni Sylvester
Stallone,
Majaliwa ni Wesley Snipes na
Ombeni Sefue ni
Dolph Lundgren, yaani ni kichapo
kwa kwenda
mbele!
Alichokifanya Majaliwa pale bandarini
kimevumbua madudu mengi. Hivi
hawa watu wa
TRA wanataka kuifilisi nchi? Kumbe
ndio maana
watoto wao wanasoma shule za nje
na kuishi
kwenye majumba ya kifahari. Hivi
hizo hela za
kodi zingepatikana si zingesaidia
kutujengea hii
zahanati yetu hapa kwetu. Uncle hivi
unaamini
kuwa hadi leo tunaenda kutibiwa
kwenye kile
kituo cha afya kilicho karibu na
mashamba ya
bibi? Kule kuna umbali wa kilomita
13.
Uncle baraza lako la mawaziri
utalitaja lini?
Nasikia wabunge wengi wanaogopa
kasi yako.
Wengi walizoea kula bata na
kupishana airport
utadhani nchi yetu ina vita.
Watauweza muziki
wako wa Hapa Kazi tu? Nina hamu ya
kulisikia
baraza lako, fanya ulitangaze sasa
Uncle.
Uncle mimi nina imani sana na wewe
kuwa
utainyoosha hii nchi. Umeichukua
ikiwa katika
hali mbaya sana. Umeikuta katika
hali ambayo
kuna baadhi ya watu wanaishi kama
miungu
watu. Kwa fedha za serikali watu
wamegeuka
kuwa mabilionea. Ona kama wale
waliokula
shilingi trilioni 1.3 za Stanbic! Hivi
hawa watu
hizi hela zote wanazipeleka wapi?
Fedha hizi
zingepelekwa vyuoni wanafunzi wote
wangepata
mikopo kwa asilimia mia. Uncle
unajua kuwa ni
shilingi bilioni 345 tu zilitengwa
katika mwaka
wa fedha uliopita (2014/2015)
kwaajili ya
mikopo ya wanafunzi 98,000? Sasa
hebu jiulize
wanafunzi wangapi wangepata
mikopo!
Kama fedha zinazoliwa na mafisadi
wachache
zikikombolewa, naaamini walimu,
polisi, wauguzi
na wafanyakazi wengine wa chini wa
serikali
watakuwa na mishahara mizuri. Sina
shaka na
wewe naamini mpaka mwishoni mwa
mwaka
2016 heshima itakuwa imerudi mjini.
Uncle mimi ninaamini kuwa hadi
June mwaka
huu ugonjwa utakaosumbua maofisa
wengi wa
juu utakuwa ni pressure. Wakimbize
hivyo hivyo
atakayeshindwa kasi yako na
kukubali maisha
ya kupata kipato halali apishe
wengine.
Uncle Magu, walinzi wako
wamejipanga vizuri
kukuhakikisha usalama wako? Nina
wasiwasi
katika safari yako utatengeneza
maadui wengi
na wengine ambao wana nguvu
kubwa kifedha.
Najua kasi yako itawakosesha ulaji
mapapa
wengi na hawatakuwa na furaha na
wewe
kwahiyo naomba uimarishe kidogo
ulinzi wako.
Wananchi wa kawaida wanakuombea
sana
ufanye kazi yako bila kuchoka..
Tunakuombea
uwe na busara zaidi ili wale
wanakuombea
uteleze katika maamuzi yako wabaki
na aibu
zao. Endelea kuwashangaza kila
kukicha.
Uncle nisikuchoshe kwa barua ndefu.
Naamini
umenisamehe kwa kukusaliti.
Naomba tu
ukipata nafasi unikumbuke hata
kaelfu 20
katanisaidia kidogo. Mungu akubariki
Uncle
Magu.
Ndimi mpwa wako, Shidondofilo
.
Nimeitoa hukoooooooooo...