Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Katika majipu sugu jipu lililopo katika Halmashauri { A.k.a wazee wa madokezo} zote Tanzania ni jipu sugu na lipo sehemu mbaya sana.
Asilimia 90 ya muda utumikao Halmashauri unatumika kwa vikao visivyo kua na tija. Vikao hivyo huenda na kulipana posho.

Unaweza fika Halmashauri kuanzia juma tatu mpaka Ijumaa ni vikao tu. Hivi huwa wanajadili nini na kuacha wananchi wakiwa wamepangana kwenye makorido.

Kwa sababu inaonekana wanapenda sana vikao kuliko kuhudumia wananchi Nashauri vikao hivyo viwe vinafanyika Jumamosi na Jumapili ili siku za kazi wahudumie wananchi.
 
UDOM kuna jamaa alikuwa analeta kiburi kwa sababu ya JK. Huyu jamaa alichochoea uasama baina ya Staff na wanachuo kwa mlengo wa udini. Employment na Vyeo.

Magufuli tungua hili JIPU, liko kwenye koromeo. Tungua hadi Bernard Membe akimbie nchi.
 
Nimekuwa nikijiuliza ilikuwaje aliyekuwa Mkurugenzi wa bandari Madeni Kipande kuondolewa ukurugenzi kisha kuteuliwa kuwa katibu tawala mkoa.

Baada ya kuwajibishwa juzi ndipo nimebaini kuwa kumbe serikali iliyopita ilikuwa ikikumbatia wezi wa mali ya umma.

Kilichotusaidia ni katiba kutaja ukomo wa vipindi viwili vya urais vinginevyo nchi ingefilisiwa kabisa.

Nakushauri mhe.Magufuli usipokee ushauri kutoka kwa walioshindwa kuongoza taifa. Iwapo utaona haja ya kushauriwa nenda kwa Paulo Kagame ambaye serikali yake haina mchezo.

Hivi kweli serikali iliyopita haikuona mradi wa vitambulisho vya taifa kuwa ni jipu.
 
Serikali iliyo pita ilikuwa ya vunja mifupa kama meno ipo"*kula nchi* huo ndio uliokuwa mtazamo wake, watendaji yafanye mazuri au mabaya who cares!!! Isipokuwa wezi wa kuku na akina babu seya waliangaliwa sana kwa kuwa walijaribu kulia sahani ya mfalme. Uozo wote huu unao onekana sasa ulikuwa unaeleweka watu walishauri na ushauri wao haukusikilizwa/kusikilizwa, viongozi wanapoikia hatua hiyo matokeo yake ndio haya tunayo yaona sasa.
Siamini kama rais anahitaji kupata ushauri toka nje kwani hakuna asilolijua amekuwa waziri kwa miaka ishirini kipi kigeni kwake, la msingi kwake asimamie kwa haraka katiba mpya itoke naiboreshwe ili haya yote anayo yafanya yawe documented ili yawe kisheria. Hapa ni kazi tuu ni slogan yakuonyesha hataki upuuzi kwenye awamu yakevya uongozi.
Rais peke yake hawezi kuleta maendeleo ya nchi hii, inatupasa wananchi wote kwa pamoja tushikamane tuwe na lengo moja tuache tabua ya ubadhilifu wa maili za umma, tutii sheria na mamlaka then wale mafisadi (woteee) awe wa ccm, chadema cuf awe amestaafu utumishi wafilisiwe mali zao kwa kuwa wameliibia taifa na watupwe kolokoloni.
 
Rais wako hashauriki ni dikteta
Katika kutafuta maendeleo iwe katika nchi au hata majumbani udikiteta haukwepeki. Nchi zote ambazo zipo juu kama Rwanda Udikteta ndipo kwao (the dictatorship of the proletariats or the poor. Kindly revisit Marx)
 
Mzee wa kutumbua majipu.
Nilitegemea umrudishe Agrey Mwanry awe waziri wa kuisimamia TAMISEMI.

Hata hivyo kuna majipu huko halmashauri za miji.

