Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kama watanzania tusingekuwa na ubinafsi kusingekuwa na haja ya " ukuta" wala sakafu, tatizo la ubinafasi kila kigogo anatunisha misuli dhidi ya wenzake na haangalii maslahi ya watanzania!
Kama wameanza kuandamana na Moshi safi sana.

Tunawaomba waandamane kabisa usiku na mchana ,tuwe tunaandamana kutoka moshi mjini hadi Hai kila siku , kwa sababu ndio tulichoahidi wakati wa uchaguzi
 
Kama wameanza kuandamana na Moshi safi sana.

Tunawaomba waandamane kabisa usiku na mchana ,tuwe tunaandamana kutoka moshi mjini hadi Hai kila siku , kwa sababu ndio tulichoahidi wakati wa uchaguzi
Una mawazo mfu sana wee gamboshi...
 
Kwa kuwa sasa ni mwenyekiti wa chama, kwa nini asikae na wenyeviti/ makatibu wa vyama vingine awasikilize nini wanachotaka? Kusema usijaribiwe, wewe ni tofauti, myi gani katika hii dunia asiye na majaribu au changamoto za maisha. Nchi kwenda mbele ni wajibu wa kila mTz kuipeleka mbele wakiwamo wapinzani, kaa nao ujue mikakati yao kuliko kutishana.
 
yaani tz inavyopelekwa kipindi hichi ni kama tupo kwenye giza haieleweki kila mmoja anajaribu kumtunishia mwenzie misuli sasa shida ipo kwa ngazi za juu huko ndo balaaa
 
Kwa kuwa sasa ni mwenyekiti wa chama, kwa nini asikae na wenyeviti/ makatibu wa vyama vingine awasikilize nini wanachotaka? Kusema usijaribiwe, wewe ni tofauti, myi gani katika hii dunia asiye na majaribu au changamoto za maisha. Nchi kwenda mbele ni wajibu wa kila mTz kuipeleka mbele wakiwamo wapinzani, kaa nao ujue mikakati yao kuliko kutishana.

Yaani ukae meza moja na mtu alietangaza tarehe 1 kuwa siku ya mikutano Na maandamano nchi nzima?? Labda upige unga/viroba kidogo. Dalili za mtu asiekuwa na hoja utazijua tu and according to 1st Newton's law of motion anaekuja kwa ubabe unamzibua tu kwa ubabe ili mambo yaende
 
USHAURI KWA MAGUFULI
Kwanza kabisa nakupongeza kwa hatua uliyopiga katika kututetea sisi maskini na kuweka nidhamu katika ofisi za umma.

Umeonyesha moyo wa dhati wa kupambana na rushwa na ufisadi japokuwa mengine ni ngumu kumeza kama Lugumi,Tegeta escrow,Richmond nk.

ZIARA MIKOANI
Mh. Raisi Kila ukanyagapo Mungu akulinde kwa sababu umedhamilia kwa dhati kutetea maslahi ya wanyonge na kuendelea kuwa gumzo mitaani na kutikisa mtima wa mafisadi na wezi wa kalama ambao nia yao kubwa ni kukuona ukishindwa kutekeleza ahadi zako.

Mh. Ningependa kusikia maneno matamu kama sega la asali ambayo yalinishawishi mpaka nikaweka kavema kangu kwenye jina lako siku ya kupiga kura.

Masikio ya watanzania yatazibuka zaidi wakisikia mipango endelevu juu ya uhakika wa kupata matibabu kwenye zahanati zao za kila kata ulizowaahidi,watanzania wangependa kusikia juu ya uhakika wa kupata ajira kwenye viwanda ulivyoviahidi, akina mama wanazisubili mil 50 za kila kijiji ili waweze kuboresha maisha yao kwa kunufaika na mikopo yenye riba nafuu.

