Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Marais waliomtangulia walijuvunia kukua kwa democrasia je yeye anajisikiaje akiambiwa democrasia imedidimia? Je anajua kuwa hakuna maendeleo kama hakuna democrasia?
 
Nitamwambia ahadi yake aliyoitoa Nyamongo kuhusu malipo ya fidia tarehe 11/09/2016 alipokuwa anapita kuomba ridhaa ya wananchi wa Nyamongo kuwawakilisha ikulu ya magogoni,aliwambia wananchi wa Nyamongo kuwa,sitawavumilia wawekezaji wasiojali wananchi, nikiingia ikulu tu itakapofika mwezi wa pili,wananchi wote wangelikuwa wamepewa haki zao,lakini hadi Leo ni kama ndoto,mgodi unadhurumu ardhi na kuleta madhara makubwa kwa wananchi, mgodi unatiririsha maji yenye sumu kwenye makazi ya watu,mgodi sasa hausikilizi hata unayoambiwa na serikali,hayo ndo ningemkumbusha mh Rais wetu ili anapokuja TARIME mwezi huu afike na Nyamongo ajionee mwenyewe,
 

Attachments

  • a-victim-of-poisonous-chemicals-from-barrick-gold-mines-at-north-mara-in-nothern-tanzania-131.jpg
    a-victim-of-poisonous-chemicals-from-barrick-gold-mines-at-north-mara-in-nothern-tanzania-131.jpg
    141 KB · Views: 42
  • main.jpg
    main.jpg
    183.9 KB · Views: 38
..nitamwambia afuate ushauri ya Mzee Ibrahim Kaduma.

..alishauriwa atubu kwa makosa aliyofanya ktk kuuza NYUMBA ZA SERIKALI nchi nzima na kulitia taifa HASARA.

..zaidi azirudishe serikalini bila kuchelewa.
 
Ntamshukuru kwa kurudisha heshima kwa jamii.
NitaMwambia asante Rais sasa hivi tunaheshimiana mtaani.
ila kuna mchwa wamehamia kwenye fedha za miradi ya nje ya wafadhili. Wanazitafuna kwa safari uchwara za mikoani ili mradi wapate per diem. Namba mbili ningemsihi amwambie DG Kalinga, kuwa watumishi wa Umma hawana Cash ya mkupuo ya kununua Nyumba, pia kuwatuma wakakope Benki ni kuwatia umaskini wanapostaafu. Cash mane ya milioni mia kwa mkupuo ni ngumu. Nampenda Rais ni msikivu, kama alivyotatua suala la Wapangaji Wa MAGOMENI kota, atufikirie pia sisi watumishi wa Umma wanyonge wa kipato cha chini.
 
Nitamwambia asipende kuwatukana wenzake vilaz.a wakati yeye akitukanwa anawapeleka watu mahakamani.
Kuniita mi Kilaz.a kisa nawatetea wanafunzi wa UDOM waliotimuliwa aliniudhi sana.

Awache wapinzani wafanye kazi ya kueneza sera na kutafuta wanachama zaidi. Pia awaache wafanye vikao vya ndani. Nasikia polisi waliwahi kuvamia semina ya TRA wakidhani ni Ukuta.
 
Nitamshauri aruhusu taasisi za serikali ziendelee kuajiri baada kuzuiwa kwa miez mitatu sasa
 
Nitamwambia:
1. AMCHAGUE ZITTO ZUBERI KABWE KUWA.MSHAURI WAKE WA.UCHUMI.
2. ASANTE KWA KUMPA BINTI YANGU MKOPO.
3. MUNGU AMLINDE.
 
Nitampongeza kwa kuwakata maini waliozoea kuishi mijini kwa mishe mishe,na pia ningemuomba azikoromee mamlaka zilizolala usingizi wa pono mpaka kupelekea utitiri wa baa kwenye makazi ya watu na kusababisha kero na mmomonyoko wa maadili katika jamii.
 
MH RAIS AKIKUPA NAFASI YA KUONGEA NAE LEO JAPO KWA DAKIKA MOJA TU,

JE UTAMWAMBIA NINI? PAMOJA NA...PONGEZI,USHAURI HATA MAOMBI n.k

Angalizo..maneno ya staha ni muhimu.
Kwanza mimi nitamshukuru sana kwa uongozi wake!ameleta heshma sana kwenye hii nchi!!alafu nitamwambia ajaribu kumwiga yule wa korea kaskazini zile sheria zake.!!alafu atie saini wale wote wenye kutakiwa kunyongwa asaini wapigwe kitanzi!!
 
MH RAIS AKIKUPA NAFASI YA KUONGEA NAE LEO JAPO KWA DAKIKA MOJA TU,

JE UTAMWAMBIA NINI? PAMOJA NA...PONGEZI,USHAURI HATA MAOMBI n.k

Angalizo..maneno ya staha ni muhimu.
Nitamwambia kuwa Majiji makubwa hapa nchini, kama vile Dar, Arusha, Mbeya na Tanga, wananchi wa majiji hayo wamechagua Ukawa uongozi majiji hayo.

Kitendo cha serikali yake ya awamu ya 5, kuyawekea majiji hayo 'economic sanctions' ili kuwaadhibu wakazi wa majiji hayo kwa 'kosa' la kuwapiga chini CCM, ndiyo linazidi kuwatia hasira wakazi wa majiji hayo na kuyafanya majiji hayo katika chaguzi za siku za usoni, wananchi wasiweze tena kuichagua CCM kutokana na kuwaona kumbe siyo wana demokrasia kamili kwa kuwa kwenye demokrasia kuna kushinda na kushindwa.......

Cha kushangaza ni kuwa principle hiyo kuu ya demokrasia CCM hawaiamini kwa kuwa wanajiona wao kama ndiyo waliopewa hati miliki ya kuitawala nchi hii hadi mwisho wa dunia!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom