Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Tatizo Upinzani tulio nao unaombea Rais ashindwe ili wapate hoja... kifupi upinzani hasa Chadema ni kama hawana nia njema na nchi hii.

Upinzani umepoteza mwelekeo, sasa hivi wapo Nyuma ya Magufuli kazi yao ni kukosoa kauli za Magufuli tu.

Hawana sera za kulisaidia Taifa..... Nawapongeza ACT wazalendo kwa kujipambanua na kuanzisha mjadala kuhusu Katiba Mpya.

Wapinzani wanapaswa kubadilika sio kutafuta umaarufu wa mda mfupi.
 
Upo sahihi mkuu kabisa kama tukiendelea na siasa za umaarufu bila kuwa na sababu za msing kukosoa nguvu ya upinzani 2020 itakua ndogo sana nauna pia Kiongozi mkuu wa ACT naye kawa mtu wa kukosoa kila siku
 
="FaizaFoxy, post: 14507518, member: 43551"]Kwani Maalim Seif anatekeleza ilani ipi kama Makamu wa Rais wa Zanzibar?

FaizaFoxy,
Wewe unataka kuleta uchochezi kwa serikali ya Magufuli! Hivi wakti JPM alipotembelea Zanzibar hivi majuzi wewe ulikuwa wapi??
Je,hukusikia tamko lake akimshangaa Dk.Shein kuwaingiza Wapinzani kwenye serikali ya Mapinduzi? JPM aliweka wazi kuwa hataki kusikia habari ya wapinzani na hayuko tayari kuwashirikisha wala kushirikiana nao kwene serkali yake!!!!
Unaweza kuuliza mbona Mzee wa kiraracha Mrema yuko kwenye parole ya JPM?Ukweli ni kwamba Mrema ni pro-CCM au CCM-B! Mrema yuko upinzani lakini anafanya kazi za Serkali ya CCM!

Hivo wazo lako mama kwa Magufuli ni kama kumpigia mbuzi gitaa ukitegemea acheze!!!Pole sana.
 

Kasome tarehe ya huu uzi na hiyo post uliyoijibu wewe halafu linganisha na kituko ulichokileta.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Uso kwa Uso Na Mh Rais Maghufuli

Ikitokea Mh rais amekupa Nafasi ya kula nae Dinner

Je ungependa kumshauri nin Mh rais wakat mkipata Dinner...???
 
Ahakikishe sukari ya kiwanda cha Bakhresa inaachiwa huru mara moja. Pia Tanesco wafikishe umeme haraka sana. Tunataka juisi sisi.... tena kutoka kwenye kiwanda cha watanzania wa viwanda.
 
Hivi we unamjua Magufuli au unamsikia, huwa hapokei ushauri yule kwa hiyo hata sita hangaika kumshauri kwani hata kubali
Naskia yeye ndio huwa ana washauri washauri wake
 
Nitamcha live aache Kukurupuka.......

Aitafishe IPTL.,......

Afungulie Ajira kwa kuamasisha viwanda
 
Bi Faiza,
Uliyoyaandika ni kuntu. Huyu mama hata mimi nimekuwa nikimfuatilia sana na kwa maoni yangu amekaa kitaifa zaidi kuliko kichama.
 
Ustawi wa familia sio vitu vya kuwa-impress majirani tu wakati watoto wako wana-suffer utapiamlo, wanavaa matambara, likewise ustawi wa taifa.
 

Kazi kwelkwel
 
Mpendwa Rais wangu John Pombe Magufuli Nakusalimu katika jina la Bwana. Pole sana na majukumu mazito ya kuliongoza taifa letu. Mara nyingi nimekusikia ukitumia msemo mmoja unaosema MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU. Msemo ambao hata mimi hunigusa sana na kunifanya nihitaji kupata nafasi ya kuongea nawe ili japo kwa simu tu. Hakika wewe au kama si wewe wasaidizi wako naamini huwa mnasoma post za jamii forum. Hivyo basi naomba kama ukibahati kupita hapa naomba unipe nafasi ya kuongea na wewe ili nami niweze kukuambia jambo ambalo nihitaji kujisalimisha kwako. Maana Msema Kweli ni mpenzi wa Mungu. Nitafurahi endapo nitapata fursa hii ambayo naitamani sana.
 
Watanzania huu ni wakati Wa kumshauri Raisi wetu vitu muhimu ili nchi izidi kusonga mbele. Yeye ni msomaji mzuri Wa mtandao huu na huwa anapenda kuchukua ushauri pale anapoona inafaa kwa manufaa ya watu wote. So tujitokezeni kumshauri. Karibuni
 
Ushauri wangu kwa raisi ni kwamba, aruhusu bunge lirushwe moja kwa moja, mikutano ya kisiasa ya wazi, busara na hekima vitumike katika maamuzi na siyo ubabe. Neno la Mungu linasema hivi, ''heri wale wapatanishi maana wataitwa wana wa Mungu''. Awe mpatanishi na siyo mchonganishi hasa kwa suala la Zanzibar.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…