KUHUSU MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA
Mh.Raisi ni ukweli usiopingika kuwa ni lazima tutenganishe wakati wa kazi na siasa,katika hilo chama chako mwenyewe kilitakiwa kuonyesha mfano kwa vyama vingine,Mfamo kama ziara zako ni ziara ya kiserikali sina la kuongea,lakini kama ziara yako ni ya chama kwa kuwashukuru wananchi kukuchagua hapo kuna kigugumizi.

Kumbuka kuwa ulichaguliwa na watanzania milioni 8 na mpinzani wako mkuu alichaguliwa na watanzania milioni 6 sasa basi kama utazunguka kuwashukuru watanzania milioni 8 waliokuchagua tambua kuwa aliyechaguliwa na watanzania millioni 6 naye ana haki ya kuwashukuru hao wachache waliomchagua kwani Maandiko yanasema "Shukuruni kwa kila jambo" maandamano na kila aina ya maneno yanayotishia kuvuruga amani ya nchi hii hayapaswi kupewa nafasi ni lazima yakemewe na kuzuiliwa kwa nguvu zote huku ukikaa chini na watu hawa kuzungumza nao pia na wao ni watanzania ambao wako chini yako.

NAOMBA KUWASILISHA.
 
Mkuu humu JF kuna watu walikuwa wanamsifia kwa kila kitu anachofanya sasa hivi wanaanzisha uzi au wanaposti maoni ya kumpinga au kumkebehi
 
Magu kaza kaza zaidi
Hao watu wasikutishe
Waponyuma ya Majizi na Mafisadi
Simamia haki na ukweli.



"Nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni’"
 
Ungeuliza kistaarabu ningekujibu naona leo umeamka vibaya acha kunukuu posti zangu maana tutagombana
Hahaha utapiga ngumi UKUTA!!!?
Kugombana!! Niogope nikishuhudia Ugoro, uongo pia unafiki!!!?

Hahaha haiwezi tokea .
 
Mheshimiwa Rais wangu, kiukweli mi naona pale unapo toa tamko fulani kuhusu serikali, viongozi wako wanafata kile ulicho sisitizia. Mfano, uliosema stand huko igunga itumike, tayari imeanza kutumika. Uliposema, watumishi hewa watolewe, kila kiongozi alitekeleza agizo hilo. Vile vile, bila kusahau la serikali kuhamia dodoma, baadhi ya wizara walikaa vikao ili wahamie dodoma hata kabla ya hiyo miaka minne uliyo sema. Sasa Mheshimiwa, naomba pia utamke kuhusu watumishi wanao tumia vyeti feki na digriii za kununua makazini, pia wamechangia kufikisha nchi ilipo kuwa imefikia.
 
Tunajua kwamba tulikosea lakin ni harakati tu tulikua tukitafuta maisha,
unapoendelea na ukaguzi wa vyeti sisi tunazidi kudhoofika wengine kidato cha nne tulikisoma mara sita yote hyo ni kutafuta maisha tu,
tunaomba tugange yajayo haya ni maisha tu, tutatunzaje familia zetu? nakuomba sana sana anza upya ulipofikia mambo ya nyuma yaache tu.
hatuna amani kabisa maisha ni magumu mtaani chonde chonde bado tunasomesha tunaomba msamaha wako,
tunakupenda sana our lovely prezdent
 
kumbe vyeti feki hapa hakuna cha msamaha wala nini tutawasaka kokote mliko, hakuna janja janja serikali hii kama vipi pisha mapema nenda kimbiji kalime waache wenye vyeti halisi walio visotea vyuoni wafanye kazi.
 
Rais Mtukufu Isombo la Sahoyo wakwa! Mtukufu ni Mungu Peke yake. Huyo Rais Unayemtaja Simjui Ila Utukufu alio nao ni Nini? Nahisi Rais Unayemtaja ni Wa Nchi ya Afrika na Marais Mengi wa Afrika wamejaa Ushetani, Ninauhakika na Unayemtaja hali kadhalika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom