Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
mtajuta kskz hakuna waziri safari hii

Tujute kwa kipi sasa?? Akiwepo waziri itasaidia nin? Maghembe si alikuwa waziri so sisi wakaskazini tumefaidi nin na uwaziri wake?? Sisi kuipiga ccm chini tunajua sababu na hatutaki upuuzi wa kusema eti tuache majizi ili waje wawe mawaziri...Wee chagua ccm huko kwenu af wawe mawaziri uvimbe misifa ya kijinga.Upuuzi huo sie hatuna.
 
Katika viongozr wa awamu iliyopita nilifurahishwa sana na utendaji wa naibu wazi wa tamisemi ndugu agrey mwanri.kwakweli ni mtendaji mahiri ila nimeshangaa kwanini amekosa ubunge kule kwao.ina maana hawaoni uwajibikaji wake?naomba muheshimiwa rais umwone huyu ndugu kwani atakufaa kwenye kikosi chako hasa mambo ya ndani.

Kwenye UCHAGUZI wananchi hawakuona ni mtendaji Mahili? Wakamchagua
 
Wana JF.

Nadhani sisi wote ni watumiaji wa hudumu za simu kutoka kwa haya makampuni Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel na mingineo.

Wananchi tumekuwa kama watumwa wa haya makampuni ya siku tunalazimishwa kila siku kujiunga usipojiunga uwezi kupiga simu gharama zinakuwa kubwa.

Kwa siku haya makampuni yanakusanya pesa nyingi sana bila hata kulipa kodi watu 500,000 kila kampuni wakijiunga kwa 1000 kampuni inakusanya 500,000,000 hii pesa wanakusanya bila kulipa kodi kila siku.

Bado wanatuuzia vocha na MB kwa bei kubwa Mh Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa, angalieni sana saula ili wananchi tunatapeliwa haya makampuni yamekuwa kama makampuni ya upatu siyo ya kutoa huduma.

Kwa nini wananchi walazimishwe kujiunga kila siku bila makubaliano, achilia mbali gharama za makato ya huduma zao za M-PESA na TIGO-PESA makato yanatisha.
 
Katika viongozi wa awamu iliyopita nilifurahishwa sana na utendaji wa naibu wazi wa tamisemi ndugu Agrey Mwanri kwakweli ni mtendaji mahiri ila nimeshangaa kwanini amekosa ubunge kule kwao ina maana hawaoni uwajibikaji wake?

Naomba muheshimiwa rais umwone huyu ndugu kwani atakufaa kwenye kikosi chako hasa mambo ya ndani.

unaweza pia ukampa uwaziri wa nyumbani kwako hapo.
 
Huyu si ndio alikimbia kazi mwenyewe kuogopa kukamatwa na alitaka kuiba ubunge akakimbilia kupanda ndege aondoke huko kwao huku ameacha maagizo eti wamtangaze yeye.

Kuna jamaa alidafiri kwenda huko kikazi ndio akapata muda wa kuzurura jioni ya matokeo akakuta Kagasheki kawai kupanda ndege ya mwisho huku watu wa serikali wakihaha kutangaza wakidai wameombwa wamtamke yeye mshindi hata kama kwa namba kashindwa.

Akatupa ubuyu kuwa alishangaa ma kasheshe hayo ya ubunge yeye anafanya kazi na NGO, sote twaishi mkoa mmoja hapa TZ.

Ndio walibanwa wakamtaja mshindi aliyeshinda kwa kura nyingi.
 
Katika viongozi wa awamu iliyopita nilifurahishwa sana na utendaji wa naibu wazi wa tamisemi ndugu Agrey Mwanri kwakweli ni mtendaji mahiri ila nimeshangaa kwanini amekosa ubunge kule kwao ina maana hawaoni uwajibikaji wake?

Naomba muheshimiwa rais umwone huyu ndugu kwani atakufaa kwenye kikosi chako hasa mambo ya ndani.

Haya basi ni waziri
 
Kama Serikali ina nia ya dhati kabisa ya kuondoa umasikini kwa wananchi wake basi ifanye maamuzi ya kiasa ya wazi kabisa kwa kukopa kwenye mabenki ya nje na taasisi za kimataifa ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa riba inayotozwa na mabenki hapa nchini, mabenki ya hapa nchini yamekuwa hayasikilizi maoni ya wadau wao wanaoshauri kupunguza viwango vyao vya riba kwa sababu wanafahamu Serikali itakopa kwao na watanunua government bonds na kadhalika. Kwa kuwa Serikali inaweza kukopa nje ya nchi basi ifanye hivyo ili haya mabenki ya hapa nchini yaanze kushindana kutafuta wakopaji miongoni mwa wananchi na kwa kufanya hivyo riba zitapungua na wananchi watapata ahueni ya maisha.

Cc. Governor wa BOT - tafadhali Mshauri rais
 
Mkuu, umesikika..
JPM anaangalia namna ya kuyatumbua hayo majipu..
Tuzidi kumuombea Rais wetu.
 
Ushauri mzuri ila kwa sasa ni vizuri tukamshauri Rais kuweka mikakati ya kujitegemea kuliko kuendesha serikali kwa kukopa kopa...ingawa hata mataifa makubwa km UK na USA yanakopa kwny taasisi za kifedha!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom