Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Tatizo Upinzani tulio nao unaombea Rais ashindwe ili wapate hoja... kifupi upinzani hasa Chadema ni kama hawana nia njema na nchi hii.

Upinzani umepoteza mwelekeo, sasa hivi wapo Nyuma ya Magufuli kazi yao ni kukosoa kauli za Magufuli tu.

Hawana sera za kulisaidia Taifa..... Nawapongeza ACT wazalendo kwa kujipambanua na kuanzisha mjadala kuhusu Katiba Mpya.

Wapinzani wanapaswa kubadilika sio kutafuta umaarufu wa mda mfupi.
 
Tatizo Upinzani tulio nao unaombea Rais ashindwe ili wapate hoja... kifupi upinzani hasa Chadema ni kama hawana nia njema na nchi hii.

Upinzani umepoteza mwelekeo, sasa hivi wapo Nyuma ya Magufuli kazi yao ni kukosoa kauli za Magufuli tu.

Hawana sera za kulisaidia Taifa..... Nawapongeza ACT wazalendo kwa kujipambanua na kuanzisha mjadala kuhusu Katiba Mpya.

Wapinzani wanapaswa kubadilika sio kutafuta umaarufu wa mda mfupi.
Upo sahihi mkuu kabisa kama tukiendelea na siasa za umaarufu bila kuwa na sababu za msing kukosoa nguvu ya upinzani 2020 itakua ndogo sana nauna pia Kiongozi mkuu wa ACT naye kawa mtu wa kukosoa kila siku
 
="FaizaFoxy, post: 14507518, member: 43551"]Kwani Maalim Seif anatekeleza ilani ipi kama Makamu wa Rais wa Zanzibar?

FaizaFoxy,
Wewe unataka kuleta uchochezi kwa serikali ya Magufuli! Hivi wakti JPM alipotembelea Zanzibar hivi majuzi wewe ulikuwa wapi??
Je,hukusikia tamko lake akimshangaa Dk.Shein kuwaingiza Wapinzani kwenye serikali ya Mapinduzi? JPM aliweka wazi kuwa hataki kusikia habari ya wapinzani na hayuko tayari kuwashirikisha wala kushirikiana nao kwene serkali yake!!!!
Unaweza kuuliza mbona Mzee wa kiraracha Mrema yuko kwenye parole ya JPM?Ukweli ni kwamba Mrema ni pro-CCM au CCM-B! Mrema yuko upinzani lakini anafanya kazi za Serkali ya CCM!

Hivo wazo lako mama kwa Magufuli ni kama kumpigia mbuzi gitaa ukitegemea acheze!!!Pole sana.
 
FaizaFoxy,
Wewe unataka kuleta uchochezi kwa serikali ya Magufuli! Hivi wakti JPM alipotembelea Zanzibar hivi majuzi wewe ulikuwa wapi??
Je,hukusikia tamko lake akimshangaa Dk.Shein kuwaingiza Wapinzani kwenye serikali ya Mapinduzi? JPM aliweka wazi kuwa hataki kusikia habari ya wapinzani na hayuko tayari kuwashirikisha wala kushirikiana nao kwene serkali yake!!!!
Unaweza kuuliza mbona Mzee wa kiraracha Mrema yuko kwenye parole ya JPM?Ukweli ni kwamba Mrema ni pro-CCM au CCM-B! Mrema yuko upinzani lakini anafanya kazi za Serkali ya CCM!

Hivo wazo lako mama kwa Magufuli ni kama kumpigia mbuzi gitaa ukitegemea acheze!!!Pole sana.

Kasome tarehe ya huu uzi na hiyo post uliyoijibu wewe halafu linganisha na kituko ulichokileta.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Uso kwa Uso Na Mh Rais Maghufuli

Ikitokea Mh rais amekupa Nafasi ya kula nae Dinner

Je ungependa kumshauri nin Mh rais wakat mkipata Dinner...???
 
Ahakikishe sukari ya kiwanda cha Bakhresa inaachiwa huru mara moja. Pia Tanesco wafikishe umeme haraka sana. Tunataka juisi sisi.... tena kutoka kwenye kiwanda cha watanzania wa viwanda.
 
Hivi we unamjua Magufuli au unamsikia, huwa hapokei ushauri yule kwa hiyo hata sita hangaika kumshauri kwani hata kubali
Naskia yeye ndio huwa ana washauri washauri wake
 
Nitamcha live aache Kukurupuka.......

Aitafishe IPTL.,......

Afungulie Ajira kwa kuamasisha viwanda
 
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mghwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.



















Bi Faiza,
Uliyoyaandika ni kuntu. Huyu mama hata mimi nimekuwa nikimfuatilia sana na kwa maoni yangu amekaa kitaifa zaidi kuliko kichama.
 