Piga marufuku kabisa ujenzi wa barabara za kiwango cha changarawe kwenye miji yote. Hizi zinalipa taifa hasara kubwa na kuwanufaisha makandarasi wanaozijenga kila mwaka kwa kiwango cha kusombwa na mvua na kila msimu wa mvua.
Barabara zote za miji mikubwa na midogo ni lazima ijengwe kwa kiwango cha lami au hata mawe kama sio zege.
Tuna viwanda vingi sana vya sementi na mawe mengi sana kila kona ya nchi lakini Halmashauri zinashindwa hata kujenga standi ya matofali au mawe. Huu ni ujinga mkubwa na kukosa maono kwa wakurugenzi wetu wa halmashauri. Ubunifu ni ziro kabisa ,kila mwaka standi nyingi zinasombwa na maji na kujaa vumbi tu huku wakitoa tenda za mamilioni kumwaga vifusi vya udongo wa kulimia mahindi. Aibu kabisa.

Huko kwenye halmashauri kuna upotevu mkubwa wa fedha za umma kwa sababu ya miradi ya maendeleo isiyokamilika miaka nenda rudi.
Kila mwaka barabara ile ile inatengewa pesa na ujenzi ni ule ule wa kiwango cha udongo.
Kwa nini wasitumiale angalau mawe na sement kama sio lami tatizo likausha fedha zikapelekwa eneo lingine kujenga barabara mpaka maeneo yote yakawa ma barabara nzuri angalau serikali ikakaa hata miaka Kumi bila kukimbizana na vifusi vya barabara za udongo?

Utashangaa kuona mkoa wenye mawe mengi kama Kagera tena yaliyochongeka vizuri kama marumaru lakini standi zake zote za halmashauri za wilaya zote ni za udongo na mashimo kibao na vumbi tupu huku wakiwatoza wananchi na wamiliki wa magari pesa za kuingia standi kuchafua magari yao kwenye vumbi kubwa. Huu ni ujinga na kukosa ubunifu kama binadamu. Binadamu anapaswa kujua namna ya kutatua matatizo yanayomzunguka kutokana na rasilimali zinazomzunguka.

Unakuta Halmashauri imezungukwa na maji mengi lakini inashindwa kubuni vyanzo vyake vya kutoa huduma ya maji kwa wananchi kama miradi ya ziada.
Halmashauri inashindwa hata kuchimba kisima kirefu ndani ya mji waje kupunguza adha ya upatikanaji wa maji.
Kazi ni kukaa vikao tu kila siku visivyo na tija kwa jamii zaidi ya kugombania tenda.
Poor wakurugenzi wetu na wakuu wa wilaya na wabunge wao wasio na maono kwa taifa hili
 
Habari za huko kwenu wadau,

Katika kutafakari saaana matatizo ya hii nchi kuanzia kwenye huduma za maji mjini na vijijini zilivyo duni, miundombinu ya maji taka ilivvyo duni hapa Dar hadi mvua ikinyesha kwa siku moja tu ni bonge la dhahama.

Madarasa hayatoshi na madawati pia hakuna ya kutosha watoto wanakaa chini, shule nyingine hazina hata vyoo,shale hazina maabara za kisasa ili kuendana na mabadiliko yanayotokea katika sayansi na teknolojia, umeme vijijini ni shidaa hata huku mjini ni wa kuunga unga, zahanati ni za kuongeza pia vijijini na matatizo mengine lukuki.

Sasa serikali imeshindwa kutatua mizigo yoote hii inakuja kujitwisha mzigo mwingine wa elimu bure? Mimi naona kwa wale wazazi ambao ni masikini wasioweza kulipia watoto wao karo wangeandikishwa kisha watoto wao wakawekwa kwenye program maaalum ya kulipiwa na serikali.

Wale wanaoweza kulipia wakaendelea kulipia kama kawaida, na michango ya shule isingefutwa bali wangetafuta namna ya kuidhibiti, miradi wanayodai imefanywa na hiyo michango iangaliwe na kama kuna uongo hatua kali zinachukuliwa kwa mkuu wa shule ikiwamo kuachishwa kazi na faini kubwa

Michango ya shule iendelee kuwepo kwa kua serikali haiwezi ikafanya kila kitu kwa uchumi huu wa kutegemea misaada na mapato mengi hayajakusanywa bado, vitu kama ujenzi wa choo na ukarabati wa majengo kutegemea serikali kuu itakua ni kuchelewesaha vitu hivyo kufanyika tungeweka mambo yetu yanyooke kwanza, mapato yetu tuwe tunaweza kuyakusanya effectively, miundombinu tuwe tumeiboresha vizuri, then ndio tuanze kutoa elimu bure kwa wote.
 
ILANI YA UKAWA ni ngumu kuiga wao ndio wanazo data kama wapinzani.yeye kadakia tu atadaka na vitu visivyodakwa.

swissme
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom