Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Huu ni uchochezi, maswali kama haya yatawafanya raia wema wamchukie mtukufu rais. Nani kakupa kibali cha kuuliza maswali magumu kama haya! Subiri hadi 2020 utapata majibu.
 
Hili kwakweli Rais anawaumiza watumishi wa serikali!
 
hahahaha hii serikali inakomesha raia hata ccm mtaisoma namba kuna watu wanajiita ccm.damu.wacha wakome
 
Hali aliyoikuta Rais Magufuli nchini inakera sana kwa mtu yeyote ambaye ana uchungu na watanzania wenzake. Wote tunafahamu kuwa nchi yetu ilikuwa na mambo mengi yanayochukiza kuanzia bandarini, wanyama pori, misitu, wafanyakazi na wanafunzi hewa, wakwepa ushuru, mikataba feki, misururu ya safari za nje, migogoro ya ardhi, rushwa, uwajibikaji mdogo wa watumishi, wizi wa mali za umma, madawa ya kulevya, n.k. Labda Rais Magufuli ameshindwa tu kujieleza kwa wananchi wenzake kuwaeleza kuwa taifa lao liko kwenye vita kubwa, mbaya na hatari sana kuliko hata ile vita ya Uganda dhidi ya Idd Amin. Vita ile ya Uganda adui alikuwa nje ya mipaka lakini vita hii ufisadi anayopambana nayo adui yuko ndani na pengine uvunguni mwa kitanda. Dr. Magufuli alipoamua kupambana na ufisadi, wakwepa kodi, wala rushwa, wauza meno ya tembo na madawa ya kulevya amejiamulia kujipa kazi kubwa sana na ngumu isiyoweza kulinganinwa hata kidogo na uhuru wa kuandamana, kufanya mikutano, kuandika na kutangaza. Watanzania wema tunapaswa tujikusanye nyuma yake tumpe joto, moyo, faraja na ulinzi ili kumpa ujasiri na moyo wa kuyabwekea majizi ya mali zetu.

Kwa hali ilipokuwa imefikia nakubaliana kabisa na Rais Magufuli kuvikanyaga baadhi ya vifungu vya katiba angalau kwa miaka 3 hivi ili kulikomboa taifa dhidi ya wakora. Duniani kote wakati wa vita katiba za nchi huwa zinapindishwa kwa muda ili kutafuta uchindi dhidi ya adui. Vita dhidi ya ufisadi ni vita sawa na vita nyingine.

Watanzania tusije tukadanganywa na kuamini kuwa uhuru wa mikutano ni bora kuliko vita dhidi ya wezi wa mali zetu. Uhuru wa kusema na kuandamana kwa sasa ni kilio cha wenye nacho, ni kilio cha walionyang'anywa mirija ya kufyonzea mali zetu, ni kilio cha wenye hofu na mali zao za wizi, ni kilio cha waliopoteza mali zao kwenye uchaguzi, ni kilio cha wenye hasira za kushindwa, n.k.

Kule Libya na Irak walililia uhuru wa kuandamana na kusema wakawachinja marais wao, sasa hivi wanawakumbuka Gadaffi na Saadam.

Wachina waliwaita wale wanaotaka China izingatie haki za binadamu na uhuru wa mikutano nchi nzima kuwa ni wapumbavu wasiojua ni kwa namna gani China inaweza kuhudumia robo ya watu wote duniani peke yake. Kwa China kazi ya kuwatunza (chakula, matibabu, mavazi, malazi, elimu,...) Wachina ambao idadi yao ni robo ya dunia ni muhimu sana kuliko uhuru wa kusema, kuabudu, mikutano, kuandika.

Imebainika kuwa uhuru wa maandamano hauzuii twiga kupakizwa kwenye ndege wala tembo kung'olewa meno, tulipaswa kuutumia uhuru wa kuandamaana katika awamu ya nne katika kuzuia uporaji wa maliasili zetu na ufisadi nchini uliokuwa unafanywa waziwazi mchana kweupe.

