Rais na Serikali yako,wananchi wako tunauliza bila kukuchukiza. Vipi kuhusu ajira ulizozisitisha bila kutisha nchi nzima kwenye sekta ya umma? Kupanda na kushuka vyeo kulisitishwa;kuingia na kutoka ajirani kulisitishwa.
Kulitangazwa kwa kushangaza miezi miwili. Miezi ya uhakiki wa uhakika wa wafanyakazi hewa na hai. Miezi miwili imekwisha. Watumishi hawajapanda vyeo,hawajapata nyongeza za mishahara wala ajira mpya kuanza. Vipi?
Wasomi walishaomba kazi. Wakaitwa kwenye usaili. Na hata wengine kuitwa kazini. Lakini,tangazo la Serikali liliwapa maumivu makali. Walilazimika kurejea walikotoka bila kutaka kwakuwa ajira zimesitishwa. Kikatiba,kuajiriwa ni haki. Kwanini ukimya huu?
Wananchi wanaomba bila kugomba majibu mujarabu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam