Habari za huko kwenu wadau,
Katika kutafakari saaana matatizo ya hii nchi kuanzia kwenye huduma za maji mjini na vijijini zilivyo duni, miundombinu ya maji taka ilivvyo duni hapa Dar hadi mvua ikinyesha kwa siku moja tu ni bonge la dhahama.
Madarasa hayatoshi na madawati pia hakuna ya kutosha watoto wanakaa chini, shule nyingine hazina hata vyoo,shale hazina maabara za kisasa ili kuendana na mabadiliko yanayotokea katika sayansi na teknolojia, umeme vijijini ni shidaa hata huku mjini ni wa kuunga unga, zahanati ni za kuongeza pia vijijini na matatizo mengine lukuki.
Sasa serikali imeshindwa kutatua mizigo yoote hii inakuja kujitwisha mzigo mwingine wa elimu bure? Mimi naona kwa wale wazazi ambao ni masikini wasioweza kulipia watoto wao karo wangeandikishwa kisha watoto wao wakawekwa kwenye program maaalum ya kulipiwa na serikali.
Wale wanaoweza kulipia wakaendelea kulipia kama kawaida, na michango ya shule isingefutwa bali wangetafuta namna ya kuidhibiti, miradi wanayodai imefanywa na hiyo michango iangaliwe na kama kuna uongo hatua kali zinachukuliwa kwa mkuu wa shule ikiwamo kuachishwa kazi na faini kubwa
Michango ya shule iendelee kuwepo kwa kua serikali haiwezi ikafanya kila kitu kwa uchumi huu wa kutegemea misaada na mapato mengi hayajakusanywa bado, vitu kama ujenzi wa choo na ukarabati wa majengo kutegemea serikali kuu itakua ni kuchelewesaha vitu hivyo kufanyika tungeweka mambo yetu yanyooke kwanza, mapato yetu tuwe tunaweza kuyakusanya effectively, miundombinu tuwe tumeiboresha vizuri, then ndio tuanze kutoa elimu bure kwa wote.