Tuwe wazalendo kwa taifa letu kwa kumshauri vema Rais Magufuli ni namna gani vyama vyetu vya siasa vitajiendesha katika kipindi hiki ambacho Rais anapohangaika na ufisadi uliokuwa unalitafuna taifa letu. Nilichogundua mimi katika vita hii ambayo Magufuli ameamua kujitwisha kichwani kwake hata CCM wenyewe wako hoi, hawajui hatima yao, hata mirija ya mabwanyenye wa CCM imezibwa nta. Hivyo tusidhani kuwa ni vyama vya upinzani tu vinavyolia bali hata CCM maslahi ya akina nanihino na watoto wao iko mavini pia kwenye vita hii.

Ni mawazo yangu tu
 
In summary:
Na wewe tuambie uhuru wa mikutano hiyo unazuiaje vita dhidi ya mafisadi na majangili.
 
Naunga mkono hoja.
Pasco
Kwa kuwa unaunga mkono hoja bila maelezo yoyote ya ufafanuzi, naomba unisaidie maelezo ni kwa vipi huo uhuru uliopingwa na mleta uzi unavyoweza kuzuia jitihada za Rais kupambana na ufisadi na ujangili. Point-kwa-point, na si yale majibu yaliyofunikwa blanketi. Pasco
 
In summary:
Na wewe tuambie uhuru wa mikutano hiyo unazuiaje vita dhidi ya mafisadi na majangili.
Inapunguza concentration na umakini kwa mpambanaji. maandamano ni dhidi yake na vita ya ufisadi ni dhidi yake pia
 
Magufuli apige marufuku wachaga kuajiriwa serikalini. Halafu wachaga matajiri wafilisiwe kabisa maana wameiibia sana serikali
 
Rais haongelei elim, afya, ajira, michezo na sanaa. Vipi kwani anahofu gani? Mbona usalama upo tu? Kuna shida ya kiusalama ndani ya nchi? Kama Rais kuna mambo muhim yakuongelea na kusimamia ila sio kila siku santuri ya usalama, ukali na ubabe. TUMECHOKA TAYARI.
 
Tired, really tired
 
Kweli,hata mimi najiuliza,hivi huyu Lowassa ni nani mpaka nchi haifanyi maendeleo bali kujihami tu??
 
Sijui ni nguvu ya mitandao ama ni kelele za wachache ila ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mambo yanalalamikiwa sana. Suala la uchumi, ajira kwa vijana, issue ya bandari, msuguano kati ya TRA na TPA, na suala la kodi zimekuwa zikijadiliwa sana, na wengine kwa jazba...

Jana Mbunge wa Igunga alisema kuna viongozi wanaogopa kumwambia Mh. Rais ukweli, ama wanamdanganya.... Hivyo, naomba Mh. Rais chukua wafuatao watakusaidia na kulisaidia Taifa kwa kusema ukweli

1. Professor Issa Shivji (UDSM)
2. Dr. Mwami (UDSM)
3. Dr. Bashiru Ally (UDSM)
4. Professor Palamagamba Kabudi (UDSM)
5. Professor Haji Semboja (UDSM)

Hawa wakija kama jopo la ushauri, kwa hakika tutaona mabadiliko ya kweli. Na sio waoga kabisa. Kwa sasa taifa limekumbwa na uoga, watumishi waoga sana, na wanahofu kiasi cha kupelekea kutokufanya maamuzi... Kila kitu wanasubiri maelekezo...
 
Ashasema kama sio ccm sahau serikali yake

Hapana. Nafkiri alikuwa anachombeza, unajua Rais wetu anapenda sana kuchombeza... Kwa manufaa ya Taifa itamlazimu achukue wanazuoni. Wanasiasa ni waoga sana hawawezi kumshauri..
 
Hao wote hawawezi kumsaidia.....
yuko Benno Ndulu.....ndie aliepaswa kumsikiliza kwa masuala yote ya uchumi ..hamsikilizi...

Ni yuko vizuri. Tatizo wanatofautiana katika mtazamo... Ndio yale yale ya Nyerere na Mtei...

Ndulu ni liberal, Rais ni mjamaa... Ingawa ni vyema kuwachangaya na hao wanazuoni...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom