Katika wabunge wa CCM wachache waliokua wakifanya kazi zao kwa weledi wa hali ya juu basi ni Khamis Kagasheki, alikuwa ana uchungu sana na maliasili hasa majangili waliokuwa wanahatarisha usalama wa wanyama pori hasa tembo, alisimama kidete hadi kuforce operesheni tokomeza kuanza ni bahati mbaya watekelezaj vyombo vya ulinzi ndio vilivyoharibu kwa kukosa weledi wa walichotakiwa kukifanya na Kagasheki kama kanuni ya collective responsibility akajiuzulu huku wengi tukijua kosa halikuwa lake per se.
Nadhani ni muda muafaka kwa serikali iliyodhamiria kufanya kazi ya Magufuli kurudisha hili jembe mahal husika, yule bishoo Nyalandu hana lolote ndio walewale wana conflict of interest na sekta ya utalii kinyume na kanuni za utumishi wa umma.