Wana JF.
Nadhani sisi wote ni watumiaji wa hudumu za simu kutoka kwa haya makampuni Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel na mingineo.
Wananchi tumekuwa kama watumwa wa haya makampuni ya siku tunalazimishwa kila siku kujiunga usipojiunga uwezi kupiga simu gharama zinakuwa kubwa.
Kwa siku haya makampuni yanakusanya pesa nyingi sana bila hata kulipa kodi watu 500,000 kila kampuni wakijiunga kwa 1000 kampuni inakusanya 500,000,000 hii pesa wanakusanya bila kulipa kodi kila siku.
Bado wanatuuzia vocha na MB kwa bei kubwa Mh Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa, angalieni sana saula ili wananchi tunatapeliwa haya makampuni yamekuwa kama makampuni ya upatu siyo ya kutoa huduma.
Kwa nini wananchi walazimishwe kujiunga kila siku bila makubaliano, achilia mbali gharama za makato ya huduma zao za M-PESA na TIGO-PESA makato yanatisha.