MH Rais. Nimeamka na neno moja tu lakukuambia nalo ni Usiogope.
Usiogope kusimamia yale una amini kwa ustawi wa taifa hili.
Usiogope vitisho vya watu wachache wenye nia mbaya na taifa hili.
Usiogope wanao tishia kujiuzulu kama wapo maana taifa hililitasimama hata kama wao hawatokuwepo. Umoja wetu nguvu zetu watanzania bara na visiwani tuna imani juu ya utendaji wa serikali yako.
Usiogope matajiri wachache ndani ya taifa hili ambao utajiri wao unaukakasi mzito wa dhuluma kwa watanzania.
Usiogope pesakukauka mtaani maana mtu asie fanya kazi na asile. Simamia nyia sahihi pesa irudi mtaani.
Usiogope wakurugenzi wachache wamabank wenye kutumika na mafisadi siku zao zinaesabika wala usihangaike nao.... Utawatambua kwa matendo yao
Usimuogope kiongozi fulani anaye endesha uwasi mzito bara na visiwani kwa kutamani angekuwa yeye Rais. Huyu ni chakula cha alie mleta duniani usipoteze nguvu kushindana nae maana ataadhibiwa ukimuona nawewe utakiri Mungu yupo.
Usiogope juu ya ulinzi wako maana unalindwa angani na ardhini na hakuna atakaye izima nyota yako ila Yeye alie kutuma.
Usiogope nasema usiogope maana hawa unawaona sasa hutowaona tena ktk miaka tisa na miezi ilio baki. Taifa hili limekusubira sana nasasa limepata baba mpaka misitu itabarikiwa. Usiogope!!!!!
Ustawi wa familia sio vitu vya kuwa-impress majirani tu wakati watoto wako wana-suffer utapiamlo, wanavaa matambara, likewise ustawi wa taifa.
 
kama aitoshi
Wizara ya kazi ilipiga marfuku watanzania kwenda kutumikishwa kama hgal..majuzi Niko airport madada wanne wamepita NA tkt zao

Mdada mmoja Yuki immigration pembeni anafanyakazi wizara ya kazi akawaita ..akawabana sana anataks laki mbilimbili kila MTU ndio awaachie

Ukwelii waliwapigia nduguzao wakawarushia kwabahati mbaya walikuwa NA lakimoja moja kila MTU akapewa..

Wale madada wakaachiwaa..ndugu MH Rais..MH waziri wakazi...Tunaombaa mpige marufuku kabisaa Hawa watoto kwenda kuwa mahgal NA wengi wanarudi wakilia walikuwa wanafanywa kinyume na maumbile

Nashauri serikali tuwe serious NA hili KUNA vijikampuni viko temeke NA kinondoni ndio wauzaji wakubwa wa Hawa mabinti mbaya wanaanzwa kwanza kutendwa ili wapate nafasi yakuondokw wakifika nje wanatendwa kinyume kabisa NA maumbile

Hawa n watanzania wenzetu tuwasaidie hatakama watuwanawafanya miradi..MH waziri husika ingilia kati

Hawaa mabinti no vitega uchumi vya WATU pale airport nannilivyokuwa nikiongea nao wanasema immigration wametoa lakilaki kila MTU NA yule mdada wa wizara yakazi nae karushiwa lakilaki kila MTU....

Tufike sasa tuwakomboe sisi wenyewe

Tunaomba serkli yako MH Waziri wa Kazi safishabwale mabinti wa airport NA muweke kitengo cha takukuru pale ili Hawa mabinti wasiwe watumwa huko nje

Kazi kwelkwel
 
Mpendwa Rais wangu John Pombe Magufuli Nakusalimu katika jina la Bwana. Pole sana na majukumu mazito ya kuliongoza taifa letu. Mara nyingi nimekusikia ukitumia msemo mmoja unaosema MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU. Msemo ambao hata mimi hunigusa sana na kunifanya nihitaji kupata nafasi ya kuongea nawe ili japo kwa simu tu. Hakika wewe au kama si wewe wasaidizi wako naamini huwa mnasoma post za jamii forum. Hivyo basi naomba kama ukibahati kupita hapa naomba unipe nafasi ya kuongea na wewe ili nami niweze kukuambia jambo ambalo nihitaji kujisalimisha kwako. Maana Msema Kweli ni mpenzi wa Mungu. Nitafurahi endapo nitapata fursa hii ambayo naitamani sana.
 
Watanzania huu ni wakati Wa kumshauri Raisi wetu vitu muhimu ili nchi izidi kusonga mbele. Yeye ni msomaji mzuri Wa mtandao huu na huwa anapenda kuchukua ushauri pale anapoona inafaa kwa manufaa ya watu wote. So tujitokezeni kumshauri. Karibuni
 
Ushauri wangu kwa raisi ni kwamba, aruhusu bunge lirushwe moja kwa moja, mikutano ya kisiasa ya wazi, busara na hekima vitumike katika maamuzi na siyo ubabe. Neno la Mungu linasema hivi, ''heri wale wapatanishi maana wataitwa wana wa Mungu''. Awe mpatanishi na siyo mchonganishi hasa kwa suala la Zanzibar.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom